Carlos Simeone, baba mzazi wa kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone amefariki Dunia siku ya Ijumaa Machi 25.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Klabu hiyo Mzee Carlos Simeone (80) ambaye pia alikuwa babu wa mshambuliaji wa Atletico Madrid B Giuliano amefariki jana Ijumaa katika Jiji la Buenos Aires nchini Argentina.
Katika kumkumbuka Bendera katika uwanja wa Wanda Metropolitano itapepea nusu mlingoti.
Klabu mbalimbali na wachezaji wametuma salamu zao za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire