Google tag
samedi 28 novembre 2015
Magufuli kanikata stimu, dah!
Dah nimechanganyikiwa kabisaaa. Akili
haifanyi kazi, yaani dah hata sijui nianzie wapi. Picha imekuwa
chengachenga kabisa. Unajua kiukweli, nilikuwa nimepanga kuwa nianze
wiki hii mipango ya harusi yangu, nilikuwa nataka harusi iwe mwezi wa
sita mwaka kesho, nilishatayarisha bonge ya plani, nilikuwa nimeipanga
kisayansi kabisa. Sasa mambo yanaharibika mbele yangu na sina la
kufanya, nimechanganyikiwa.
Kuna mtoto mmoja wa kike mtaani kwetu,
wengi mnamfahamu maana anaonekana kwenye runinga karibu kila wiki na
kwenye magazeti ndiyo hakosi, mtoto anawaka, guu guu, sauti kama
kinanda, shepu ya katalogi. Sasa huyo ndiye niliyepanga kumuoa,
nilipanga harusi iwe ya kiwango cha kimataifa, yaani jambo hili
lingetikisa vyombo vya habari kwa muda mrefu.
Hata baada ya harusi vyombo vya habari
vingetufuatilia sana, mtoto wetu naye angekuwa maarufu, tungemtumia
kwenye matangazo na kukusanya mkwanja wa kueleweka, picha nilikuwa
nimeipanga kwa kuangalia mipango ya muda mfupi na muda mrefu. Yaani kila
kitu nilikwishakipanga vizuri sana sasa dahh picha inaungua taratibu.
Yaani ilipotangazwa tu kuwa mjomba wangu
kashinda Ubunge, nikajua sasa maisha yangu yanabadilika, nilianza
kuimba ule wimbo wa Vijana Jazz Band unaitwa Umaskini Bye Bye. Mimi na
mjomba tuko karibu sana tangu nikiwa mdogo, mjomba wangu alikuwa
akinipenda sana.
Niliona wazi kabisa kuwa mjomba wangu
atachaguliwa kuwa waziri, tena ikawezekana hata kuwa waziri mkuu. Sasa
kasheshe lilianza baada ya kuona kwanza mjomba amekwisha ukosa uwaziri
mkuu, na sasa nimemsikia rais kafuta safari za nje za mawaziri kabla
hata hajawataja, yaani ndoto ndiyo imeharibika kabisaaa.
Unajua huyu mtoto kwa kweli sijaongea
naye, nilikuwa nangoja mjomba akichaguliwa kuwa waziri ndiyo nimuibukie
na kumhakikishia kuwa maisha ya kifahari akikubali tu kuolewa na mimi.
Harusi yetu yetu ingekuwa Uswisi, hanimuni Australia, na kote huko
mjomba angekuwa mgeni rasmi, sasa mkuu wa nchi katangaza hakuna safari
za nje, tena kaanza hata kupunguza gharama za sherehe, ni wazi ndoto
yangu haitatimia hata mjomba akipata zari la kuwa waziri. Ndiyo mjue
sioi tena hivyo, dahh, kweli Hapa Kazi Tu!
Picha 16, hali ya hewa yabadilika ghafla Uingereza
mercredi 3 juin 2015
Iyanya ni nani kwa kifupi
Iyanya Onoyom Mbuk alizaliwa tarehe 31
October 1986 . Iyanya ni mwanamuziki
kutoka Naijeria aliyetoka kwa kushinda
Project Fame West Africa mwaka 2008, na
akajulikana zaidi kutokana na wimbo wake
Kukere. Iyanya ni mmoja wa wakurugenzi wa
lebo ya Made Men Music Group, lebo
ambayoimewatoa wanamuziki kama Emma
Nyra, Tekno, Selebobo and Baci. Iyanya
huimba nyimbo zake katika lugha mbili
Kiingereza na Ki Efik.
Mama yake alikuwa Mkuu wa shule, baba
yake alikuwa Afisa Misitu, wote walifariki
2008. Huyo ndie Iyanya
samedi 30 mai 2015
Kundi la UHURU la Sauzi Afrika Lamuomba Diamond Platnumz Kufanya Remix ya Wimbo wa Nana Uliotoka Jana na Kuwa Gumzo Afrika.
Diamond ni Star Africa kuliko watanzania
tunavyomchukulia wakati Kundi la Uhuru
Kutoka Sauzi Afrika wakiomba kufanya
Remix ya Wimbo wake Mpya wa Nanaa,
Usiku wa kuamkia leo nchini Nigeria video ya
nana ilikuwa gumzo kwenye mitandao.
Wabongo sijui kwanin hatupendi vya kwetu
siku Diamond Platnumz mungu amemchukua
hawa wanao mbeza na kumtukana ndo
wanafiki wa kwanza kujifanya kulia hadi
kuzimia huku wakimsifia......
vendredi 29 mai 2015
Coran complète
Listen to complete Qur'an without internet access, only one click.
عبدالرحمن السديس
ـ http://rb2.in/6K1
سعود الشريم
ـ http://rb2.in/6K2
عبدالباسط عبدالصمد
ـ http://rb2.in/5Mh
محمد المنشاوي
ـ http://rb2.in/7zB
ماهر المعيقلي
ـ http://rb2.in/7zC
ادريس ابكر
ـ http://rb2.in/5Tg
عبدالله الجهني
ـ http://rb2.in/7zD
محمد المحيسني
ـ http://rb2.in/7zE
ياسر الدوسري
ـ http://rb2.in/7zF
ناصر القطامي
ـ http://rb2.in/7zG
محمد ايوب
ـ http://rb2.in/7zI
عبدالولي الاركاني
ـ http://rb2.in/7zJ
احمد العجمي
ـ http://rb2.in/7zK
مشاري العفاسي
ـ http://rb2.in/7zL
سعد الغامدي
ـ http://rb2.in/7zM
ابو بكر الشاطري
ـ http://rb2.in/7zN. القران كاملا بدون تشغيل نت
samedi 16 mai 2015
Sababu Zilizosaidia Ndege ya Nkurunzinza Isitunguliwe Bujumbura
Pierre Nkurunzinza janja janja sana huyu
bwana,hata jana nchini mwake hakuondoka
na ndege ya nchi yake...ili kuwapoteza
maboya maadui wake alikodi ndege toka
South Africa ikaja kumchukua Bujumbura -
Dar es Salaam.Hata "Call Sign" yake
haikuwa inaita kama "Burundi 001" ilikuwa
inaita kwa Registration number yake ambayo
ni ya South Africa,maana nasikia alipanda
LearJet45(LJ45) yenye usajili wa ZS-OPR
ambayo ni usajili wa Afrika Kusini
Sasa kama Rais alifikia kukodi ndege toka
Afrika Kusini maanake alianza kunusa harufu
za uasi toka kwa watu wake,ambao pengine
angekuja na ndege ya Serikali kwayo
Marubani wake ni Wanajeshi wangeweza
kumuhujumu kwa namna yoyote ile.Hii
kukodi ndege ya nchi nyingine na
kuendeshwa na marubani ambao ni raia wa
nchi nyingine ya Afrika kusini ndio
imemuokoa jana Rais Pierre Nkurunzinza,laa
sivyo kama angekuwa amekuja na ndege ya
Serikali ya Burundi basi historia ya mwaka
1994 ingejirudia jana ktk uwanja wa ndege
wa Bujumbura kwa Nkurunzinza kuripuliwa
na ndio ingekuwa mwanzo wa machafuko
kati ya wale wanaomuungu Nkurunzinza na
wale wasio watiifu kwake
Kwenye usafiri wa anga kuna kitu wanaita
"Call Sign",huu huwa ni muito wa ndege au
utambulisho wake inapokuwa ktk safari
zake,utambulisho huu unaweza kuwa ni
namba ya usajili ya ndege,au jina la kampuni
ya ndege au jina "mahalia" linaloambatana
na "flight number"...kwa mfano wa jina
"mahalia" kwa ndege za shirika la umma la
Afrika Kusini ni "springbok",huyu ni mnyama
mwenye sifa na heshima kwa S.Africa,British
Airway wao ni "Speedbird",wakati mashirika
kama Fly 540 hujiita kama "swift Tango" n.k
Kwa mfano Tanzania shirika la ndege la fast
jet "call sign" yake hujiita kama "Greybird"
kutokana na picha ya ndege wa kijivu kama
alama ya ndege pale mkiani mwa ndege
zao.Kwa hiyo hata watu mashuhuri duniani
huwa na "call sign" zao wawapo angani au
ardhini iwe tu ni ndani ya ndege,mfano Rais
wa Marekani akiwa ndani ya ndege ya Rais
"call sign" yake huwa ni "Air Force One",
akiwa ndani ya meli ataitwa kama "Marine
One";kwetu hapa Tanzania ndege ikiwa
imebeba rais hujitambulisha kama "Tanzania
One",akiwa makamu wa Rais "Tanzania
Two" na akiwa Waziri mkuu rubani huita
"Tanzania Three".
Tukirudi kwenye mada ya Nkurunzinza
Pierre,jana wakati akiondoka Bujumbura kuja
Tanzania hakujitambulisha kama "Burundi
One" bali marubani wa kukodiwa toka Afrika
Kusini waliita kwa "Call sign" ya "ZS-
OPR",kitu ambacho kilifanywa kuwa siri ya
nani alikuwa ndani ya ndege hiyo,kwa aina
ya usajili wa ndege maadui wa Nkurunzinza
iliwawia vigumu kujua hasa ni nani yupo
ndani ya ndege hiyo na wasingefanya lolote
sababu usajili wa ndege ilikuwa ni Afrika
Kusini.
Mara baada ya mkutano hapa
DSM,Nkurunzinza alitaka kurudi kwa lazima
Bujumbura ili akahutubie Taifa kupitia Radio
na Tv za Serikali,kujiamini kwako kulikuwa na
sababu ya aina ya ndege aliyotumia ili kutua
ktk uwanja wa Bujumbura,kitu ambacho
aliamini maadui zake hawawezi "kuitungua"
kwa sababu zifuatazo:
(1)Ilikuwa ni ndege ya kiraia toka Afrika
Kusini
(2)Ilikuwa ndege inayoongozwa na marubani
raia wa S.Afrika.
Kuitungua ndege hii yenye marubani wa
Afrika Kusini tena "raia" waliombeba "mteja"
aliyeikodi,ingeamsha mgogoro mpya wa
kidiplomasia ambao "maadui" zake
wasingeweza kukubali mtego huo
Nkurunzinza aliondoka Dar es Salaam
milango ya saa 1815hrs,lakini baada ya
kama saa moja na nusu alirudi tena kutua
kwenye uwanja wa ndege wa Dsm,hii ni
baada ya kujaribu kutua mara mbili katika
uwanja wa Bujumbura kwa "Call sign" ya "
ZS-OPR" badala ya "Burundi One".Hata
baada ya rubani kuulizwa mara kadhaa
"status of souls on board" alisisitiza kuwa ni
"customers" waliomkodi toka Bujumbura-
Dsm-Bujumbura.
Baadae Rubani wa ndege akaambiwa "Clear
to land at your own risk"...hii ni baada ya
chumba cha waongoza ndege kuwa tayari
mikononi mwa wanajeshi wasio watiifu kwa
Nkurunzinza,hali hii ilimfanya Rubani
kugeuza na ku-opt Entebbe International
Airport,ambapo Mseven hakuwa tayari,ndipo
Pierre akaamua kurudi kwa "Baba" zake
Tanzania,mpaka sasa hajulikani amefikia
sehemu gani ktk jiji la Dsm,hata Waziri
Membe alipooulizwa leo kuwa Nkurunzinza
yupo Tz sehemu gani,hakutaka kusema
mahali alipo
Hiki ndio kitu pekee kilichomuokoa Brother
Nkurunzinza,vinginevyo maadau zake
waliokuwa wamefunga mipaka na kutawala
viwanja vya ndege wangefanya lolote
endapo tu ndege aliyokuwa anatumia
ingekuwa ni ile ya Rais ambayo huitumia
mara kwa mara,maana kwa maadaui zake
kurudi kwa Nkurunzinza toka Dsm na
kuhutubia Taifa ingekuwa ni pigo kwani
ingezuia vuguvugu na harakati za kumuondoa
madarakani zilizokwisha anza.
Lakini mbadala mwingine kama Nkurunzinza
angekuwa ametumia ndege ya Rais kurudi
Bujumbura kwa kulazimisha ni ima maadui
zake wangeitungua ndege yake au
wangeruhusu itue na kumshikiria Pierre kwa
nguvu,lakini kwa sababu ya "mbeleko" ya
ndege ya "kiraia" yenye marubani " raia"
toka nchi ya Afrika Kusini,Maadui zake
walizingatia diplomasia ya kimataifa na
kumsihi rubani asitue Bujumbura "if and only
among the souls on board,the soul of
Nkurunzinza was boarded"...hii ndio ilikuwa
nafuu ya Bro Nkurunzinza na "ujanja" wa
team yake ya kijasusi,vinginevyo leo
tungekuwa tunaongea mengine na pengine
kama yale ya mwaka 1994 ambapo baada ya
mkutano wa Dsm,watu walipokuwa wanarudi
Makwao wakatunguliwa.
mardi 12 mai 2015
Gasya upande wa Buterere Bujumbura
Hiyo ni vedeo ya gisi raia leo quarter ya buterere wamemshambulia polici wakike baada ya kushtumiwa kufyatuwa masase yakuuwa dhidi ya waandanaji
https://m.youtube.com/watch?v=6MBtyUk9xHg
lundi 11 mai 2015
Picha za Shilole Zazua Gumza Mtandaoni, Mchumba Wake Nuhu Mziwanda Asema Haya Kumtetea
I love you is My Country aka Shilole Kiuno
Amejikuta tena leo akiwa Gumzo la watu
mitandaoni baada ya picha zenye utata
akiwa jukwaaa kuzagaa kwenye mitandao
mbali mbali na kujadiliwa hasa Instagram.....
Baada ya Picha hizo Kusambaa Mpenzi
wake aliingia mtandaoni na kuposti haya
maneno kumtetea:
" Show ni movement na uwezi mkataza mtu
kupiga picha ukiwa kwa stage'na kuna nguo
za show na nguo za kutoka out
kikawaida'ukiruka ruka sana sidiria ni rahisi
kuchomoka akina dada mnafaham na mtu
yupo stejini anakua hajitambui kama nini
kimetokea coz yupo stejin kwenye mood ya
kazi na kila mtu ni binadamu na ndio mana
wengine wanateleza kwa stage'huyo paparazi
aliopiga picha alifanikiwa kuzoom na kipata
picha mbaya lakin katika hali ya kawaida na
watu waliokua wakicheza nae hawakuweza
kugundua lolote'na kiubinaadamu kama
muhandishi wa habari hakupaswa kuchagua
picha ambayo kaonekana vibaya mana naamini
alipata picha nyingi nzuri tu za kupost ila
aliamua tu kumchafua'So Mashabiki
kumbukeni alikua yupo kazini hakupanga
itokee ivyo na yote mradi atoe burudani nzuri
kama mlivyomzoea''ambae hana upeo mdogo
wa kufikiria ataongea shit ila kaa jiulize
ingekutokea wewe ungesemaje?naomba
mtusaidie kurepost hii habari'tunawapenda
sana"
Haya ni Baadhi ya Maoni ya watu mbali
mbali waliokasirishwa na Picha hizo:
MrekebishaTabia
Sitaman hata kuibandika hii picha
hapa...kichefuchefu!! hii tabia chafu
iliyopitiliza...na si mara yako ya kwanza
@shilolekiuno unafanya vituko tadhan mtoto
mdogo wkt mtu mzima na watoto wakubwa. Si
bahati mbaya amefanya kusudi... mtu
mwenyewe kuimba hujui na hata kujiheshimu
unashindwa? Kale kaheshima kadogo
ulikonako kwa shabiki zako utakapoteza, soon
tutasikia umerudi kucheza tamthilia. ....Sijui
umekunywa pombe za wapi wewe...!!!
ambassador_angelo
Pole mdada hahaha kazi ndo zilivyobwe kioo
cha jamii siku nyingine vaa vizuri sawa mdada
mzuri eeeee
mimas_wa_pwiiii
sasa@shiloleliuno kwani hakunaga nguo zenye
heshma Dada yangu mbona hiyo nguo IPO
wazi kupitiliza ivi mbona wanaume wanavaa
vizuri tu kwenye shoo zao why nyie madada
hamujiheshimu asee hii sibahti mbaya
imekusudiwa nguo yenyewe ni uchi tosha na
iyo sidiria ulitegemea Haiti vukaa ebu
jiheshimuni bwana munaboaa tuachieni ujinga
wenu stejin kwani mukivaa nguo zinazo still
hapo kidogo mnakuwa hamujui kuchezaa
sheeenzeee zenu wakaa uchi wotee
nyota_ya_warembo
Anamaudhi sana havumiliki kabisa, utavumilia
hili baadae anaibuka najingine aisee
tutamvumilia mpaka lini!!!!!! Nampenda sana
lakini anakero sana, niaibu kusema mbele za
watu shilole 'nampenda' watakushangaa
johar_seleman
Afu hapo mbona km kabambiwa ivi mcheki uyo
mshua anavomtolea minjicho hahaaaaa ni
shigidiiii shidaaa
dimanche 10 mai 2015
UKITAKA MAPENZI YA ALLAH, THIBITIKA KATIKA TAWHIYD
Assallamun allaykoum wa rahmatullah wa barakatuh
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Na kama leo siku yetu tukufu ya ijumaa tupate sabuni ya roho kwa haya mawaidha :
🌙
UKITAKA MAPENZI YA ALLAH, THIBITIKA KATIKA TAWHIYD
Kumtii Allaah amri Zake, kumpwekesha bila ya kumshirikisha ni katika dalili za kumpenda Allaah na kupata mapenzi Yake pia. Waumini wa kikweli humpenda Allaah Pekee bila ya kumshirikisha yeyote katika mapenzi Yake. Kinyume chake ni kuelemeza mapenzi kwa wasiokuwa Allaah. Kauli Yake Subhaanahu wa Ta’aalaa:
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ
Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah kuwa niwanaolingana (na Allaah) wanawapenda kama mapenzi (yapasavyo) ya kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. [Al-Baqarah: 165]
Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akaonya Waumini kwamba ikiwa watamkanusha na kuikanusha Dini Yake basi Anaweza kuwaleta wengineo ambao Atawapenda nao watampenda kikweli, Anasema hivyo:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ
Enyi mlioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda; wanyenyekevu kwa Waumini, wenye nguvu juu ya makafiri; wanafanya jihaad katika njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama ya (yeyote) anayelaumu [Al-Maaidah: 54]
Anayempenda Allaah kikweli hupenda yale Anayoyapenda Allaah kama kumpwekesha kwa aina zote za Tawhiyd, na huchukia yale Anayochukia Allaah kama kumshirikisha, na hapo iymaan ya mtu inathibitika. Ndipo sharti mojawapo ya “laa ilaaha illa Allaah” ikawa ni: “Kupenda ambako kunaondowa kinyume chake”; yaani kutokupenda au kuchukia”. Ndio pia maana ya “Al-Walaa Wal-Baraa” (Kuwa na urafiki wa karibu na kujitenga).
Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametaja hayo katika Hadiyth zifuatazo:
Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa):
((أَوْثقُ عُرَى الإِيمان: الموالاَةُ في الله والمعاداةُ في الله، والحب في الله، والبغضُ في اللَّه عز وجل))
Shikizo thabiti kabisa la iymaan ni kuwa na urafiki wa karibu kwa ajili ya Allaah na kujitenga kwa ajili ya Allaah, na kupenda kwa ajili ya Allaah, na kuchukia kwa ajili ya Allaah ‘Azza wa Jalla)) [Atw-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr na ameisahihisha Al-Abaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (2539))]
Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu):
((ثَلاَثٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ وَجَدَ حَلاَوَةَ الإِيمَانِ: أَنْ يَكُونَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِمَّا سِوَاهُمَا, وَأَنْ يُحِبَّ الْمَرْءَ لاَ يُحِبُّهُ إِلاَّ لِلَّهِ, وَأَنْ يَكْرَهَ أَنْ يَعُودَ فِي الْكُفْرِ كَمَا يَكْرَهُ أَنْ يُقْذَفَ فِي النَّارِ)) متفق عليه
((Mambo matatu atakayekuwa nayo, atapata utamu wa Iymaan: Allaah na Mtume Wake wawe vipenzi zaidi kwake kuliko wengineo, ampende mtu na wala asimpende isipokuwa kwa ajili ya Allaah, na achukie kurudi katika ukafiri baada ya Allaah kumwokoa kutoka huko kama anavyochukia kuingizwa motoni)). Al-Bukhaariy na Muslim
عَنْ أَبِي أُمَامَةَ ، قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((مَنْ أَحَبَّ فِي اللَّهِ وَأَبْغَضَ فِي اللَّهِ وَأَعْطَى لِلَّهِ وَمَنَعَ لِلَّهِ فَقَدِ اسْتَكْمَلَ الإِيمَانَ))
Kutoka kwa Abi Umaamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Atakayependa kwa ajili ya Allaah, akatoa kwa ajili ya Allaah, akazuia kwa ajili ya Allaah, atakuwa amekamilisha iymaan)) [Abu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy (4681)
عَنْ أَنَسٍ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لاَ يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَلَدِهِ وَوَالِدِهِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ)) أَخْرَجَاهُ
Imepokewa toka kwa Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) wamba Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Mmoja wenu hawi Muumini mpaka anipende mimi kuliko watoto wake na baba yake na watu wote)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
Mafanikio ya duniani na ya Aakhirah hayapatikani isipokuwa pale Muislamu atakapopenda kwa ajili ya Allaah na akachukia kwa ajili ya Allaah na akafuata maamrisho ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hapo atakuwa miongoni mwa vipenzi vya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
عَنْ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ:قَالَ النَّبِىُّ صلى الله عليه وسلم: ((إِنَّ مِنْ عِبَادِ اللَّهِ لأُنَاسًا مَا هُمْ بِأَنْبِيَاءَ وَلاَ شُهَدَاءَ يَغْبِطُهُمُ الأَنْبِيَاءُ وَالشُّهَدَاءُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ بِمَكَانِهِمْ مِنَ اللَّهِ تَعَالَى)) قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ تُخْبِرُنَا مَنْ هُمْ. قَالَ: ((هُمْ قَوْمٌ تَحَابُّوا بِرُوحِ اللَّهِ عَلَى غَيْرِ أَرْحَامٍ بَيْنَهُمْ وَلاَ أَمْوَالٍ يَتَعَاطَوْنَهَا, فَوَاللَّهِ إِنَّ وُجُوهَهُمْ لَنُورٌ وَإِنَّهُمْ عَلَى نُورٍ, لاَ يَخَافُونَ إِذَا خَافَ النَّاسُ وَلاَ يَحْزَنُونَ إِذَا حَزِنَ النَّاس)) وَقَرَأَ هَذِهِ الآيَةَ: ((أَلاَ إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّهِ لاَ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ))
Kutoka kwa 'Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Hakika miongoni mwa waja wa Allaah ni watu ambao si Manabii wala si mashahidi. Manabii na mashahidi watawaonea wivu kutokana na vyeo vyao vya juu mbele ya Allaah Ta’aala Siku ya Qiyaamah)) Wakasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Tujulishe nani hao?” Akasema: ((Hao ni watu waliopendana kwa ajili ya Allaah bila ya kuwa na uhusiano wa damu, wala hawakuungana kwa ajili ya mali. Naapa kwa Allaah! Nyuso zao zina nuru nao wako katika nuru. Hawaogopi wanapoogopa watu, wala hawahuzuniki wanapohuzunika watu)) Kisha akasoma Aayah hii: ((Tanabahi! Hakika awliyaa (vipenzi) wa Allaah hawana khofu juu yao, na wala hawatohuzunika)) [Abu Daawuwd (3527) na ameisahihisha Al-Albaaniy (Aayah: Suwrat Yuwnus: 62)]
Tambua pia kwamba mapenzi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) hayakamiliki bila ya kumfuata Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama Anavoamrisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) katika Qur-aan:
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni (mimi Rasuli Wake), Atakupendeni Allaah [Aal-‘Imraan: 31]
Kwa maana; kufuata Sunnah zake bila ya kuwenda kinyume na mafundisho yake na bila ya kuzusha mambo katika Dini.
Wanawake toeni Sadaka
ALISEMA MTUME MUHAMMADI(S.A.W) : ENYI WANAWAKE TOWENI SWADAKA KWAWINGI, YAHAKIKA MIMI NIMEKUONENI MKIWA WENGI NDANI YA MOTO WAJAHANNAMA , WANAWAKE WAKASEMA KUMUULIZA MTUME S.A.W : KWANINI TUPO WENGI NDANI YA MOTO WAJAHANNAMA EWE MTUME WA ALLAH? MTUME MUHAMMADI (S.A.W) AKASEMA : MWAZIDI KULANI LANI KILA WAKATI NA MWAKUFURU WEMA (YANI HAMSHUKURU MEMA MTENDEWAWO NA WAUMEZENU BALI MWAKANUSHA KUWA HAKUNA KHERI ZOZOTE MZIPATAZO KUTOKA KWA WAUME ZENU)!!!
bukhari na muslim.
allahumma swalli alaa muhammadi(s.a.w)
samedi 9 mai 2015
Mja Atafufuliwa Kwa Kitendo Alichofariki Nacho
Hadiyth :
Mja Atafufuliwa Kwa Kitendo Alichofariki Nacho
عَنْ جَابِرٍ (رضي الله عنه) قَال: قَالَ النَّبِيَّ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((يُبْعَثُ كُلُّ عَبْدٍ عَلَى مَا مَاتَ عَلَيْهِ)) رواه مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) ambaye amesema: Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Kila mja atafufuliwa katika hali aliyofia)).[1]
Mafunzo Na Hidaaya:
Hima ya kutenda mema na kubakia katika istiqaamah ili kitendo cha mwisho kabla ya kufariki kiwe ni kitendo chema, na kiwe ni kiliwazo siku ya kufufuliwa. [Al-Hijr 15: 99, Al-‘Imraan 3: 102].
الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَامٌ عَلَيْكُمُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Ambao Malaika huwafisha katika hali njema watasema: (kuwaambia Waumini): “Salaamun ‘Alaykum (amani iwe juu yenu)! Ingieni Jannah kwa yale mliyokuwa mkitenda”[2]
Umuhimu wa kupata husnul-khaatimah (mwisho mwema) kabla ya kuaga dunia na sio kuwa katika maasi, khasa pale mtu anapofikia katika umri mkubwa.
Umuhimu wa kuomba du’aa ya Sunnah: ((Allaahuuma Yaa Muqallibal-Quluub Thabbit Qalbiy 'Alaa Diynik – Ee Allaah Mgeuza nyoyo, Thibitisha moyo wangu katika Dini Yako))[3], na Du’aa ya Nabii Yuwsuf (عليه السلام (: (([Allaahumma] Anta Waliyyi fid-Duniya wal-Aakhirah, Tawaffaniy Musliman wa-Alhiqniy bis-Swaalihiyn – Ee Allaah, Wewe ni Mlinzi wangu duniani na Aakhirah, Nifishie katika Uislamu na nikutanishe na (waja) wema))[4], ili ajaaliwe mtu kuwa na mwisho mwema kwani ((Allaah Huingia kati ya mtu na moyo wake))[5]. Na hivyo kuna hatari kwa mtu ya kubadilika na kutoweka Iymaan yake. [Hadiyth: ((Mmoja katika nyinyi hufanya vitendo vya watu wa Peponi mpaka baina yake na Pepo ikawa dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na mmoja katika nyinyi hufanya ‘amali ya watu wa motoni mpaka baina yake na moto ikawa dhiraa, na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa peponi, akaingia peponi))].[6] Na katika riwaaya inayomalizikia: ((…’amali zinahesabika za mwisho)).[7]
Hatari ya kutenda maasi yakaja kuwa ndio kitendo cha mwisho cha mja, kwani mauti yanamfikia mtu bila ya taarifa, mfano mwenye kusikiliza muziki huku akiendesha gari badala ya kusikiliza Qur-aan.
Kilicho muhimu ni ‘amali za mwisho, basi atakayefanya ‘amali zake kuwa ni bora katika uhai wake wa mwisho atapata bishara njema na kheri Siku ya Qiyaamah, na atakayefanya maovu katika uhai wake wa mwisho atakutana na shari huko Aakhirah [An-Nahl 16: 97].
Kutochoka wala kulegea katika kufanya mema na kuacha mabaya kwa kuwa hakuna anayejua wakati gani atatembelewa na Malakul Mawt (Malaika wa kutoa roho).
DALILI ( REFERENCE)
[1] Muslim.
[2] An-Nahl (16: 32).
[3] At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan.
[4] Yuwsuf (12: 101).
[5] Al-Anfaal (8: 24).
[6] Al-Bukhaariy na Muslim.
[7] Al-Bukhaariy.
MAMBO 8AMBAYO YANAKUPA AFYA BORA NA KUONDOA MARADHI
MAMBO 8AMBAYO YANAKUPA AFYA BORA NA KUONDOA MARADHI:
Rumman.
Mtindi
Vitunguu Saumu.
Vitunguu majina.
Grean tee.
Ngano ili ok oboe wa
Maboga.
brokly hili neno kwa kirabu lkn ni jamii ya mboga.
--------------------------------------MAMBO 3 YANALETA MARADHI KTK MWILI.
1-Maneno mengi.
2-Kulala saana.
3-Kula sana.
-------------------------------------MAMBO 4 YANADHOOFISHA MWILI.
1-Kufikiria sana.
2-Kuhuzunika.
3-Kukaa na njaa.
4-Kukesha.
-------------------------------------MAMBO 4 YANAFAFANYA USO UWE NA BASHASHA .
1-Kumcha Allah.
2-Kujitosheleza.
3-Ukarimu.
4 - Uwe mtu Muruwa.
-------------------------------------MAMBO 4 YANALETA RIZKI.
1-qiyamu ley.
2-Kukithirisha istighfar hasa wakati wa usiku sana.
3-Kutekeleza ahadi.
4-kufanya adhkar mwanzo wa Siku na mwisho wa Siku.
-------------------------------------MAMBO 4 YANAZUIA RIZKI.
1-Kulala wakati wa asubuhi.
2-Kutoswali.
3-Uvivu.
4.Kua na khiyana.
-------------------------------------KILA UNAPOTAKA KUFANYA DHAMBI KUMBUKA AYA HIZI TATU.
- الم يعلم بأن الله يری"
-ولمن خاف مقام ربه جنتان"
-ومن يتقي الله يجعل له مخرجا"
-------------------------------------UKIPENDEZEWA NA HAYA MANENO USIONE TABU KUMRUSHIA MWENZIO PINDI UNAPOMALIZA TU KUSOMA MSG HII.
UJIRA WAKO KWA ALLAH NI KAMA UJIRA WA ALIEANDIKA MSG HII.
WABILLAHI TAWFIQ.
jeudi 30 avril 2015
Inscription à :
Articles (Atom)