Google tag

lundi 6 janvier 2014

FAHAMU KISUKARI KATIKA MAFUNGU MATATU

Wengi wanapenda kujua ugonjwa wa kisukari unavyoanza kwa binadamu. Ugonjwa huu au kitaalamu huitwa Diabetes mellitus hutokea pale tezi kongosho au Pancrease inaposhindwa kutengeneza homoni au kichocheo aina ya Insulin, au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka kiwango cha sukari kwenye damu au kitaalamu huitwa Hyperglycemia.
Insulin ni kichocheo au homoni inayotengenezwa na kongosho ili kudhibiti sukari katika damu. Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa kuwa na kiwango kidogo cha Insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili.
Ili kuelewa vyema ugonjwa wa kisukari ni muhimu kwanza kueleza namna chakula kinavyovunjwavunjwa na kutumiwa na mwili ili kuzalisha nguvu mwilini. Wakati chakula kinapoyeyushwa matukio kadhaa hutokea. Moja ni sukari inayoitwa Glucose ambayo ni chanzo cha nguvu mwilini huingia katika damu.
Tukio la pili ni kiungo kinachoitwa kongosho au kwa kitabibu Pancrease hutengeneza kichocheo cha Insulin ambayo kazi yake ni kuondoa Glucose katika damu na kuingiza katika misuli na seli za mafuta na ini, ambako hutumiwa kama nishati mwilini.
Watu wenye ugonjwa wa kisukari huwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kwa sababu miili yao haiwezi kupeleka sukari kwenye seli za mafuta, ini na misuli ili ihifadhiwe kwa ajili ya kuzalisha nguvu.
Hii ni kutokana na moja kongosho zao kushindwa kutengeneza Insulin ya kutosha  au seli za mwili wao haziathiriwi na Insulin kama inavyotakiwa au sababu zote hizo mbili.
MAFUNGU MATATU YA KISUKARI
Ugonjwa wa kisukari umegawanyika katika mafungu matatu, la kwanza ni kisukari aina ya kwanza  kitaalamu Type 1 Diabetes Mellitu ambayo wanaoathirika zaidi ni watoto na vijana.
 Ugonjwa huu hujitokeza iwapo seli maalumu zinazotengeneza homoni ya Insulin zinapokosekana katika tezi kongosho au zinapoharibika kutokana na sababu yoyote ile,  hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu mwilini.
Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa seli hizi katika tezi kongosho ni pamoja na kushambuliwa tezi kongosho kunakoweza kufanywa na magonjwa ya kinga ya mwili ya mtu mwenyewe au Autoimmune diseases, au kushambuliwa na vyanzo visivyojulikana.
Kwa vile, uharibifu katika tezi kongosho husababisha kutokuwepo kabisa Insulin mwilini au Insulin kuzalishwa kwa kiwango kidogo sana, wagonjwa wa aina hii ya kisukari huhitaji kupewa dawa za Insulin kwa njia ya sindano au pampu kila siku za maisha yao ili waweze kuishi.
Kwa sababu hiyo aina hii ya kisukari huitwa pia kisukari kinachotegemea Insulin au Insulin Dependent Diabetes Mellitus (IDDM).
Aina ya pili ya kisukari  kitaalamu huitwa  Type 2 Diabetes Mellitus ni fungu la pili la maradhi haya na  huwapata watu  ukubwani na husababishwa na kupungua utendaji kazi wa homoni ya Insulin.

Itaendelea wiki ijayo.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire