Siku hizi katika soka tunaona jinsi gani msisitizo mkubwa ukizingatiwa kwa Magolikipa kuwa na uhitaji wa kuweza kutumia miguu yao vizuri kwenye kuanzisha mashambulizi ( Modern Goalkeeping )
Kuanzia kwa Victor Valdes ndani ya Barcelona ya Pep Guardiola mpaka Manuel Neuer akiwa Bayern Munich na timu ya Taifa ya Ujerumani na sasa ndio imekuwa utamaduni.
Katika vikosi viwili Liverpool na Manchester City kuna Magolikipa wawili wa kimataifa wa Brazil ambao timu zao zinapata faida kubwa sana pindi wanapoanza mashambulizi kutoka nyuma , hata wakiwa wanashambuliwa wanageuka kuwa ‘ Sweepers ) hiyo inasaidia timu zao kuanza kukabia juu ya uwanja .
Lakini swali kubwa baina ya Ederson Moraes na Alisson Becker ni Golikipa yupi yupo bora zaidi ya mwenzake wakiwa na mpira mguuni ? ( wote wazuri lakini nani bora zaidi ya mwenzake )
A: Alisson Becker
B: Ederson Moraes
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire