Alibaba

mardi 6 décembre 2016

Manchester City na Chelsea kushtakiwa na FA

Timu za Manchester City na Chelsea zimeshtakiwa na FA kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wao wakati wa mechi ya Ligi ya Premia iliyochezwa Jumamosi.

Mashtaka hayo yanatokana na mfarakano wa wachezaji uliozuka dakika ya 95 wakati wa mechi hiyo iliyochezewa Etihad ambapo Chelsea walishinda 3-1.
Mshambuliaji Sergio Aguero na kiungo wa kati Fernandinho walitolewa uwanjani, lakini kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas hatachukuliwa hatua.
Kocha wa City Pep Guardiola aliomba radhi kwa kitendo hicho kwa timu yake katika kisa hicho.
Aguero amepigwa marufuku kucheza mechi nne kutokana na kisa chake hicho.

Fernandinho walikabiliana na Fabregas baada ya kosa hilo na Mbrazil huyo atatumikia adhabu ya kukosa mechi tatu.
Klabu zote zimepewa hadi saa 18:00 GMT mnamo 8 Desemba kujibu mashtaka hayo.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire