Ukizungumzia kati ya studio zenye hits nyingi kwa sasa huwezi kuacha kuitaja Wasafi records iliyo chini ya WCB lebo ambayo wanatokea wakali kibao kama Diamond, Rich Mavoko, Harmonize, Ray Vanny na wengine kibao.
Lakini imekuwa ni mara chache sana kusikia studio hiyo ikifanya kazi na wasanii wengine tofauti na hao niliowataja kama tunavyoona kwenye studio nyingine ukiwatoa Dully Sykes, Shetta pamoja na Chege ambao nao wanachukuliwa kama ni wana familia ya WCB.
Nikafika mpaka WCB nikapiga story na producer wa studio hiyo anayefahamika kwa jina la Lizer ambaye aliniambia kuwa Wasafi Records ni kama studio zingine na msanii yeyote anaweza kwenda kufanya kazi na studio hiyo.
“kama studio zingine wanavyofanya nasi tunafanya hivyo hivyo pia. Msanii mwingine yeyote kutoka sehemu yoyote anaruhusiwa kuja kurekodi hapa. Hatuna bei kubwa sana bei yetu ni ndogo sana ukizingatia na studio ilivyo kubwa lakini bei yetu ni ndogo sana,” alisema Lizer.
NA EDWARD FABIAN
Bongo
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire