Ciara kutafuta asiliya yake

Mwanamuziki Ciara Princess Wilson amefanikiwa kupata uraia wa Benin baada ya kurejea nchini humo kufuatilia chimbuko la asili ya mababu zake kwa kile anachodai kuwa aligundua kwamba sehemu kubwa ya ukoo wake inatoka Benin. 
Ciara amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cardinal Bernardin Gantin jijini Cotonou Julai 25,2025 na kupokelewa na Maofisa wa Benin na wakiwemo raia mbalimbali wa Taifa hilo ambapo alisimama kutoa maneno machache ya kujivunia kujua asili yake kwa kutumia lugha ya Beninese na kutafasiriwa kwa Kifaransa, “Je suis Béninoise” (“Mimi ni Mbenini”). 

Kitendo cha Ciara kuamua kutafuta asili ya ukoo wake kimewagusa watu wengi mitandaoni na wengine wakimpongeza kwa uamuzi huo na wengine wakisema kuwa ni ishara njema na isiishie tu kwake, bali hata kwa watu wengine wanaoishi Ughaibuni wajaribu kufuatilia chimbuko la asili yao ili waweze kufahamu mila, tamaduni, desturi za asili zao barani Afrika. 
Ciara alizaliwa Oktoba 25, 1985, huko Austin, Texas nchini Marekani na malezi yake yalikuwa ya maeneo mbalimbali katika kambi za Jeshi huko Ujerumani, New York, Utah, California, Arizona, na Nevada kabla ya familia yake kuamua kuweka makazi yao ya kudumu Atlanta, Georgia. 

Post a Comment

Plus récente Plus ancienne