Frank de Boer amefutwa kazi na klabu ya Inter Milan ya Italia baada ya kufanya kazi kwa siku 85 pekee ambapo ambapo ameshindwa mechi nne ligini.
Inter wamo nambari 12 kwa sasa Serie A baada ya kushindwa 1-0 Sampdoria Jumapili.
Hiyo ilikuwa mechi yao ya nne kushindwa katika mechi tano za ligi walizocheza chini yake msimu huu.
De Boer, mwenye myaka 46, alikuwa beki wa Uholanzi enzi za uchezaji wake na aliwahi kuwa mkufunzi wa Ajax.
Alihusishwa na kuhamia klabu za Everton na Southampton majira ya joto.
Inter watakutana na Southampton ligi ndogo ya Ulaya, Europa League siku ya Alhamisi.
Mkufunzi wa timu ya vijana Stefano Vecchi atakuwa kwenye usukani mechi hiyo.
Wakati wa uchezaji wake, alichezea Ajax, Barcelona, Galatasaray na Rangers.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire