Alibaba

jeudi 24 novembre 2016

Borussia Dortmund na Legia Warsaw wavunja rekodi

Klabu za Borussia Dortmund na Legia Warsaw zilivunja rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumanne, kwa kufungana jumla ya mabao 12.

Wajerumani hao chini ya Thomas Tuchel walishinda wapinzani wao kutoka Poland 8-4 mechi ya kusisimua iliyochezewa Ujerumani.
Walivunja rekodi iliyowekwa mabao 11 yalipofungwa mechi ambao Monaco waliwalaza Deportivo La Coruna 8-3 mwaka 2003.

Mabao saba yalifungwa dakika 22 za kipindi cha kwanza.
Legia ndiyo klabu ya kwanza kufunga mabao manne mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na bado kushindwa kwenye mechi.

Rekodi zilizovunjwa
---------------------

* Ni mara ya kwanza historia ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wachezaji wanane kufunga mechi moja

* Dortmund ni klabu ya nne baada ya Liverpool, Monaco na Real Madrid kufunga mabao manane mechi moja Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

* Ilikuwa mechi ya kwanza michuano ya ngazi ya juu Ulaya kufungwa magoli 12 tangu Ajax walipolaza Red Boys Differdange wa Luxemburg 14-0 michuano ya zamani ya Kombe la Uefa 3 Oktoba 1984.

* Ni mechi moja pekee historia ya Kombe la Ulaya na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambapo mabao zaidi yalifungwa, Feyenoord ya Uholanzi ilipolaza KR ya Iceland 12-2 mnamo Septemba 1969.

* Dortmund sasa wamefunga mabao 14 dhidi ya Legia msimu huu, mabao mengi zaidi kufungwa dhidi ya mpinzani mmoja msimu mmoja wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

* Shinji Kagawa - ambaye wakati mmoja alichezea Manchester United - alifunga mabao mawili katika sekunde 76, mabao mawili ya kasi zaidi historia ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

* Reus arejea kwa kishindo
Marco Reus wa Dortmund alirejea kwa kishindo baada ya kukaa nje kwa miezi sita kutokana na jeraha. Alikuwa na nahodha wa timu na alifunga mabao matatu.

"Nilifurahia kuwa hapo tangu mwanzo," alisema Reus ambaye alikosa Kombe la Dunia 2014 na Euro 2016 kutokana na jeraha.

Mambo yalivyokuwa
------------------

Moja - Legia wajiweka kifua mbele

Mbili - lakini hawaongozi muda mrefu

Tatu - Wajerumani wanaongoza

Nne - nakuongeza jingine

Tano - lakini Legia wanakomboa

Sita - sasa ni 4-2, wataendelea?

Saba - Reus anafanya mambo

Nane - na kisha anafunga jingine

Tisa - watajikwamua?

Kumi - tumefikisha mabao kumi!

11 - umekuwa usiku mrefu?

12- mambo yanamalizika 8-4

MAENEO FLANI ya KISHUA"


-Mshikaji alimuona demu mkali
anakatiza kitaa akamkubali akaamua amfuate amtemee cheche
MSHIKAJI- mambo dada?
DEMU- powa
MSHIKAJI-
umependezaa!!!
DEMU- asante.
MSHIKAJI- unaweza ukanisaidia namba yako ya simu.......
maana duh nmekukubali kinyama.
Demu baada ya kuambiwa vile akazama kwenye pochi lake akatoa noti ya 10000 akaandika namba yake kwenye noti akampa mshikaji.

Mshikaji kapokea ile noti akachana sehem iliyoandikwa namba halafu kamrudishia Demu noti yake..!!!

JE NANI ANA DHARAU

NA NANI JEURI..

DEMU AU MSHIKAJI??
🤒🤒🤒🤒🤒🤒🤒🤒