Google tag

jeudi 3 novembre 2016

Champions League L'Équipe de la 4e journée

Champions League L'Équipe de la 4e journée selon les points remportés au Fantasy Football

Kichapo chaibua hasira za Messi

HAKUNA mwanadamu anayekubali kushindwa kirahisi. Lionel Messi anaonekana mpole kumbe nyuma ya upole huo kuna mambo, unaambiwa jamaa ni ngumi mkononi. Imetokea juzi baada ya Barcelona kuchapwa mabao 3-1 katika dimba la Etihad jijini Manchester.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Hispania, inadaiwa kuwa Messi alitiana mkononi na mchezaji mmoja wa Manchester City wakati akielekea katika vyumba vya kubadilishia nguo mara baada ya kumalizika kwa pambano la juzi.
Ripoti zinadai kwamba mchezaji huyo wa Manchester City alimwambia kitu nyota huyo wa kimataifa wa Argentina lakini kikamkera kiasi cha kumuita mchezaji huyo wa City kuwa Mpumbavu na hapo ndipo walipotiana mkononi.

Kwa mujibu wa habari za ndani kutoka Hispania, Messi ambaye anasifika kwa upole na nidhamu alikasirika kiasi cha kwenda katika chumba cha kubadilishia nguo cha Manchester City kwa ajili ya kugombana na staa huyo wa City.

Hata hivyo, rafiki mkubwa wa Messi nyota mwenzake wa kimataifa wa Argentina, Sergio Aguero wa Man City ambaye katika pambano hilo alipika bao moja la Man City ndiye aliyegeuka kuwa msuluhishi wa ugomvi huo ambao uliwashangaza wengi.

Messi alifunga bao la kwanza katika pambano hilo lakini kikosi cha kocha, Luis Enrique kilichemsha katika pambano hilo huku kocha wa City, Pep Guardiola ambaye ni kocha wa zamani wa Barcelona akilipiza kisasi cha pambano la kwanza ambalo City ilichapwa 3-1 jijini Barcelona.

Kiungo wa kimataifa wa Ujerumani, Ilkay Gundogan ambaye alinunuliwa kwa dau la Pauni 20 milioni kutoka Borussia Dortmund katika dirisha kubwa la majira ya joto alifunga mabao mawili katika pambano hilo huku staa wa kimataifa wa Ubelgiji, Kevin De Bruyne akifunga bao moja murua la faulo.

Baada ya pambano hilo, Guardiola alionekana kukoshwa na kiwango cha timu yake ingawa alikiri kwamba alikuwa hana furaha sana kwa sababu alikuwa ameifunga timu yake ya zamani Barcelona ambayo ametwaa nayo mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

“Wakati klabu kama Manchester City inapokuwa na miaka 25 bila ya michuano ya Ulaya inakuwa historia. Historia ina maana unapocheza na timu kubwa unakuwa haujiamini kupigana uso kwa uso. Hatukucheza dhidi ya Barcelona, tulicheza dhidi ya utamaduni wetu,” alisema Guardiola ambaye pia aliwahi kuwa staa mkubwa wa
Barcelona.

“Nina furaha. Ni kawaida kwamba haya mambo yanatokea. Nina furaha kwa sababu tumepata pointi tatu. Nimejifunza kwamba wachezaji wangu wanaweza kufanya mashambulizi ya kushtukiza. Lakini kwa upande mwingine nina huzuni kidogo kwa sababu nimeifunga klabu ambayo naipenda sana,” aliongeza Guardiola.

Guardioala pia alimsifu mshambuliaji wake, Sergio Aguero ambaye alianza katika pambano la juzi baada ya kuachwa nje katika pambano la kwanza baina ya timu hizo dimba la Nou Camp wiki mbili zilizopita.

WCB WAKANUSHA TAARIFA ZA KIFO CHA SALOME NA KUSEMA ALIE KUFA SIO SALOME WAO

Habari zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii siku ya jana iliripoti tukio la Model Juliana kufariki Dunia baada ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia (kubakwa).

(Picha iliyosambaa ikitaarifu tukio hilo)Lakini hali imekuwa tofauti baada ya taarifa zilizotolewa na akaunti moja ya Instagram inayojulikana kwa jina la Young_msafi ambayo imekanusha taarifa hizo.

Akaunti kiyo imeeleza kuwa aliyekutwa na ukatili huo hadi kupelekea kifo chake sio SALOME wa Diamond Platnumz bali ni model ambaye alikuwa Dancer wa chuo kikuu cha Mkumila.

Juliana amekutwa na mauti hayo usiku wa Jumatano ya tarehe 1/11/2016 baada ya Kutekwa wakati akiwa anakwenda kukutana na Marafiki zake kisha akateswa na kubakwa na watu wasiojulikana na kisha wakamtupa kichakani na mwili wake kuonekana asubuhi ya tarehe 2/11/2016.

Kupitia akaunti ya Instagram ya Ma-Model inayojulikana kwa jina la BLACKFOX_MODELS imethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa Misa ya maombezi itafanyika siku ya Jumapili katika ofisi zao.

Sababu za Aubameyang kutoka cheza dhidi ya Sporting Lisbon

Mshambuliaji Pierre Emerick Aubameyang ambaye jana aliachwa katika kikosi cha Dortmund kilichocheza dhidi ya Sporting Lisbon kutokana na sababu za ndani ya klabu.

Alitaraji kuanza katika mchezo huo wa klabu bingwa Ulaya lakini muda mchache kabla ya mechi jina lake halikuonekana katika kikosi na nafasi yake ilichukuliwa na Adrian Ramos ambaye alifunga goli pekee katika mechi hiyo.

Aubameyang ambaye hadi saivi amefunga magoli 10 katika mechi 13 katika msimu huu.
Baada ya mchezo kocha wa BVB Thomas Tuchel aliongea na waandishi alisema kuwa mchezaji huyo amefungiwa na klabu toka jumanne mpaka Alhamis (leo), lakini hakueleza sababu za zilizopelekea kifungo hicho
Imeripotiwa kuwa Aubameyang alifungiwa juzi jumanne kwa sababu alikuwa akitumia simu yake wakati wa kikao cha timu kuelekea mechi ya jana, na pia sababu nyingine ya kufungiwa, mshambuliaji huyo jumatatu hii alienda katika sherehe ya rafiki zake huko nchini Italia bila ya kupata ruhusa kutoka klabuni.

Aubameyang amepewa onyo kali mbele ya wachezaji wenzake kwa kosa la kwenda kwenye Party huko Italia bila ya ruhusa na kuambiwa lazima awepo jukwaani katika mchezo dhidi ya Lisbon uliopigwa Iduna Park, ambapo alihudhuria na kuondoka dakika 10 kabla ya mchezo kuisha.

Mchezaji huyo atarejea uwanjani wikiendi hii katika mechi ya Bundesliga dhidi ya Hamburg, amethibitisha CEO wa BVB Joachim Watzke.

Huyu Ndio Mwanamuziki wa Bongo Flava Mwenye Mafanikio Makubwa zaidi Kuliko Wanamuziki Wote Tanzania

Anaitwa AMBWENE YESSAYA AKA AY
       ni mmoja wa wasanii ambaye ana mafanikio makubwa sana kimuziki kuliko msanii yeyote yule hapa nchini Tanzania,vile vile yeye ndiye msanii wa kwanza Tanzania kuipeperusha bendera ya Tanzania katika anga za kimataifa mpaka ulaya.

Historia yake ya muziki ilianzia miaka 1998

-Pesa yake ya kwanza kurekodi ngoma studio alipewa na mama yake Tshs 20000/=
-Ni mkulima (ana mashamba ya mpunga zaidi ya heka 100 huko ifakara Morogoro
-Ni mjasiriamali mwenye biashara nyingi ikiwemo duka la nguo
-Ni mmiliki wa vipindi vya TV vya MKASI na NGAZI KWA NGAZI vinavyorushwa EAST AFRICA TV
-Anamiliki kampuni ya UNITY ENTERTAINMENT inayojihusisha na uwakala wa kazi za sanaa, matangazo na kuunganisha wasanii,pia kuleta wasanii wa nje

CONCLUSION: HAYO NI MACHACHE KUHUSIA NA SUPER LEGEND AY MZEE WA COMERCIAL