Chama cha soka nchini Uingereza FA kimemuadhibu kwa kumfungia mchezaji wa klabu ya Manchester City, Kun Aguero mechi nne baada ya kumchezea rafu beki David Luiz wa Chelsea Jumamosi iliyopita wakati timu hizo zilipokutana kwenye mchezo wa ligi kuu.
Wakati huo huo chama hicho kimemuadhibu kiungo Fernandinho kutocheza mechi tatu baada ya kumkaba kooni na kumsukuma hadi chini kiungo Cesc Fabregas.
Kwenye mechi hiyo Chelsea ilifanikiwa kuifunga Man City mabao 3-1 na kuendelea kuongoza kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na jumla ya pointi 34 wakifuatiwa na Arsenal yenye pointi 31 huku Man City wakishuka hadi kwenye nafasi ya nne wakiwa na jumla ya pointi 30.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire