Google tag

lundi 28 novembre 2016

Hii ndio sababu ya timu ya Real Madrid kuvaa jezi za plastic dhidi ya Sporting Gijon

Klabu ya Real Madrid ya Hispania katika mchezo wao wa ligi kuu Hispania dhidi ya Sporting Gijon huku wakiwa wamevaa jezi zinazoangaza.

Jezi hizo zimetengenezwa na kampuni ya kijerumani ya Adidas, zimetengenezwa kwa kuyeyushwa plastiki laini iliyotokana na chupa zilizokuwa zimetupwa katika bahari ya Hindi, jezi moja inaripotiwa imetengenezwa kwa kutumia chupa 28.

Real Madrid na Adidas wametoa sababu ya kufanya hivyo huku wakishirikiana Parley ambao ni wanaharakati na utunzaji wa mazingira kama sehemu ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa kuacha kuharibu vyanzo vya maji.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire