Google tag

lundi 23 décembre 2019

Cavani Kutua Atletico:



Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay Edinson Cavani amekubali mkataba wa miaka mitatu kujiunga na Atletico Madrid mwezi Januari 2020


Cavani mkataba wake na PSG unafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu. 

Tuzo barani Afrika


Wana fainali watatu walioteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka barani Afrika 

1: Mo Salah 
2: Riyad Mahrez
3: Sadio Mane 



Mshindi atatangazwa siku ya Jumanne , Tarehe 07 Januari 2020 , Hurghada, Egypt.

Flick kuendelea kuinoa Bayern.


Klabu ya Bayern Munchen imethibitisha, kocha wa muda Hansi Flick ataendelea kuinoa klabu hiyo hadi mwishoni mwa msimu huu wa 2019/20.


Rekodi ya Thierry Henry , EPL

Gwiji wa klabu ya Arsenal Thierry Henry ndio mwanaume pekee aliyefanikiwa kuwa na assists 20 katika msimuy mmoja wa Ligi alifanya hivyo msimu wa 2002/03 mpaka sasa hakuna kiumbe aliyewahi kufikia.

Je msimu huu inaweza kuvunjwa ?? Kiungo mshambuliaji wa Man City Kevin De Bruyne jana baada ya kutengeneza goli amefikisha assists 10 msimu huu mpaka zikiwa zimepigwa mechi 17 , zimebaki mechi 21 . Ataweza kutengeneza magoli 10 mengine katika mechi 21 zilizobaki ??