Google tag

jeudi 26 décembre 2019

Vita ya Technique Kutoka kwa Samba Boys



Siku hizi katika soka tunaona jinsi gani msisitizo mkubwa ukizingatiwa kwa Magolikipa kuwa na uhitaji wa kuweza kutumia miguu yao vizuri kwenye kuanzisha mashambulizi ( Modern Goalkeeping )

Kuanzia kwa Victor Valdes ndani ya Barcelona ya Pep Guardiola mpaka Manuel Neuer akiwa Bayern Munich na timu ya Taifa ya Ujerumani na sasa ndio imekuwa utamaduni. 



Katika vikosi viwili Liverpool na Manchester City kuna Magolikipa wawili wa kimataifa wa Brazil ambao timu zao zinapata faida kubwa sana pindi wanapoanza mashambulizi kutoka nyuma , hata wakiwa wanashambuliwa wanageuka kuwa ‘ Sweepers ) hiyo inasaidia timu zao kuanza kukabia juu ya uwanja . 

Lakini swali kubwa baina ya Ederson Moraes na Alisson Becker ni Golikipa yupi yupo bora zaidi ya mwenzake wakiwa na mpira mguuni ?  ( wote wazuri lakini nani bora zaidi ya mwenzake ) 

A: Alisson Becker 
B: Ederson Moraes

Mzee aiba pesa na kuzitoa kama zawadi akisema 'Merry Christmas'

Bwana mmoja mwenye ndevu nyeupe alifanya uvamizi wa benki siku mbili kabla ya Krismasi na kuzirusha juu kwa furaha na kuwatakia kheri ya siku kuu wapita njia, mashuhuda wameeleza.
Polisi wamethibitisha "mwanaume mzee wa kizungu" alivamia benki ya Academy mjini Colorado Springs, Marekani siku ya Jumatatu.


"Aliiba pesa benki, akatoka nje na kuzitawanya kwa watu," shuhuda Dion Pascale alikiambia kituo cha Colorado 11 News.
"Alianza kurusha fedha kutoka kwenye begi na kisha akaanza kusema, 'Merry Christmas!'"
Kwa mujibu wa mashuhuda, mtuhumiwa huyo akapiga hatua chache kutoka benki na kuketi mbele ya mkahawa wa Starbucks akisubiri kukamatwa.
Katika hali ambayo inaweza kuwa ya kustaajabisha kwa wakazi wa Afrika Mashariki, wapita njia wanaripotiwa kuwa walichota fedha zote zilizozagaa na kuzirudisha benki.
Polisi wamemtaja mtuhumiwa huyo kwa jina la David Wayne Oliver, mwenye miaka 65 .
Polisi hawadhani kuwa alikuwa na usaidizi wowote.