Kama utakuwa na kumbukumbu miaka ya nyuma msanii alikuwa akitaka kuachia project ya wimbo au albamu basi ataandaa T-shirt pamoja na kofia kwaajili ya promotion ingawa trend hiyo ilipotea.
Njia hiyo iliwasaidia sana wasanii wengi kwenye promotion ya kazi zao, ambapo mpaka zikazaliwa brand kama African Boy ya Jux, PKP ya Ommy Dimpoz ambazo kwa sasa ni brand chache sana ambazo bado zinaendelea kufanya vizuri.
Diamond kupitia #FOA tayari amekuwa gumzo mtandaoni na huwenda hii ni ishara kwamba amefanikiwa kutengeneza shauku kwa mashabiki wake pamoja na mashabiki wa muziki.
Mashabiki wengi wa muziki tayari wamekaa mkao wa kula kwaajili ya ujio wa project hiyo ambayo bila shaka itakwenda kukata kiu yao.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire