Google tag

jeudi 20 octobre 2022

Aonesha uchi wake ili kuziwiya Free kick

Beki wa Klabu ya Independiente Santa Fe ya nchini Colombia, Geisson Perea amewaacha mashabiki kwenye mshangao mkubwa baada ya kufanya kitendo kisicho cha kawaida katika mchezo wao dhidi ya Jaguares de Cordoba wikiend ya Oktoba 17, 2022.


Geisson Perea akiwa sehemu ya ukuta wa mabeki kuzuia mpira wa adhabu (free-kick) uliyokuwa sehemu ya hatari zaidi karibu na lango la goli lao, aliamua kutoa nje sehemu zake za siri ili kumchanganya mpigaji wa mpira bila mwamuzi kuona tukio hilo lililonaswa na kamera za uwanjani.


Kitendo hiko kimetafsiriwa kama njia ya kumchanganya mpigaji wa mpira huo uliyokuwa umetengwa na mwamuzi kuelekea katika milingoti mitatu ya timu yake.

Kupitia Win Sports TV, Geisson Perea amesema kuwa lengo lake lilikuwa ni kuiweka sawa bukta yake na sio kujiweka hadharani kwa ulimwengu. Hakufahamu pia kuwa kamera zilikuwa zikimmulika yeye.

Kwa mujibu wa Dailymail mashabiki wametaka mchezaji huyo apatiwe adhabu kali kutokana na kitendo hicho ambacho ndani ya uwanja hakupatiwa kutokana na mwamuzi kutokuona kilichotokea.


Hata hivyo beki huyo mwenye umri wa miaka 31 hakuisaidia timu yake kuepukika na kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya Jaguares.

lundi 17 octobre 2022

Kuna Wachezaji mashoga EPL

Mwanasoka wa zamani wa England ambaye kwa sasa ni Mtangazaji wa michezo Gary Lineker (61), amedai kuwa anawajua wachezaji wawili wa Ligi ya England ambao ni mashoga na anatumani kuwa watajitokeza hivi karibuni.


”Huu ndio wakati mwafaka, wakati tunakaribia Kombe la Dunia,mjitokeze mtetee msimamo wenu ”

Akizungumza na gazeti la Daily Mirrow, Lineker alisema “Ninajua kwa uhakika kabisa kuwa hawa watu walikuwa karibu sana kujitokeza, ninawajua ni wapenzi wawili, lakini siwezi kuwataja,”

”Hofu ya Mashabiki na ukosoaji kutoka kwa wachezaji wenzao ndio unawafanya wengi wajifiche, na kubaki wakiishi maisha ya uwongo,”

”Ninajua ni ngumu sana, lakini nilikuwa natamani mjitokeze tu, sababu najua mpo, ni dhahiri kuna wachezaji wengi ambao wanalazimika kuishi kwa uwongo.”

Kombe la Dunia litafanyika mwezi ujao nchini Qatar ambako kutokana na sheria kali za Kiislamu mahusiano ya jinsia moja hayakubaliki na hukumu yake ni kifo.

samedi 8 octobre 2022

Type C lazima Ulaya

Moja kati ya habari kubwa Wiki hii ni hii ya Bunge la Ulaya kupitisha sheria mpya ambazo zitaanzishwa katika nchi za Umoja wa Ulaya, ambazo zinawalazimu Watumiaji na Watengenezaji wa vifaa vyote kama vile smart phones, vishkwambi, camera nk kutumia charger aina ya type c ifikapo mwaka 2024, hili likiwa ni jambo la kwanza duniani ambalo linatarajia kumuathiri Mtengenezaji wa simu za iPhone na Apple zaidi ya Wapinzani wake.


Kura hiyo inathibitisha makubaliano ya awali kati ya Taasisi za Umoja wa Ulaya kuifanya USB aina ya C inayotumiwa na vifaa vinavyotumia Android kuwa kiwango pekee cha Umoja wa Ulaya na hivyo kuilazimu Kampuni kutokea nchini Marekani Apple (AAPL.O) kubadilisha sehemu zake za kuchajia simu za iPhone na vifaa vingine.




Wachambuzi pia wanatarajia matokeo chanya kwa sababu inaweza kuwahimiza Watu kununua vifaa vilivyotolewa hivi karibuni vya kampuni hiyo, badala ya vile visivyo na USB-C.



Makubaliano haya pia yataathiri vifaa vya kusomea, na teknolojia nyinginezo, kumaanisha kuwa huenda pia mabadiliko hayo yakaathiri kampuni ya Samsung pamoja na Huawei.