Google tag

samedi 14 janvier 2017

El Salvador yafurahia kumaliza siku bila mauaji

Polisi nchini El Salvador wanasema taifa hilo la Amerika ya Kati limemaliza siku moja bila mauaji yoyote kuripotiwa, jambo ambalo ni nadra sana katika taifa hilo.
El Salvador, taifa ambalo limeathiriwa sana na mapigano ya magenge ya wahalifu, ina mojawapo ya viwango vya juu zaidi vya mauaji duniani kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Watu 10 walikuwa wameuawa, mmoja kila siku mwaka huu nchini humo hadi kulipotokea Jumatano yenye utulivu wiki hii.
Mengi ya mauaji hutekelezwa na magenge ya uhalifu, ambayo hufahamika sana kama maras, ambayo huendesha shughuli zake maeneo mengi ya Amerika ya Kati.


Polisi hawajatoa maelezo yoyote kuhusu nini labda kilisababisha kutotokea kwa mauaji siku hiyo ya Jumatano.
Lakini serikali imekanusha madai kwamba imeamua kuanza kufanya mazungumzo ya kusitisha vurugu na magenge hayo.

Magenge hayo ya uhalifu mwanzoni yaliundwa kwenye barabara za mji wa Los Angeles miaka ya 1980 na watoto wa wahamiaji kutoka El Salvado waliokuwa wametoroka vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Vita vilipomalizika mwaka 1992, wengi wao walirejea nyumbani na utamaduni huo wa uhalifu.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire