Alibaba

vendredi 16 août 2013

ROSE NDAUKA AANIKA MAJIBU YA UKIMWI

Na Gladness Mallya
BAADA ya kuzodolewa kuwa alikimbia majibu ya ngoma kwa tetesi hayakuwa mazuri, staa wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka ameamua kuanika majibu ya vipimo vya Ukimwi.
Rose alitundika picha ya cheti alichopima ugonjwa huo katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar kwenye mtandao wa kijamii kuonesha kuwa yupo safi na hana maambukizi ya Ukimwi.
Baada ya kutundika picha ya cheti hicho, staa huyo alisindikiza na ujumbe wa maneno kuonesha shukrani zake kwa Mungu.
“Namshukuru Mungu kwa kuwa nimepima na nipo fiti, hope waliokuwa wakinisema watabaki na vijiba vyao vya roho, watasonyaje?” aliandika. 

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire