Wayne Rooney amemuomba radhi kaimu meneja wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate baada ya picha kutolewa zikimuonesha akiwa mlevi wakati wa sherehe ya harusi.
Nahodha huyo alihudhuria sherehe hiyo ya harusi katika hoteli ambayo timu hiyo ilikuwa inakaa wakicheza mechi ya kimataifa.
Nahodha huyo amesema kupitia taarifa kwamba picha hizo "hazifai".
Amesema ingawa picha hizo zilipigwa wakati wake wa kupumzika, "hazifai kwa mtu wa hadhi" yake.
Gazeti la The Sun la Uingereza lilichaisha picha hizo ambazo zinamuonesha Rooney, 31, akiwa kwenye sherehe usiku wa Jumamosi baada ya mechi ya England ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Scotland.
England walishinda mechi hiyo.
Chama cha Soka cha England (FA) kimesema kitathmini upya sheria kuhusu mambo ambayo wachezaji wanaruhusiwa kufanya wakati wao wa kupumzika.
Gazeti la The Sun linadai FA imechukua hatua hiyo kwa sababu wachezaji 10 wa England walikaa kwenye kilabu cha usiku hadi saa 04:30 GMT Jumapili.
Rooney hakucheza mechi ambayo England walitoka sare 2-2 na Uhispania Jumanne kwa sababu ya jeraha ndogo kwenye goti.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire