Alibaba

mardi 20 septembre 2016

Manchester United wiki hii

MARCUS Rashford amefunga mabao mengi kuliko mchezaji yeyote wa Man United tangu alipoanza kuichezea timu hiyo Februari 2016. Mabao 10.

Man United imeshinda mabao mengi ugenini kuliko timu yoyote kwenye Ligi Kuu England.
Imefunga idadi ya Mabao 800.

Arsene Wenger amtolea mbov Pep

ARSENAL oya oya. Baada ya kuigonga nne Hull City huko kwenye vyumba vyao vya kubadilishia ni mwendo wa kupiga selfie tu, kisha Kocha wa Arsene Wenger akachimba mkwara labda Manchester City watibue mipango.

Arsenal imeshinda mechi tatu mfululizo za ligi kwa mara ya kwanza tangu mwaka huu uanze na tamu zaidi wamefunga mabao saba katika mechi zao mbili za karibuni walizocheza ugenini.

Hata hivyo, Wenger amewaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba wasifurahie sana kupita kiasi kwa sababu kuna timu moja inawapa homa, Manchester City ya Mhispaniola Pep Guardiola.

Man City wameiacha Arsenal kwa pointi tano kileleni kwenye msimamo na Wenger anasema: “Kwa sasa wamekuwa na timu nzuri sana na wamekuwa wakishinda mfululizo.
“Lazima tucheze kiakili sana, lakini naamini tutawakamata hata mwaka jana, Man City ilishinda mechi zao tano za mwanzo.”

Arsenal waliutawala mchezo wao dhidi ya Hull City na hakukuwa na shaka kabisa kuhusu kushinda mchezo huo hasa baada ya Jake Livermore kutolewa kwa kadi nyekundu kabla ya mapumziko. Lakini, Wenger anawaambia wachezaji wake kukaza buti ili kufanya vizuri kwa mechi zao za nyumbani pia.

“Tunapocheza ugenini, tunakuwa kwenye kiwango kizuri sana,” alisema Wenger.
Wenger alimsifu pia kiungo wake Alex Iwobi na kumwambia anapaswa kucheza kwa kiwango kikubwa kama ilivyokuwa kwa mjomba wake Jay Jay Okocha alivyokuwa akitesa kwenye kikosi cha Bolton. Iwobi alikuwa staa wa mchezo huku mabao ya Arsenal yakifungwa na Alexis Sanchez (mawili), Theo Walcott na kiungo wa shoka, Granit Xhaka. Wakati mambo yakiwa matamu kwa Wenger na Arsenal yake ambayo kwa sasa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, mpinzani wake Jose Mourinho na Manchester United yake ni majanga, wakiporomoka hadi kwenye nafasi ya saba baada ya vipigo viwili mfululizo kwenye ligi hiyo. Man United imeruhusu mabao matano kwenye mechi mbili za ligi za karibuni, huku yenyewe ikiwa imefunga mawili tu na kuonyesha hali ya hatari kwa miamba hiyo ya Old Trafford.

PEP GUARDIOLA : "SI YAYA TOURÉ VEUT REJOUER, SON AGENT DEVRA S’EXCUSER"

Visiblement très en colère après les propos de l’agent de Yaya Touré, le coach de Manchester City compte bien se passer de l’Ivoirien s’il ne s’excuse pas.

Décidément, les choses ne s’arrangent pas entre Yaya Touré et Pep Guardiola. Depuis l’arrivée du Catalan, l’international ivoirien vit un véritable cauchemar.

"Yaya est déçu, mais il restera professionnel et continuera à donner le meilleur de lui-même pour City. Plusieurs offres ont été formulées et nous sommes en train de les évaluer",

confiait en mai dernier l’agent du joueur, Dimitri Seluk, prévenant que son protégé ne comptait pas faire de vieux os à Manchester City avec l’arrivée de Guardiola, son ancien coach au FC Barcelone.
Et la réponse ne s’est pas faite attendre puisque Touré a très vite été évincé du groupe pour la Ligue des champions. Ce à quoi l’agent avait de nouveau répondu par voie de presse, au début du mois de septembre :

" Si Pep Guardiola gagne la Ligue des champions, alors j’irai jusqu’en Angleterre et je dirai à la télévision que Pep Guardiola est le meilleur entraîneur du monde. Mais si City ne gagne pas la C1, alors j’espère que Pep aura les c******* de dire qu’il avait eu tort d’humilier un aussi grand joueur que Yaya."

Et visiblement, ces propos ont été la goutte qui a fait déborder le vase du côté de l’Etihad Stadium. Fatigué d’être attaqué par l’agent de son joueur, Pep Guardiola a pris ce mardi la parole en conférence de presse, ne se cachant pas sur ses intentions futures.
"C'était difficile de le laisser à l'écart de la liste, mais le jour suivant, son agent a parlé dans les médias. Touré n'a pas eu le courage de m'appeler. À partir de ce moment-là, il était sorti de l'équipe. Son agent doit s'excuser. S'il ne le fait pas, il ne jouera pas" , a prévenu Guardiola.

"Pour le moment, Yaya est à l’écart. Et il le sera jusqu’à ce que son agent ait le courage de me téléphoner ou d’aller devant les médias pour s’excuser. Quand ce sera fait, alors Yaya fera partie du groupe et il aura la même chance de jouer tous les matches que les autres. Parce que je ne peux pas accepter, en tant que coach, que tous les agents, lorsque leur joueur ne joue pas, aillent dans les médias pour parler et parler et parler",
a finalement conclu Guardiola, très remonté.

Pep Guardiola has threatened to never play Yaya Touré again!

Kiungo wa Manchester City Yaya Toure, 33, ametangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa. Toure aliichezea timu yake ya taifa kwa mara ya kwanza mwaka 2004, na alichukua unahodha mwaka 2014 kutoka kwa Didier Drogba. Mwaka Jana aliiongoza timu yake na kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu 1992. Ameichezea Ivory Coast mara 113.

Wakati huohuo meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema hatomchezesha Yaya Toure mpaka kwanza aombe radhi kufuatia matamshi yaliyotolewa na wakala wake.

Waathiriwa wa Samsung Galaxy Note 7 wabadilishiwa simu

Simu ya Samsung Galaxy Note 7 iliodaiwa kuwa na betri zinazolipuka imeanza kubadilishwa Uingereza.
Kampuni ya Samsung inataka wamiliki wa simu hizo walioathirika kuwajulisha waliowauzia,lakini wengi wa wafanyibiashara wa simu hizo wanasema tayari wanawasialiana na wateja wao moja kwa moja.

Simu hizo zilitakikana kurudishwa kufuatia ripoti duniani kwamba betri zake hulipuka zinapopata chaji .
Samsung inatoa simu za bure kwa wale walioathirika huku wafanyibiashara wa simu hizo wakipata mali mpya huku simu zaidi zikiendelea kufikishwa sokoni katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

''Tumetoa wito kwa waathiriwa wa simu hizo kuzibadilisha haraka iwezekanavyo.Simu ya galaxy Note 7 zenye betri ishara ya betri ya kijani zilikuwa salama kutumia'',Samsung imesema.

Watu 50 wauawa' maandamano ya upinzani DR Congo

Muungano mkuu wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo unasema kuwa zaidi ya watu 50 waliuawa wakati wa mandamano ya kumpinga rais Joseph Kabila siku ya Jumatatu mjini Kinshasa.

Mmoja wa walioshuhudia anasema polisi waliwafyatulia risasi waandamanaji.

Upinzani umevilaumu vikosi vya usalama kwa kutumia risasi dhidi ya maandamano yanayotaka kutangwazwe tarehe ya uchaguzi wa urais.

Upinzani umeitisha maandamano zaidi leo Jumanne.

Serikali ya DRC iliwalaumu waandamanaji waliokuwa wamejihami na kusema waliouawa ni watu 17 wakiwemo polisi watatu.

Waziri wa mambo ya ndani Evariste Boshab amesema mmoja wa maafisa hao wa polisi aliuawa kwa kuchomwa moto akiwa bado yu hai.
Kuna wasiwasi kuwa rais Joseph Kabila ana njama ya kutaka kusalia madarakani baada ya kumalizika kwa muhula wake mwishoni mwa mwaka huu.

Mwandishi wa BBC aliyeko Kinshasa Poly Muzalia anasema polisi waliwakamata zaidi ya waandamanaji 10

Shule nyingi na biashara katika mji huo mkuu zilifungwa.

Kwa mujibu wa katiba, muhula wa pili wa Rais Kabila, aliyeingia madarakani baada ya kuuawa kwa babake Laurent Kabila mwaka 2001, unafaa kumalizika tarehe 20 Desemba.

Mwaka uliopita, watu 12 waliuawa katika maandamao sawa na hayo.
Tangu kujinyakulia uhuru zaidi ya miaka 55, hakuna kiongozi aliyewahi kumkabidhi mrithi wake madaraka kwa njia ya amani.

Faili za mwanariadha wa Burundi zadukuliwa

          Mwanariadha wa Burundi ambaye alishinda medali ya fedha katika mbio za mita 800 upande wa wanawake katika michezo ya Olimpiki mjini Rio

ni Mwafrika wa kwanza ambaye faili zake za kimatibabu zilidukuliwa na wadukuzi wa mtandao wa Fancy Bears.

Fancy Bear ni jina la wahalifu wa mtandaoni ambao waliiba habari za kibinafsi za wanariadha ambazo zinamilikiwa na shirika la kukabiliana na dawa za kusisimua misuli WADA na wanaangazia utumizi wa dawa za kusisimua misuli zilizopigwa marufuku.

Dawa ambayo Francine Nyonsaba aliruhusiwa kutumia na shirikisho la riadha duniani IAAF ni Tibolone.

Dawa hiyo hutumika kuongeza homoni za kike katika wanawake ambao wana homoni za kike chache.