Davido ameonyesha yeye si mtu wa mchezo mchezo. Staa huyo aliungana na wachezaji wa Chelsea kusherehekea ushindi wa timu hiyo walioupata dhidi ya Tottenham Hospurs wa mabao 2-1, Jumamosi iliyopita.
Hitmaker huyo wa How Long alifanikiwa kupiga picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo akiwemo Diego Costa, Eden Hazard, Victor Moses, David Luiz na César Azpilicueta.
Kupitia mtandao wa Instagram, muimbaji huyo ameandika, “GREAT
GAME!!@chelseafc ..”
Naye mchezaji wa timu hiyo Victor Moses ambaye ni raia wa Nigeria, ameandika kwenye mtandao wake wa Twitter, “What a feeling!So happy to get the win in such a big game.Thankful to score and help the team!Good to celebrate with @iam_davido too #CFC What a feeling!So happy to get the win in such a big game.Thankful to score and help the team!Good to celebrate with @iam_davido too #CFC.”
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire