Alibaba

vendredi 16 août 2013

KIOJA; KAKA MBARONI KWA KUMUOA DADA’KE

Kaizilege Jabiri (katikati) akiwa mikononi mwa wanausalama nyumbani kwake Ubungo Kisiwani, Dar.
Na Waandishi Wetu
MWANAFUNZI wa kidato cha pili jina kapuni (16), amejikuta akiozeshwa na wazazi wake kwa mwanaume aliyetambulika kwa jina la Kaizilege Jabiri (31) ambaye ni mtoto wa mama yake mkubwa, Risasi Mchanganyiko linakupa habari.
...Dada mtu akiandaa msosi.
Tukio hilo lilitokea Juni 14, mwaka huu jijini Dar nyumbani kwao Mlandizi, Bagamoyo, Pwani ambako mwanaume huyo alifunga ndoa na binti huyo na kurejea naye nyumbani kwake, Ubungo Kisiwani, Dar huku baadhi ya watu wakihofia uhai wa ndoa hiyo.
Baada ya kuanza maisha ya ndoa kama mke na mume, Agosti 6, mwaka huu taarifa zikafika kwenye Kituo cha Polisi cha Ubungo ambapo maafande walisema hiyo haiwezekani.
...Mtuhumiwa akihojiwa.
“Polisi walipopata habari walisema hakuna ndoa hapo, wakajipanga kwenda kuvamia nyumbani kwa wanandoa hao,” kilisema chanzo.
Chanzo kiliongeza kuwa, nje ya nyumba hiyo walimkuta msichana huyo anapika huku kaka yake akiwa kajipumzisha ndani akisubiri lishe hiyo.
...Akipigwa pingu.
Kaizilege alipobanwa alikiri kuwa mwanafunzi huyo ni mkewe walifunga ndoa ya Kiislamu, Mlandizi. Kwa kuwa kisheria ni kosa kuoa mwanafunzi aliye chini ya miaka 18 alilazimika kupelekwa Kituo cha Polisi, Magomeni, Dar.
...Mke (kulia) akishangaa baada ya mumewe kutiwa nguvuni.
Kwa upande wake mwanafunzi huyo alikiri kuolewa na kaka yake. Alisema yeye ni mwanafunzi, yuko kidato cha pili Mlandizi. Alisema hakuwa na maamuzi  ya kuikataa ndoa hiyo kwani uwezo huo ni wa wazazi wake.
Denti huyo alizidi kuweka wazi kwamba, chanzo kikubwa cha kuozeshwa kwake ni kutokana na ugumu wa maisha ulioko katika familia hali iliyomsukuma baba yake mzazi kumshawishi aolewe na kaka yake.
...Akitolewa nyumbani kwake.
Alisema kuwa aliambiwa atakapoolewa, mumewe  huyo angeendelea kumsomesha jambo ambalo halikufanyika.
‘’Mimi nilikubali niolewe ili baadaye nipelekwe shule kwani wazazi wangu hawana pesa za kunisomesha na mimi siwezi kukataa kwa sababu wazazi ndiyo wameamua,’’ alisema.
...Akipelekwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea kituoni.
VYANZO VYA HABARI
Hata hivyo, kwa mujibu wa baadhi ya ndugu, dini ya wawili hao inaruhusu kumuoa mtoto wa mama’ke mkubwa endapo atakuwa amefikisha umri wa miaka 18 haki ambayo kwa mwanafunzi huyo haipo.
...Mtuhumiwa akiwa kichwa chini.
Risasi Mchanganyiko liliwasiliana na msemaji wa dawati la jinsia Wilaya ya Kinondoni, Dar, Inspekta Prisca Komba ambapo mhusika mmoja alisema:
...Mtuhumiwa na mkewe wakiingia kwenye gari.
‘’Kwa mujibu wa sheria na taratibu za utamaduni wetu si ruhusa kuoa mtoto wa mama mkubwa tena akiwa bado mwanafunzi, mimi naona ni kuvunja sheria na ni lazima huyu bwana afunguliwe jalada la uchunguzi.”
...Safari kuelekea kituoni.
Kaizilege amefunguliwa jalada la uchunguzi kwa Kumbukumbu MAG/RB/9015/2013, mara uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.  
Mlango wa kuingia kwa mtuhumiwa.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire