Taarifa zaidi .....
Straika wa kimataifa wa Norway Erling Braut Haaland ametua ndani ya klabu ya Borussia Dortmund kutoka RB Salzburg kwa dau linaloripotiwa kufika kiasi cha Pauni Milioni 18 na mkataba mpaka mwaka 2024.
Haaland alikuwa akiwindwa na Juventus, Manchester United na RB Leipzig lakini ni Dortmund ndio wamefanikiwa kumnasa na atajiunga na wenzake Januari 3.
Haaland mwenye umri wa miaka 19 msimu huu ameweka kambani magoli 28 katika mechi 22 pamoja na yale 8 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire