Wachezaji wa PSG ya Ufaransa Neymar na Gianluigi Donnarumma inaelezwa kuwa walizozana vikali hadi kupelekea kupigana kwenye vyomba vya kubadilishia nguo na hii yote ni baada ya PSG kushindwa kushinda mbele ya Real Madrid katika mchezo wa pili wa michuano ya Ligi ya Mabingwa ULAYA UEFA.
Kwa mujibu wa gazeti la Marca, mzozo huo ulianza uwanjani pale mshambuliaji huyo wa Brazil alipomtuhumu mlinda mlango huyo wa Italia kuwa alifanya kosa la kipuuzi lililopelekea bao la kusawazisha la Real Madrid dhidi ya Paris.
Tayari baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, ilipobainika kuwa wababe hao wa Ufaransa wametolewa kwenye mashindano, mapigano kati ya wachezaji wa timu yaliendelea kwenye chumba cha kubadilishia nguo.
Neymar inaelezwa alimlauma Donnarumma kuwa alifanya kosa la kipuuzi huku mlinda mlango huyo naye akimtuhumu Neymar kufanya kosa la kipuuzi pia baada ya kupoteza mpira mbele ya modric na kushindwa kumpokonya hadi kupelekea goli la pili kufungwa na Benzema.
PSG wametupwa nje ya michuano ya UEFA baada ya kupokea kichapo cha goli 3-1 katika dimba la Bernabu na kufanya jumla ya magoli 3-2 baada ya mchezo wa kwanza Real Madrid kupoteza goli 1-0 dhidi ya PSG. magoli yote ya PSG yakifungwa na Benzema huku magoli ya PSG yakifungwa na Mbappe.
Timu ambazo tayari zimetinga robo fainali ya UEFA ni Liverpool, Bayern Munich, Manchester City, na Real Madrid bado michezo minne ambayo ni Manchester United vs Atletico Madrid, Chelsea vs Lille, Ajax vs Benifica na Juventus vs Villareal.
Fainali za UEFA mwaka huu zitafanyika katika uwanja wa Stade de France ulipo jijini Paris ambao ni uwanja wa taifa la Ufaransa mnamo tarehe 28 mwezi wa tano na hii yote ni baada ya uwanja kubadilishwa kutoka St, Petersburg Urusi kutokana na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire