Klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza imethibitisha kumuuza kiungo wao Oscar dos Santos kwenye timu ya Shanghai SIPG ya China.
Kupitia mtandao wa Twitter wa klabu hiyo umeandika, “Thank you, @oscar8 and good luck for the future.”
Mchezaji huyo alikuwa anawindwa kwa muda mrefu na timu hiyo ambayo iliahidi kulipa ada ya uhamisho wa paundi milioni 52 na kumlipa mshahara wa paundi laki nne kwa wiki na kumfanya awe mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani.
Naye mchezaji wa Boca Juniors ya Argentina anatazamiwa kujiunga na ligi hiyo ya China kwenye timu ya Shangahi Shenhua.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire