Habari zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii siku ya jana iliripoti tukio la Model Juliana kufariki Dunia baada ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia (kubakwa).
(Picha iliyosambaa ikitaarifu tukio hilo)Lakini hali imekuwa tofauti baada ya taarifa zilizotolewa na akaunti moja ya Instagram inayojulikana kwa jina la Young_msafi ambayo imekanusha taarifa hizo.
Akaunti kiyo imeeleza kuwa aliyekutwa na ukatili huo hadi kupelekea kifo chake sio SALOME wa Diamond Platnumz bali ni model ambaye alikuwa Dancer wa chuo kikuu cha Mkumila.
Juliana amekutwa na mauti hayo usiku wa Jumatano ya tarehe 1/11/2016 baada ya Kutekwa wakati akiwa anakwenda kukutana na Marafiki zake kisha akateswa na kubakwa na watu wasiojulikana na kisha wakamtupa kichakani na mwili wake kuonekana asubuhi ya tarehe 2/11/2016.
Kupitia akaunti ya Instagram ya Ma-Model inayojulikana kwa jina la BLACKFOX_MODELS imethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa Misa ya maombezi itafanyika siku ya Jumapili katika ofisi zao.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire