Google tag

samedi 26 mars 2022

Huenda Lionel Messi akastaafu soka la Kimataifa

Huenda Lionel Messi akastaafu soka la Kimataifa baada ya Kombe la Dunia baadae mwaka huu na huenda mchezo wa usiku wa kuamkia leo wa Argentina dhidi ya Venezuela ukawa ndio mechi yake ya mwisho katika ardhi ya nyumbani.


Argentina iliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Venezuela huku Messi akiwa mmoja wa wafungaji.

Mess katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi alisema huenda mechi hiyo ikawa ndio mechi yake ya mwisho katika ardhi ya nyumbani kwa sababu baada ya World Cup hajui nini kitafuata ila atakuwa na nafasi ya kufilikilia zaidi.

Baba mzazi wa Diego someone afariki duniya

Carlos Simeone, baba mzazi wa kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone amefariki Dunia siku ya Ijumaa Machi 25.


Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Klabu hiyo Mzee Carlos Simeone (80) ambaye pia alikuwa babu wa mshambuliaji wa Atletico Madrid B Giuliano amefariki jana Ijumaa katika Jiji la Buenos Aires nchini Argentina.


Katika kumkumbuka Bendera katika uwanja wa Wanda Metropolitano itapepea nusu mlingoti.


Klabu mbalimbali na wachezaji wametuma salamu zao za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii.