Google tag

dimanche 29 décembre 2019

Fred na Manchester United

FREDINHO.đŸ”„⚽️

Huyu Mwamba hatajwi sana ndani ya Manchester United lakini kwa mtazamo wangu mimi binafsi ndio amekuwa mchezaji bora wa Manchester United katika kipindi cha takribani miezi miwili 



United ashinde au afungwe mara zote huwa anaonesha kiwango cha juu sana, energy level ya juu, passing , defending, interceptions ( anakata sana pasi zinazopita njiani kwenda kwao ) lakini pia anaanzisha mashambulizi haraka sana 

Anahitaji wachezaji wenzake wawe na ‘ consistency ‘ nzuri ili kazi yake izidi kutoa matunda na jana dhidi ya Burnley alikuwa Bingwa tena katikati ya kiwanja akisaidiana na Matic ambaye alionesha uzoefu wake.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire