👉KISA CHA KONDOO WA EID AL ADH-HA🐑🐑🐑🐑
👉Jamaa mmoja alielekea sokoni kununua kondoo wa iddi.
Pindi alipokuwa akirudi nyumbani,kondoo wake akakimbia.
👉Yule jamaa akamfukuzia mpaka yule kondoo akaingia katika nyumba moja
ya mama mjane mwenye watoto yatima.
👉Baada ya watoto kumuona kondoo kaingia ndani, wakafurahi
na kuanza kuimba: 🐑Kondoo wa eid ! kondoo wa eid ! kondoo wa eidi !.
👉Mama yao alikuwa chumbani,akawajibu wanae: Hakuna kondoo wa eid.
Muhusika wa kukununulieni kondoo wa eidi hivi sasa yupo mchangani.
👉{Akikusudia baba wa watoto hao aliye fariki na kuwaacha watoto na mke}.
Pindi yule mama alipo toka sebuleni,kweli akakuta kuna kondoo na watoto
bado waendelea kushangilia.
👉Ghafla yule jamaa mmiliki wa kondoo akafika katika nyumba ile,
akapiga hodi na kukaribishwa.👉Lengo lake lilikuwa ni kumchukua kondoo wake
aliye mkimbia.
👉Lakini kutokana na hali halisi aliyo ikuta kwa watoto wale,
Kwanza kabisa nyumba yao ilikuwa ikionesha ya kwamba
wahusika ni mafakiri,lakini vile vile furaha waliyo kuwa nayo
watoto wale , ilimfanya yule jamaa awaonee huruma watoto wale
na kujisikia aibu kumchukua yule kondoo !!!
Akamwambia yule mama: 👉Hii ni swadaka yangu kwenu,
Kwa ajili ya Eid al adh-haa{Eid ya kuchinja}.
👉Yule mama akafurahi sana na watoto wake
kwa kupata kitoweo cha iddi.
👉Yule jamaa ikambidi arudi nyumbani na kuchukua fedha
nyingine,ili aweze rejea kwa mara nyingine sokoni na
kununua kondoo wa iddi.
👉Baada ya kufika sokoni,akakuta kuna gari ndio ikiwa inashusha kondoo wengine.
👉Akasubiri mpaka walipo maliza kuwashusha wale kondoo.
Baada ya hapo akaanza kuchagua kondoo munasibu kwa ajili ya iddi.
👉Kuna kondoo mmoja alipendezwa nae.
Lakini alikuwa ni mkubwa na kanona kulikoni kondoo wa mara ya kwanza.
👉Kutokana na hivyo akawa na khofu,je fedha yangu niliyo nayo itatosha kumnunua
kondoo huyu???
👉Wacha nimuulize muuzaji.
Mteja:Ebwa ee kondoo huyu ni kiasi gani?
Muuzaji:Hebu chagua vizuri,ndiye uliye ridhika nae?
👉Mteja:Naam nimeridhika na huyu.
Anauzwa kiasi gani?
Muuzaji:Kondoo huyu nitakupatia bure,
Kwani baba yangu alinihuisa ya kwamba,
Pindi nitakapo fika sokoni na hawa kondoo,
Mtu wa kwanza kuchagua kondoo nisimuuzie,
bali nimpatie bure ikiwa ni swadaka kwa ajili ya Allah !!!
👉kutokana na hivyo kondoo huyu ni bure kwako,hongera ndugu yangu.
👉Jamaa akarudi nyumbani na kondoo wake akiwa na furaha ya hali ya juu.
************************************************** *********
🔷Subuhaana LLAH !!!
Hivi ndivyo yalivyo malipo
ya wema na swadaka,malipo yake huwa
si yenye kuchelewa.Tatizo ni kwamba sisi wanaadamu
Baadhi ya nyakati huwa hatuyahisi malipo hayo.
Allah anatueleza ndani ya kitabu chake kitukufu:
🔷(Na hamto toa chochote isipokuwa Yeye{Allah} atakilipa.
Naye ni Mbora wa wanao ruzuku) Qur-ani 34:39
Mtume rehema na amani zwe juu yake anatueleza yakwamba:
🔷(Hakuna siku yeyote isipokuwa kuna malaika wawili wakiomba:
Ewe Allah ! mpe mtoaji badala ya kile alicho kitoa.
🔷Ewe Allah ! mpe mwenye kujizuia kutoa{bakhili} huruma za kutoa katika mali yake).Aamin ...
🔷Haya ndugu zanguni !!!
Tukiwa tunaelekea katika iddi al hajj
Furaha ya iddi tusitosheke nayo peke yetu.
🔷Bali tuwakumbuke na ndugu zetu masikini na wasio jiweza.
🔷Swadaka hizo hazito punguza katika mali zetu,
bali itakuwa ni sababu ya kuongezeka mali zetu
🔹Mkono kwa mkono hadi peponi🔹
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire