Mwimbaji Ed Sheeran amefichua kwamba albamu yake itakayotolewa baada ya kifo chake, iitwayo Eject, imepangwa kwenye wosia wake. Mke wake, Cherry Seaborn, ndiye atakayechagua nyimbo zitakazojumuishwa kwenye albamu hiyo.
Akizungumza na Zane Lowe wa Apple Music, Sheeran alisema albamu hii itajumuisha nyimbo alizoandika kuanzia akiwa na umri wa miaka 18 hadi pale atakapoondoka duniani, na Cherry atachagua nyimbo 10 bora zaidi. Sheeran aliongeza kuwa hakutaka watu wasio wa karibu wachanganye kazi zake na kutoa albamu bila mpango: “Sitaki mtu aje aje achanganye kazi zangu na kutoa albamu; nataka iwe imepangwa mapema.”
Albamu ya Eject itafuata mfululizo wa albamu zake mpya yenye majina yanayohusiana na vitufe vya rekodi: Play, Pause, Fast Forward, Rewind, na Stop. Ingawa Stop inaonekana kama albamu ya mwisho kwa mtazamo wake, Sheeran alisema atabaki kuunda muziki zaidi, lakini albamu hizo zitakuwa na mpangilio maalumu, kama vile Jay-Z alivyofanya na The Black Album.
Ed Sheeran pia alilinganisha mpango huu na mfano wa Paul McCartney, akieleza kwamba baadhi ya mashabiki wake watapata albamu ya Eject kuwa ya kuvutia sana, ingawa wengine hawataipenda.
Enregistrer un commentaire