Chelsea wako kifua mbele katika ligi na alama 9 na wanaweza kujiimarisha kileleni wakati wakiipokea Arsenal ilio nafasi ya tatu.
Mechi hii kwa Chelsea ni fursa kujivua aibu baada ya kulambishwa sakafu na arsenal bao tatu kwa bila katika mechi ya awali.
Na baada ya hapo ndio ulikuwa mwanzo mzuri wa Chelsea kufululiza na matokeo mazuri .
Arsenal ambao jumanne walipokea kichapao cha Watford , wana wasiwasi mkubwa hasa baada ya kiungo wake Aron Ramsey kuumia mguu.
Pia watakosa huduma za Granit Xaka anayetumikia adhabu huku Mohamed Elneny akiwa michezo ya fainali za kombe la Afrika na timu yake ya Misr.
Ushindani pia ni kati ya washambuliaji wawili Diego Costa wa Chelsea na Alexis Sanchez ambao wanaongoza kama wafungaji bora na mabao 15.
Katika mechi nyingine hapo kesho Tottenham ilio nafasi ya pili wanaipokea Middlesbourg.
Nayo Liverpool itasaka ushindi wake wa kwanza mwaka huu wakiwa ni wageni wa Hull City .
Jumapili, Manchester City wanachuana na Swansea City huku Leicester City wakiikaribisha Man U