Google tag

mercredi 27 juillet 2022

Je kwenye Movie watu hufanya mapenzi kweli ?

Watu wengi huwa wanajiuliza kwamba zile scene ambazo katika Filamu za nje tunaona watu wakifanya mapenzi, je huwa wanafanya kweli au sio kweli.


Jibu ni kwamba mbali na PORNOGRAPHY Hakuna Filamu ambayo waigizaji wanafanya mapenzi kweli. Ninaposema kufanya mapenzi ninamaanisha Kugusanisha Sehemu za Siri, achana na mabusu na kushikanashikana.


Kinachofanyika kwenye hizo filamu ni kwamba scene ambayo inahitaji watu wafanye mapenzi kweli, au Scene inayohitaji kuonesha Sehemu za Siri za muigizaji kwa mfano Matiti, n.k basi watatafutwa Professional Porn Actors, kwa lugha ya filamu wanatambulika kama (Body Doubles) watatafutwa kisha watafanya yao kisha Kwa Techonology ya CGI (Computer Generated Images) zitapachikwa sura halisi za waigizaji.


Hivyo hivyo unaweza ukajiuliza mbona filamu fulani Star ameonekana Maziwa wazi, mfano Angelina Jolie kuna filamu yake moja yupo kifua wazi sana, huyo sio yeye ni ujanja tu wa Computer na matumizi ya Body Doubles.

lundi 18 juillet 2022

Mjomba wa Davido kuchaguliwa kuwa Gavana

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria mkali wa Afrobeats David Adedeji Adeleke alimaarufu kama Davido ameeleza furaha yake baada ya mjomba wake, Seneta Ademola Adeleke, kuchaguliwa kama gavana ajaye wa jimbo la Ogun katika awamu ya pili ya kuwania kiti hicho.
0
Seneta Adeleke alishinda kiti hicho kwa tiketi ya chala cha upinzani cha Peoples Democratic Party (PDP).

Davido alikuwa mtu maarufu katika kampeni zake zote mbilimwaka 2018 na 2022 za kuwania kiti hicho.


"Familia ni kila kitu kwangu. Kando na hilo, sisi ni watu bora kwa kazi – tupatie mwaka mmoja au miwili na utaona nini kinatakachofanyika," nyota wa muziki aliiambia BBC Idhaa ya Pidginb kutoka mji wa kwa owa Ede kusini mwa Nigeria.

Rais Muhammadu Buhari alimpongeza Senator Adelekekwa ushindi wake, akisema kuwa "watu wa Osun wameelezea utashi wao kwa njia ya kura ".

dimanche 17 juillet 2022

Riyad Mahrez na sim yake iliyo haribika

Winga huyo wa klabu ya Manchester City ambaye kwa sasa analipwa kwa euro mil 120,000 sawa na Tsh 281,954,557/= kwa wiki Riyad Mahrez ametania kuwa hangeweza kumudu kutengeneza simu yake iliyoharibika hadi asaini mkataba mpya Manchester City.


Winga huyo wa Algeria ameongeza muda wa kukaa Etihad hadi 2025, baada ya kuingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa awali mwanzoni mwa mwezi huu.

Baada ya kukubali kufanyiwa marekebisho ya mkataba alikibali kusaini na alikuwa sehemu ya kikosi cha City kilichoondoka Jumamosi asubuhi kuelekea Marekani kwa ziara ya maandalizi ya msimu mpya.


wakati waondoka kuelkea Marekani Mahrez Alipost picha kwenye Twitter akiingia kwenye ndege, lakini wafuasi waligundua haraka kuwa alikuwa ameshika simu iliyopasuka.


'Mahrez una pesa,' shabiki mmoja alijibu, huku wengine wengi wakishangaa kwamba mchezaji wa Ligi ya Premia anaonekana kushindwa kurekebisha simu yake.

Lakini kijana huyo mwenye umri wa miaka 31 alitoa jibu la kufurahisha. "Nilikuwa nikisubiri mkataba mpya," alitania.

Mahrez alijiunga na City kutoka Leicester kwa pauni milioni 60 mwaka 2018 na amefunga mabao 63 katika mechi 189 alizochezea klabu hiyo.


Ameshinda Ligi ya Premia mara tatu chini ya uongozi wa Pep Guardiola - akiongeza taji moja alilonyanyua akiwa na Foxes msimu wa 2015-16 - na pia ameshinda Vikombe vitatu vya Carabao na Kombe moja la FA.

samedi 9 juillet 2022

Aliye mpiga risasi Shinzo Abe

Huyu hapa ndiye mwanaume wa miaka (41) raia wa Japan aliyempiga risasi na kumuua leo Waziri mkuu mstaafu aliyependwa sana nchini Japan 🇯🇵, Shinzo Abe.


Shinzo Abe aliingia madarakani nchini Japan 🇯🇵 mwaka 2006, akastaafu 2020, leo alikuwa akihutubia wananchi kwenye kampeni za uchaguzi.... Ghafla akatokea mwanaume huyu akampiga risasi mbili mgongoni na kufanya aanguke chini.

Kwa mujibu wa polisi, inatajwa silaha iliyotumika ilitengenezwa nyumbani.

Japan kuna sheria kali sana kuhusu umiliki wa silaha, ni moja ya nchi tajiri Duniani ambazo zinamatukio machache zaidi ya mauaji ya kutumia Silaha.

Shinzo Abe anakumbukwa kwa kufanya Mapinduzi ya kiuchumi nchini Japan.

Taarifa za awali zinadai mwanaume huyo alikuwa mwanajeshi mstaafu. Alikamatwa mara tu baada ya kutekeleza shambulio hilo kama unavyoona hapo kwenye picha.