Pasta mmoja Afrika Kusini alijitia kitanzi baada ya kutumia waumini picha yake akiwa uchi kwenye mtandao wa WhatsApp
– Pasta huyo ambaye ameoa alitaka kumjulisha mpenzi wake wa pembeni kwamba mkewe hakuwa nyumbani, lakini akaishia kuwatumia waumini wake ujumbe huo
Pasta Letsego aliye na kanisa lake Afrika Kusini alijitoa uhai baada ya kusemekana kuwa aliwatumia waumini picha ya uume wake kwenye mtandao wa Whatsapp wa kanisa hilo.
Ripoti zasema pasta Letsego ambaye ameoa alituma picha hiyo kimakosa kwa kikundi cha kanisa hilo kwenye Whatsapp, na kwamba alinuia kumtumia mpenzi wake wa pembeni.
“Mke hayupo, hii ni yako yote usiku wa leo,”pasta huyo akasema katika maelezo yaliyoandamana na picha hiyo.
Dakika chache baada ya kutuma picha hizo, waumini walianza kumshambulia vikali na akalazimika kujiondoa katika kikundi hicho cha Whatsapp.
Siku iliyofuata pasta huyo alipatikana amefariki, akining’inia kwa kamba shingoni katika nyumba yake aliyokodishiwa na kanisa.
Pasta Letsego ni mmoja wa wachungaji wa kanisa la Christ Embassy Church. Waumini wake walisema kuwa wamekuwa wakishuku kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi baina yake na mwanadada aliyenuiwa kupokea picha hizo.
“Vitendo vya pasta kwa muda mrefu vilikuwa vya kutiliwa shaka,” alisema mmoja wa waumini wa kanisa hilo.
“Mara kwa mara alionekana na mmoja wa mashemasi kwa jina Miriam na tulishuku kuwa walikuwa na uhusiano zaidi ya urafiki. Mkewe na waumini walipomwuliza alipuuza madai yoyote na kusema kuwa, kama pasta yeye ni baba kwa kila mtu na kwamba Miriam alikuwa binti yake mpendwa.”
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire