Wizkid anakabiliwa na kifungo cha miaka 11 jela, baada ya mahakama ya Uganda kutoa hati ya kukamatwa kwake na meneja wake, Sunday Aare.
Wizkid alishindwa kutokea kwenye show iliyokuwa ifanyike December 3 mwaka huu mjini Kampala. Kampuni iliyomlipa, Face TV, kupitia mwanasheria wake, Fred Muwema, imepata kibali cha kumkamata muimbaji huyo kwa kuchukua dola $60,000 na kushindwa kutokea kwenye show. Gharama zingine walizotoa ni brokerage fee, $5,000 na per die, $3,000 kwa muda ambao Wizkid angekaa Uganda.
Muimbaji huyo alidaiwa kushindwa kusafiri na ndege toka Marekani kwenda nchini humo kwa show hiyo.
“Between 29th August 2016 and 29th November 2016, our
client (Face TV) paid to Mr. Sunday Are, Wizkid’s manager the full
performance fee of US$60,000, a brokerage fee of US$5,000 and US$3,000
being per diem for the days they were going to stay in Uganda,”
yanasomeka maelezo ya mlalamikaji.
Zaidi ya watu 25,000
walikuwa wamenunua tiketi kwaajili ya show hiyo. Maelezo
yaliyowasilishwa mahakamani yameeleza kuwa mwandaaji wa shiw hiyo
amekula hasara ya zaidi ya $300,000 kutokana na maandalizi aliyofanya.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire