Rapper wa Afrika Kusini, Cassper Nyovest amefanikiwa kutokea kwenye jarida la Forbes Africa Life.
Kupitia mtandao wa Twitter wa jarida hilo, wameandika, “@CassperNyovest started performing in front of a few people at school, 20 years later he’s filling up stadiums – @forbesafrica out NOW!.”
Naye Cassper ameonyesha furaha yake kwa kuandika kwenye mtandao wa Instagram, “Mama I made it!!! I made it on the Forbes Africa Life Cover!!!! All the glory to God!!! Black child , it’s possible!!! Go out there and do it for yourself!!! @forbesafrica out now!!!.”
Oktoba ya mwaka huu rapper huyo aliweka rekodi nyingine ya kuwa msanii wa kwanza wa Afrika kusini kuujaza mwenyewe uwanja wa mpira wa Orlando jijini Johannesburg kwenye show yake aliyoipa jina Fill Up Orlando Stadium.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire