Klabu ya Chapecoense kutoka Brazil, ambayo
iliwapoteza wachezaji 19 pamoja na wahudumu
kwenye ajali ya ndege walipokuwa wakielekea
kucheza fainali ya Copa Sudamericana,
imetunukiwa kombe hilo.
Uamuzi huo umechukuliwa na shirikisho la soka
la Amerika Kusini, Conmebol kufuatia ombi la
wapinzani wa klabu hiyo.
Watu 71, wakiwemo wachezaji 19 na wahudumu
wa klabu hiyo, walifariki Jumatatu wakielekea
Colombia kwa mechi ya mkondo wa kwanza ya
fainali ya kombe hilo.
Wapinzani wa klabu hiyo kutoka Atletico
Nacional, ambao waliomba Chapecoense
wapewe kombe hilo, wametunukiwa tuzo ya
Uchezaji Haki ili kutambua "moyo wao wa amani,
kuelewa na kucheza haki".
Chapecoense pia watapewa jumla ya $2m
(£1.57m) ambazo hukabidhiwa mshindi.
Atletico Nacional nao watapewa $1m
(£787,000).
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire