Google tag

mercredi 2 novembre 2016

Schweinsteiger aandika ujumbe huu kwa mashabiki wa Man United

Baada ya kufanikiwa kurudishwa kuanza kufanya mazoezi kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United, Bastian Schweinsteiger ameandika ujumbe wa kuwatia moyo mashabiki wa timu hiyo.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, kiungo huyo ambaye ni raia wa Ujerumani ameandika, “Felt great today! Team is in good shape, results will follow! @manchesterunited.”

Mchezaji huyo amekuwa na wakati mgumu ndani ya timu hiyo chini ya kocha Jose Mourinho akiwa mpaka sasa hajacheza mechi hata moja tangu msimu ulipoanza mwezi Agosti, mwaka huu.

Mara ya mwisho nahodha huyo wa zamani wa Ujerumani kuchezea timu yake hiyo ya United ilikuwa ni msimu uliopita wa mwezi Machi, mwaka huu akiwa chini ya kocha Louis Van Gaal aliyetimuliwa.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire