Google tag

jeudi 10 novembre 2016

Watakaoshindania tuzo ya soka ya BBC kutangazwa

Wachezaji watano nyota Afrika ambao watapigania tuzo ya BBC inayotolewa kwa Mwanakandanda Bora Afrika wa mwaka watatangazwa Jumamosi na upigaji kura kuanza.

Majina ya wachezaji hao watakaoshindania tuzo ya mwaka 2016 watatangazwa kwenye kipindi cha moja kwa moja BBC World TV na kwenye redio ya BBC World Service kuanzia saa 18:00 GMT.

Mashabiki wa soka ya Afrika kote duniani watapata fursa ya kupiga kura kwenye tovuti ya BBC African football kuanzia saa 18:50.

Upigaji kura utafungwa saa 18:00 Mnamo Jumatatu, 28 Novemba na mshindi atatangazwa moja kwa moja kupitia runinga ya Focus on Africa TV na pia kwenye redio Jumatatu 12 Desemba saa 17:35.

Wachezaji nyota wa zamani Afrika pamoja na wataalamu wa soka watahudhuria kipindi hicho maalum siku ya Jumamosi.

Kipindi hicho ambacho mtangazaji wake atakuwa Peter Okwoche, kitashirikisha mahojiano na mshindi mmoja wa zamani wa tuzo hiyo, majadiliano na watakaoshindania tuzo mwaka 2016 na utathmini wa soka ya Afrika mwaka huu.

Na kutakuwa pia na fursa ya kutazama video za matukio ya nyuma ya pazia tkwenye kurasa za Facebook za BBC Africa na BBC Sport na pia kwenye
Instagram.

BBC Sport pia wataandika ujumbe wa moja kwa moja kwenye Twitter uzinduzi utakapokuwa unafanyika, katika akaunti za Twitter za BBC Africa na BBC Sport.

Wanaotumia mitandao ya kijamii wanaweza kufuatilia matukio kupitia kitambulisha mada #BBCAFOTY.

Mshindi wa mwaka jana alikuwa Yaya Toure.

Washindi wa zamani wa Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka:
-----------------------------------

2015: Yaya Toure (Manchester City & Ivory Coast

2014: Yacine Brahimi (Porto & Algeria)

2013: Yaya Toure (Manchester City & Ivory Coast)

2012: Chris Katongo (Henan Construction & Zambia)

2011: Andre Ayew (Marseille & Ghana)

2010: Asamoah Gyan (Sunderland & Ghana)

2009: Didier Drogba (Chelsea & Ivory Coast)

2008: Mohamed Aboutrika (Al Ahly & Egypt)

2007: Emmanuel Adebayor (Arsenal & Togo)

2006: Michael Essien (Chelsea & Ghana)

2005: Mohamed Barakat (Al Ahly & Egypt)

2004: Jay-Jay Okocha (Bolton & Nigeria)

2003: Jay-Jay Okocha (Bolton & Nigeria)

2002: El Hadji Diouf (Liverpool & Senegal)

2001: Sammy Kuffour (Bayern Munich & Ghana)

2000: Patrick Mboma (Parma & Cameroon)

Msomali achaguliwa katika bunge la Marekani

Ilhan Omar, mwenye umri wa miaka 34, ameweka historia kwa kuwa mbunge wa kwanza mwenye asili ya Kisomalia nchini Marekani.

Mwanamke huyo Muislamu mwenye asili ya Somali na Marekani ndio raia wa kwanza wa Kisomali kuchaguliwa katika wadhfa mkuu kama huo nchini Marekani.

Uchaguzi wake unajiri siku chache tu baada ya rais mteule Donald Trump kushtumu wahamiaji wa Kisomali mjini Minnesota kwa kueneza maoni ya itikadi kali.

Akisherehekea ushindi wake bi Omar amesema kuwa atakuwa sauti ya waliotengwa katika bunge la jimbo hilo.

''Nadhani nimeleta sauti ya akina mama vijana wanaotafuta fursa''.
Redio ya uma katika jimbo hilo ilimnukuu akisema kuwa alitoroka nchini Somalia na familia yake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe wakati alipokuwa na umri wa miaka minane pekee.

Waliishi nchini Kenya kama wakimbizi kwa takriban miaka minne kabla ya kuelekea Marekani na kuishi katika jimbo lenye Wasomalia wengi la Minnesota.

Picha: Tattoo mpya ya Lionel Messi

Mchezaji wa klabu ya Barcelona na Argentina Lionel Messi, ameonyesha tattoo yake mpya mguuni wakati akiwa anafanya mazoezi na timu yake ya taifa.

Messi ambaye ni mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or mara tano ameamua kuonyesha mguu wake wa kushoto ulivyokuwa umefunikwa na rangi nyeusi ya tattoo ambayo ina namba ya jezi yake namba 10.

Mashabiki msitengeneze bifu isiyo ya lazima kati ya Wizkid na Alikiba

Ushabiki ni mzuri kufurahia, ni mzuri kupongezana, lakini pale unapoingiza matusi, hakika matokeo yake ni mabaya siku zote.
Ama pengine ushabiki kimuziki tulionao Tanzania, ubaki kuwa wa kurushiana matusi tu ndani kwa ndani na usihusishe wasanii wa nje ambao timu zetu hazihusiani nao asilani.

Ninasikitishwa sana na ninachokiona kwenye ukurasa wa Instagram wa Wizkid baada ya kubainika kuwa tuzo ya MTV EMA aliyokuwa ameshinda awali itachukuliwa na atapewa Alikiba – ambaye kwa mujibu wa kura ndiye aliyestahili kushinda. Hiyo imekuwa habari njema kwa mashabiki wa Alikiba. Wanastahili kufurahia – actually, Watanzania wote bila kujali timu zilizopo tunapaswa kufurahia na kumpongeza Kiba kwa hatimaye kututoa kimasomaso.
Lakini kwanini Wizkid ambaye naye alipewa tu tuzo hiyo (si kama aliwawekea MTV EMA mtutu wa bunduki ili wampe) atukanwe? Kwanini mashabiki wanataka kutengeneza uadui si tu kati ya Wizkid na Alikiba, bali ni Nigeria na Tanzania?

Unadhani mashabiki wa Wizkid au Wanaijeria kwa ujumla wanapenda kuona msanii wao anatukanwa bila sababu? Kwanini hatuwezi tu kufurahia ushindi huu bila kumtusi, kumkejeli Wizkid ambaye kwa miaka yote amekuwa akiipenda sana nchi yetu? Isitoshe Alikiba amempongeza Wizkid kwa ushindi wake.

Sasa kwanini mashabiki wanashindwa kutambua kuwa msanii wanayempenda anahitaji kushirikiana na wasanii hawa na sio kutengenezewa tension baina yao isiyokuwa na faida! Nigeria ni sehemu muhimu Afrika kimuziki, si jambo la heri kwa msanii wa Tanzania kukimwagia mchanga kitumbua anachoweza kuhitaji kutoka huko siku za usoni.

Anachofanyiwa Wiz kwenye ukurasa wake ni aibu inayoirudia Tanzania. Watu wachache wanaharibu jina la nchi kwa kuendekeza ushabiki usiokuwa na afya. Na pengine ndio maana Wiz ametweet:
Too many dumb people in the world. God help us!

Ombi kwa baadhi ya mashabiki wa Alikiba ama tu wengine ambao wameamua kutumia nafasi hiyo kumharibia siku Wizkid: Tunajidhalilisha kwa tunachokifanya. Hakuna faida ya maneno tunayomwandikia msanii huyu kipenzi cha wengi Afrika na duniani kwa ujumla. Tufurahi kuwa tuzo inakuja Tanzania na tumpongeze Ali kwa ushindi huo, basi!

Caf yaongeza fedha za washindi katika mashindano yake

Shirikisho la soka barani Afrika Caf limeongeza kitita cha fedha zinazozawadiwa washindi katika michuano yote kuanzia mwaka 2017 kueleka 2020.

Washindi wa kombe la mataifa ya bara Afrika watapata dola milioni 4,wakati ambapo Ivory Coast ilizawadiwa dola milioni 1.5 iliposhinda taji hilo mwaka 2015.
Mshindi wa kombe la vilabu bingwa Afrika atajishindia dola milioni 2.5 badala ya dola milioni 1.5 ambazo Mamelodi Sundowns walijishindia mwezi uliopita.

Wakati huohuo fedha za mshindi wa kombe la mataifa ya bara Afrika upande wa wanawake zitaongezwa na kufikia 80,000 mwaka 2019 kutoka dola 50,000 mwaka huu.
Fedha hizo ni chache mno ikilinganishwa na zile inazopewa timu iliomaliza ya mwisho katika kombe la bara Afrika upande wa wanaume.

Uchaguzi Marekani 2016: Michelle Obama mwaka 2020?

Nani ameanza kufikiria kuhucu uchaguzi mkuu ujao nchini Marekani? Kunaye?
Naam, ingawa si wengi, kunao walioanza kufikiria kuhusu uchaguzi mkuu ujao nchini Marekani, sana wengi waliokuwa wanamuunga mkono Bi Hillary Clinton wa chama cha Democratic aliyeshindwa na Donald Trump wa Republican.
Uchaguzi mkuu hufanyika kila baada ya miaka minne, maana kwamba wanafikiria kuhusu Novemba 2020.

Aliyeanza kuzungumziwa sana ni mke wa Rais Obama, Michelle Obama, ambaye kando na kuwa mwanamke kama Bi Clinton, ameonyesha kuwa na sifa nzuri.

Ni mmoja wa waliotia juhudi sana siku za mwisho za kampeni upande wa Bi Clinton na alimshambulia sana Bw Trump.
Marekani kwa sasa ni taifa lililogawanyika kisiasa, lakini umaarufu wake unaonekana kuvuka mipaka.

Mamia tayari walijitokeza kwenye mitandao ya kijamii baada ya ushindi wa Trump kumhumiza Michelle awanie 2020.
"Mazingira mwafaka sana kwa Michelle Obama kushinda uchaguzi 2020," mmoja aliandika.
Mwingine alisema: "Michelle Obama 2020 tafadhali Michelle Obama 2020 tafadhali Michelle Obama 2020 tafadhali".

Kwa mujibu wa utafiti wa Gallup, Bi Obama anapendwa asilimia 64 na Wamarekani, kiwango kilicho juu ya Donald Trump, Hillary Clinton na hata mumewe.

Kuna tatizo moja hata hivyo, kwani Bi Obama mapema mwezi Machi alisema hana nia ya kuwania urais.
Lakini hata hivyo mambo mengi yamebadilika tangu wakati huo.

Bi Clinton, wakati wa hotuba yake baada ya kushindwa, alisema ingawa mwenyewe hakufanikiwa, anaamini siku sijazo kutakuwepo mwanamke atakayefanikiwa.

Donald Trump Story

Huyo ndio Trump.... Siyo mtu ana Vogue Tatu anajiita Bilionea... Haa haa haa...

DONALD TRUMP JOHN alizaliwa 14 Juni 1946 huko Jamaica Estates, Queens akiwa ni mtoto wa pili kwenye familia ya watoto wanne wa familia ya Mary na Fred Trump na kukulia katika Jiji la New York, Marekani.

Upande wa baba yake (Fred Trump aliyefariki mwaka 1981), alikuwa mzaliwa wa Ujerumani na mama yake (Mary) ni mzaliwa wa Scottish.
Trump alianza kusoma katika Chuo Kikuu cha Fordham kilichopo Bronx mwaka 1964, miaka miwili baadaye alihamishiwa katika Shule ya mambo ya fedha na Uchumi ya Wharton iliyopo Chuo Kikuu cha Pennsylvania ambako alihitimu shahada ya kwanza katika masuala ya uchumi mwaka 1968 kabla ya kujiunga na kufanya kazi kwenye kampuni ya familia yake iliyoitwa Elizabeth Trump & Son.

Mwaka 1971 Trump alikabidhiwa kuongoza makampuni na biashara za baba yake ambapo alipata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi ambayo mpaka sasa ndiye mkurugenzi wake mkuu.

Trump ambaye ni baba wa watoto watano, ni mfanyabiashara mkubwa na bilionea nchini Marekani, pia ni mtayarishaji wa vipindi vya televisheni.

Baadhi ya mali anazomiliki
---------------------

Trump Ocean Club International Hotel and Tower lililopo Panama City, Panama
Trump Tower lililopo Manhattan
Wollman Rink lililoko Central Park
Trump Taj Mahal lililoko Atlantic City, New Jersey
Turnberry Hotel, iliyoko Ayrshire, Scotland
Trump Hotel Las Vegas
Trump International Hotel & Tower ya New York
Trump International Hotel & Tower ya Chicago
Trump International Hotel ya Las Vegas
Trump International Hotel ya Waikiki Beach Walk
Trump SoHo ya New York
Trump International Hotel & Tower ya Toronto
Taasisi ya Donald J. Trump
Branding na licensing
Ndege kubwa ya Trump’s Boeing 757, maarufu kama “Trump Force One”.

Utajiri Mwaka huu (2016), Jarida maarufu la Forbes lilikadiria utajiri wa mali za Trump kuwa unafikia dola bilioni 3.7. Ameweka rekodi ya kuwa mwanasiasa mwenye utajiri mkubwa zaidi kwenye historia ya nchi hiyo.

Ikijumulishwa na thamani ya kampuni yake (brand), Trump anakadiliwa kuwa na utajiri sasa wa dola bilioni 10 na kuwa tajiri namba 324 wa dunia na wa 156 kwa nchi ya Marekani.

Trump ni Mwenyekiti na Rais wa Shirika Kibiashara la Trump (Trump Organization) lenye makao yake makuu katikati ya Mji wa Manhattan ambalo linamiliki majengo mengi marefu, hoteli, kasino, timu za gofu, ndege na miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo nchini Marekani na nje ya Marekani.

Ni mwanasiasa wa Chama cha Republican na anagombea urais wa Marekani kupitia chama hicho mwaka huu,
Na kwa sasa ndie aliechagulia kuwa Raisi wa 45 wa umarekani