Ufaransa wakataza abaya shuleni

Waziri wa Elimu wa Ufaransa, Gabriel Attal amesema Serikali itapiga marufuku Wanafunzi kuvaa abaya wanapokuwa Shuleni.


Vazi la abaya ambalo hufananishwa na baibui la mtindo wa kisasa huvaliwa na baadhi ya Wanawake wa kiislamu kama stara.


Waziri huyo amesema atafanya mazungumzo mapema wiki hii na Wakuu wa Shule za umma ili kuwasaidia kutekeleza marufuku hayo ya Wanafunzi kuvaa abaya Shuleni,
Sheriya hiyo inatarajiwa kuanza pindi tu muhula mpya wa Shule utakapoanza Jumatatu ijayo. 

Post a Comment

Plus récente Plus ancienne