Alibaba

mardi 1 mars 2022

RAIS WA UKRAINE AKATALIWA KUJIUNGA NA UMOJA WA ULAYA


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, mchana wa leo Jumanne Machi 01, amezungunza kwa hisia kali na Bunge la Ulaya akiliomba likubali ombi la nchi yake kujiunga na Umoja wa Ulaya (European Union) na kushangiliwa kwa nguvu na wabunge hao.


Rais huyo, ambaye katika siku za hivi karibuni ameonekana kama kiongozi mwenye msimamo na ishara ya ujasiri, amezungumza na wabunge hao mjini Brussels Ubelgiji kwa njia ya video akizungumzia kutoka nchini mwake katika mji wa Kyiv.

“Tutashinda, nina uhakika. Ningependa kuwasikia na nyie mkisema kuwa chaguo la Ukraine la kuwa sehemu ya Ulaya, ni chaguo lenu pia. Tunahitaji kuwa wanachama wa Ulaya. Bila ya nyinyi, Ukraine itakuwa mpweke,” aliliambia bunge na kugusa hisia za wabunge wengi ambao walisimama na kumpigia makofi kabala na bada ya kuhutubia.


Katika hatua nyingine, Mkuu wa mambo ya sera za nje wa Umoja wa Ulaya, amekaririwa akisema kuwa ombi la Ukraine la kujiunga na umoja huo linaweza kuchukuwa miaka mingi, hivyo ombi lao la kutaka kukubaliwa kujiunga mara moja haliwezekani, hii ni kwa mujibu wa chaneli ya WION English News

Franck Ribéry afanya ajali

Mchezaji wa zamani wa klabu Bayern Munich, Frank Ribery amepata ajali baada ya gari alilokuwa akisafiria kugonga taa za barabarani.


Ribery (38) aliyekuwa miongoni mwa abiria katika gari hilo ameumia vibaya kichwani na kuwahishwa hospitali.

BOSI WA GSM, GHALIB AFIWA NA BABA YAKE MZAZI


Mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) amefiwa na Baba yake, Mzee Said Mohamed ambaye amefariki dunia alfajiri ya leo March 1 2022 na atazikwa leo saa kumi jioni kwenye makaburi ya kisutu Dar es salaam.


Marehemu Mzee Said ni Mfanyabiashara wa muda mrefu Tanzania ambapo alianzisha biashara ya kwanza mwaka 1955 kwa kuuza bidhaa ndogondogo Tanga lakini baadae alihamia kuuza nguo na kuhama kutoka Tanga hadi Songea ambako alijitanua katika kilimo cha korosho ambacho Familia yake imekiendeleza hadi leo.


Inna lillahi wa inna ilayhi rajuun