Klabu ya soka ya Leicester imeshinda tuzo ya timu bora ya mwaka kwa kuwashangaza wengi waliposhinda ligi ya Uingereza.
The Foxes kama inavyojiita ilishinda tuzo ya timu bora ya mwaka na mkufunzi wake Claudio Ranieri alitangazwa kuwa kocha bora baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda taji hilo.
Leicester ilianza kampeni ya kushinda taji hilo bila wengi kutarajia baada ya kushushwa katika ligi ya Uingereza mwaka 2014-15.
Walipoteza mechi tatu pekee katika msimu wa 2015-16 na wamefuzu kucheza kombe la vilabu bingwa Ulaya na kuendelea hadi raundi za muondoano.
Mwanzoni mwa mwezi Aprili, Leicester ilikuwa pointi saba juu katika jedwali la ligi ya Uingereza .
Mwaka mmoja kabla ,walikuwa chini ya jedwali hilo pointi saba pekee juu ya timu ambazo zilishushwa daraja.
Mwogeleaji wa Marekani Michael Phelps alishinda tuzo la mwanariadha bora wa olimpiki baada ya kushinda medali 23 za dhahabu.
Google tag
vendredi 23 décembre 2016
Leicester yashinda tuzo la klabu bora ya mwaka Uingereza
Inscription à :
Publier les commentaires (Atom)
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire