Google tag

dimanche 27 mars 2022

Masta ya AY nooma saaana

AY AACHIA MASTA “HUWA NATABASAMU NIKITAZAMA ZILE TUZO ZA MTV, WALINIWEKA KUNDI MOJA KANYE NA JAY Z”


Hayo ni mashairi ya ngoma mpya ya mkongwe kwenye game @aytanzania wimbo unaitwa Masta.

Rapa huyo wa kiwango cha hali ya juu ameachia video ya wimbo huo akiwa na @sir_nature huku ndani yake ukiwa na madini mengi.


AY kwenye Masta ametaka kuonyesha miaka yake 22 kwenye game ya muziki ikiwa ni safari yenye mafanikio mengi katika muziki wa Tanzania.

Katika video zimeonekana video za nyimbo zake za zamani pamoja na matukio makubwa yakikamii aliyoyafanya.

Juma Nature

Katika ngoma hii mkongwe @sir_nature amepita na chorus katika viwango vyake vilivyowahi kupendwa zaidi. Mastaa wengine walionekana kwenye video ni @johmakinitz , @naytrueboytz , @mhtemba na mengine.

Una mtazamo gani juu ya project hii mpya ya Ay ndani ya mwaka 2022?

Video hiyo unapatikana YouTube kupitia link iliyopo kwenye bio yake.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire