FRANE SELAK; Jamaa mwenye bahati nzuri ao mbaya

Ni mwaka 1929 nchini Yugoslavia kabla ya kugawanyika, kuna mtoto huko alizaliwa na kupewa jina la Frane Selak.

Huyu aliitwa mtoto mwenye bahati mbaya sana lakini kadiri alivyokuwa akikua, hakuonekana kuwa na bahati mbaya (Mkosi) bali alikuwa na bahati sana.
Okay! Twende kuona matukio yake.

Mwaka 1962 treni aliyokuwa amepanda ilianguka na kuangukia mtoni. Ndani kulikuwa na watu 17, wote wakafariki dunia ila yeye alinusurika.
Mwaka mmoja baadaye akapanda ndege, ndege ikazingua, mlango ukafunguka na kurushwa nje ndege ikiwa angani. Akaanguka chini, hakufa, ndege ilipata ajali na abiria wote walifariki dunia.
Kwa miaka mingine 40 alikuwa ananusurika ajali mbalimbali. Kuna basi lilitumbukia mtoni, watu walikufa lakini yeye akanusurika.
Magari mawili yakashika moto, yeye akiwa ndani ya moja, akanusurika.
Kuna gari alilokuwa anaendesha lilipata ajali kwa kuruka mpaka kwenye mti uliokuwa umeota kwenye mwamba na kuanguka chini, hakufa.

Mwaka 2003 akanunua tiketi ya bahati nasibu. Ilikuwa kawaida yake. Mwaka huo, akashinda dola milioni 1.

Akaenda kununua nyumba ufukweni wa bahari  akawaweka washikaji na familia yake, akanunua kiti cha kupungia upepo wa bahari na pia akanunua pakti kibao za sigara.
Alipohojiwa, alisema kwamba : Mimi sikuwahi kuzikimbilia bahati bali bahati zilikuwa zikinifukuzia na kunifata kwa kasi ya ajabu.

Mwanaume huyo alifariki dunia mwaka 2016 akiwa na miaka 87.

Post a Comment

Plus récente Plus ancienne