Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa ''hatosoma'' kitabu ambacho mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amesema atauvunja uso wa kocha huyo wa Arsenal.
Mourinho amekuwa akizozana na Wenger alipokuwa akiifunza Chelsea na alimuita mkufunzi huyo ''maalum kwa kushindwa''.
''Mimi huzungumza kuhusu soka-hicho ndio ninachofanya'',alisema Wenger mwenye umri wa miaka 66.
''Siko katika hali ya kutaka kuharibu,mimi hupenda kujenga.Ninaangazia mechi ya Jumamosi dhidi ya Chelsea''.
Mourinho mwenye umri wa miaka 53 alimuita Wenger ''mpiga chabo'' mwaka 2005 baada ya kutaka kujua kuhusu sera za uhamisho za Chelsea.
Raia huyo wa Ureno alimuita Arsene Wenger ''mtu maalum kwa kushindwa'',mnamo mwezi Februari 2014 baada ya raia huyo wa Ufaransa kusema kuwa baadhi ya wakufunzi wa ligi kuu ya Uingereza wameanza kulalamika kwa sababu ''wanahofia kufeli''.