Alibaba

samedi 14 janvier 2017

AFCON: Matukio sita makuu historia ya Kombe la Mataifa Afrika

Michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, makala ya 31, itang'oa nanga Jumamosi 14 Januari pale wenyeji watakapokabiliana na Guinea-Bissau ambao wanashiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza.
Kwa baadhi ya mashabiki, hii ni michuano tu ya kawaida ya soka.

Lakini AFCON kwa sasa ni michuano yenye ushindani mkali na yenye wachezaji nyota kama vile Riyad Mahrez, Sadio Mane na Pierre-Emerick Aubameyang.

Michuano hii inapong'oa nanga, tunaangalia matukio muhimu ya furaha na ya kusikitisha pia ambayo hayasahauliki katika historia ya AFCON.

1994: Zambia yajikwamua baada ya mauti

 Mnamo 27 Aprili 1993, timu ya taifa ya Zambia ilikuwa safarini mechi ya kufuzu Kombe la Dunia nchini Senegal ndege iliyowabeba ilipoanguka na kutumbukia baharini mita 500 kutoka mji wa Libreville, Gabon.
Abiria wote 25 waliangamia pamoja na wahudumu watano.
Mwaka mmoja baadaye, Zambia ilijijenga na kufana sana michuano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika 1994. Walifika fainali ingawa walishindwa na Nigeria 2-1.

2012: Herve Renard asaidia Zambia kutwaa kombe


Herve Renard and Zambia win the Africa Cup of Nations in 2012Getty Images
Zambia walikosa ushindi fainali 1994 lakini walifanikiwa 2012 chini ya kocha wao Mfaransa Herve Renard ambapo walikabiliana na Ivory Coast fainali.
Kwenye mechi hiyo, kulipigwa mikwaju 18 ya penalti, na Zambia wakashinda 8-7.

2015: Morocco yajiondoa kwa sababu ya Ebola

 

 

Kutokana na kuenea kwa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi, wenyeji waliopangiwa kuandaa michuano ya 2015 Morocco walijiondoa wakihofia michuano hiyo ingefikisha ugonjwa huo nchini mwao.

CAF ilikataa ombi la kujiondoa, na baada ya Morocco kusisitiza timu yake ikafurushwa kutoka kwa michuano hiyo.
Mataifa matano yalikataa kuwa mwenyeji kabla ya Equatorial Guinea kukubali. Ivory Coast waliibuka washindi kwa kulaza Ghana 9-8 kupitia mikwaju ya penalti.

2010: Basi la Togo lashambuliwa

Basi la timu ya Togo lilishambuliwa na watu wenye silaha timu hiyo ilipokuwa ikirejea kambini Angola.
Kundi moja la waasi kutoka eneo la Cabinda lilikiri kuhusika

Watu watatu waliuawa na wengine tisa kujeruhiwa. Nyota wa zamani wa Arsenal na Manchester City Emmanuel Adebayor ni miongoni mwa waliokuwa kwenye basi hilo.
Togo ilijiondoa kutoka kwa michuano hiyo.

2006 & 2012: Drogba ashindia amani Ivory Coast

Mshambuliaji wa Ivory Coast Didier Drogba alikuwa stadi sana uwanjani kwa taifa na Chelsea na pia alitumia hadhi yake kufanikisha amani nchini mwake.
Wakati wa vita kati ya 2002 na 2007, alipiga magoti moja kwa moja kwenye runinga akiwa na wachezaji wenzake 20045 kuwahimiza waliokuwa wanapigana kuweka chini silaha.

Kipindi cha amani kilifuata. Mwaka 2008, alisisitiza mechi ya kufuzu Kombe la Taifa Bingwa Afrika dhidi ya Madagascar ichezewe ngome ya zamani ya waasi Bouake kama wito kwa raia kuungana.
Mwaka 2006 na 2012, Drogba alisaidia taifa lake kufika fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika lakini wakashindwa kwa mikwaju ya penalti.
Hata hivyo, hakufanikiwa kushinda.

2002 & 2004: Jezi za Cameroon

Cameroon walishinda michuano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika 2002 kwa kulaza Senegal kupitia mikwaju ya penalti kwenye fainali.

Lakini kinachokumbukwa sana ni jezi za Simba Wasioshindwa ambazo zilikuwa hazina mikono.
Fifa hata hivyo waliwazuia kuzivalia wakati wa Kombe la Dunia 2002.
Mwaka 2004 walikuwa na jipya tena. Walivalia jezi moja iliyoshikana - fulana na kaptura nchini Tunisia.
Fifa hawakufurahia, na ikizingatiwa kwamba walikiuka ahadi ya awali ya kuzitumia kucheza mechi za makundi pekee,
Fifa waliwapiga faini kwa kucheza mechi ya robofainali ambayo walishindwa na Nigeria.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire