Alibaba

samedi 8 octobre 2016

Cheka Kidogo

Jamaa wawili waliiba Maembe kiroba kizima wakakimbilia mochwari chumba cha kuhifadhi maiti bila yamlinz kujua, wakati wanaingia wakaangusha Embe 2 mlangoni,

mlinz alipotoka usingizin akasikia jamaa wanagawana hii yako hii yangu..... Hii yako hii yangu.... Mlinzi akakimbia kumwita doctor
njoo usikie malaika na ibilisi wanagawana roho,

walipofika tu wakasimama mlangoni wakawasikia wanasema na zile mbili zilizoko mlangon twende tukazichukue, doct kusikia hvyo akadhan wanakuja kuchukua Roho zao docta na mlinzi wakatimua mbio.

Dokta na mlinzi sio watu wa mchezo mchezo 😀😀👆🏿

Powered by Chief pro

Neymar avunja rekodi Brazil kwa damu

Superstar wa Barcelona Neymar Jr ameendeleza rekodi yake ya kupachika mabao kwenye timu yake ya taifa wakati Brazil ikiichapa Bolivia kwa bao 5-0 kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Neymar alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 11 na ku-assist magoli mengine mawili katika kikosi cha Tite.

Goli lake dhidi ya Bolivia lilivunja rekodi ya Zico na sasa amekuwa mchezaji wa nne mwenye magoli mengi kwenye historia ya timu ya taifa ya Brazil akiwa ameshafunga magoli 49.
Wachezaji watatu wa juu yake ni Romario (55), Ronaldo (62) na Pele (77).

Lakini mchezo huo haukumalizika salama kwa upande wa Neymar baada ya kupigwa kiwiko na mchezaji wa Bolivia Yasman Duk.
Neymar alijikuta akichezea ‘kipepsi’ wakati alipojaribu kumpiga ‘tobo’ Duk lakini beki huyo wa Bolivia akampiga kiwiko cha usoni nyota wa klabu ya Barcelona lakini mwamuzi hakuamua tukio hilo liwe ‘faulo’

Damu nyingi ilitoka usoni kwa Neymar ambaye alishindwa kuendelea na mchezo na kupelekea kupumzishwa halafu nafasi yake ikachukuliwa na kiungo mshambuliaji wa Chelsea Willian.

Rekodi za Argentina ikiwa na Messi na bila Messi kufuzu Kombe la Dunia

Miamba ya soka la bara la Amerika ya Kusini timu ya taifa ya Argentina ililazimishwa sare ya pili mfululizo na Peru kwa kufungana magoli 2-2 ikiwa imetoka kupata matokeo kama hayo mwezi uliopita dhidi ya Venezuela.
Wakati Lionel Messi akiwa nje ya uwanja akiuguza majeraha, kocha wa Argentina Edgardo Bauza aliwaita washambuliaji wanne kwenye kikosi chake wakiongozwa na Angel Di Maria, Sergio Aguero, Paulo Dybala pamoja na Gonzalo Higuain.
Licha ya kuwa na safu kali ya washambuliaji wenye vipaji, Argentina imeshindwa kutetea ushindi wake katika mechi mbili ambapo ililazimishwa sare licha ya kuwa mbele ya wapinzani wake kwa mabao. Kwa sasa inakamata nafasi ya tano kwenye kundi lake la kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.

Argentina ikiwa na Messi na bila Messi

Nyota huyo wa Barcelona mwenye miaka 29 alishawishiwa kurejea kwenye timu ya taifa baada ya kutangaza kustaafu kufatia kuchapwa kwa mara ya pili mfululizo kwenye fainali ya Copa America na timu ya taifa ya Chile.
Rekodi ya Argentina ikiwa na Messi na ikiwa bila Messi inaonesha kuna tofauti kubwa kwasababu katika mechi 6 za Argentina bila Messi imeweza kupata ushindi kwenye mchezo mmoja pekee wakati imeweza kupata ushindi kwenye mechi tatu ambazo Messi alicheza.