Google tag

lundi 5 décembre 2016

Iko wapi zamani

*IPO WAPI ZAMANI?*

✏ Zamani nyumba zetu zilikua vyumba kidogo na sehemu ya kukaa tu, tunakutana ndugu, jamaa na majirani.

✏ Lakini leo nyumba zetu kubwa na zina vyumba vingi, isipokuwa hazina watu ila ardhi na kuta tu.

✏ Huyu kasafiri na yule kajilipuwa nchi nyengine, huyu kakasirika haongei na mtu na mwengine yupo hoi  na dunia.

✏ Zamani chakula chetu ni wali, mihogo, ndizi, majimbi, dagaa la kitonge, au ugari kwa chukuchuku.

✏ Tunatandika mkeka au jamvi chini na tunakula sahani moja sote, tunacheka kwa furaha mpaka jirani wanatusikia.

✏ Lakini leo hii sufuria au hotpot  imejaa nyama, kuku na minofu ya samaki na kila mmoja na sahani yake  ya aina tofauti .

✏ Basi mnakaa sehemu zipo tupu, unatamani ndugu au jirani wawepo, wazibe hilo pengo.

✏ Zamani tunakaa uwani na babu, anatuhadithia hadithi, tunakunywa chai kwa upendo na kucheka kwa pamoja kwa tabasamu mpaka meno yetu yanaonekana.

✏ Na leo kukaa kwetu ni kwenye simu za mkononi, internet na kuchat tu kwenye whatsapp, wechat, instagram, facebook na mitandao mengine ya kijamii, tumekua tupo kwingine kabisaa.

✏ Zamani tunauliziana, kujuliana hali, kutembeleana,  na tunakutana kwa furaha na kukumbatiana.

✏ Leo ni sikukuu mpaka sikukuu au harusi had harus au mpaka kuwe na maziko ndio tunatembeleana au kuonana tena kwa kujilazimisha, hata salaam ya mungu hatusalimiani, na kukaa kwetu kwa mioyo ya moto.

✏ Zamani mtu akiumwa kati yetu, tunakusanyika ndugu na majirani.

✏ Leo ndugu hakujali, hana muda na wewe na anakwambia niwahi mimi taabani hoi.

✏ Zamani ilikua ndugu anamuenzi ndugu yake na dada yake, kwa kila alichonacho hata kama kachoka au ana stress.

✏ Leo unamkuta mtu hapati kula na ndugu yake yupo kazama katika neema, anajifanya kakasirika kwa sababu za kijinga, na kukata mawasiliano kwa miaka.

✏ Leo pesa inabadili nafsi ya mtu, hajali ndugu wala jirani, utu unapotea anasahau kama kuna kufa au dunia ina mwisho .

✏ Mpo wapi watu wa zamani mje muone vipi mioyo imefanya kati ya ndugu leo hii..!!??

✏ Miaka na siku hazirudi nyuma, tenda wema uende zako usingoje shukrani.

✏ Unasaidia ndugu au mtu shukrani yake katika ulimi tu, lakini moyoni mwake kuna moto anasahau ihsani na kukusema kwa vibaya mno.

✏ Hamna tena undugu wa kuwakusanya pamoja kama zamani, hamna mapenzi na upendo ndani ya mioyo, (Hata heshima kwa mkubwa kama zamani hamna).

✏ Iko wapi zamani? Mola awarehemu wa zamani waliotangulia.
Allah atujaliye tuwe wenye kupendana na kushikamana kwa kila hali kama ilivyokuwa zamani.

*UMOJA WETU NDIO UNDUGU WETU*

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire