Google tag

jeudi 17 novembre 2016

The Rock atajwa kuwa mwanaume mwenye mvuto zaidi 2016

Jarida la The People limemtangaza muigizaji Dwayne ‘The Rock’ Johnson kuwa mwanaume mwenye mvuto zaidi kwa mwaka 2016 (Sexiest Man Alive).

Baada ya kutangazwa na jarida hilo, The Rock kupitia mtandao wake wa Twitter aliandika, “He’s sweet, smart—and sculpted! Dwayne @TheRock Johnson is PEOPLE’s 2016 .”

Muigizaji huyo amechukuwa nafasi hiyo baada ya mchezaji mstaafu wa timu ya taifa ya Uingereza, David Beckham kutangazwa mwaka uliopita.

Fc Barcelona kupata wazamini wapya

Klabu ya Barcelona imeingia mkataba mpya na kampuni ya Rakuten ya Kijapan kwa ajili ya kudhamini timu hiyo kwa miaka minne.

Rakuten ni kampuni ya kuuza bidhaa kupitia mtandaoni wameingia mkataba na Barcelona wenye thamani ya pound milioni 200 ambazo ni zaidi ya bilioni 540 za kitanzania ni kampuni ya uuzaji wa vitu online kupitia tovuti yao na websites yao ni ya 11 kwa uingizaji mapato duniani, kwa jina jingine wanajiita kama “Japan’s Largest Internert Shopping Mall”.

Kuanzia msimu ujao, jezi za Barcelona zitakuwa na nembo ya Rakuten kifuani badala ya Qatar Airways ambalo ni shirika kubwa zaidi.

Raymond atuhumiwa kuiba baadhi ya mistari kwenye wimbo wa msanii wa Singeli

Msanii wa WCB, Raymond anatuhumiwa kutumia baadhi ya mistari ya wimbo wa msanii wa muziki wa Singeli, Manyo Lee kwenye wimbo wake mpya wa ‘Sugu’.

Akiongea na kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, Manyo Lee amesema, “Mimi nilisikia kwa watu tu kuwa dogo kachukuwa mashairi yangu. Juzi kati lilifanyika tamasha kubwa tu nikaona akiimba yale mashairi lakini nikaona kawaida tu lakini hivi karibuni nimeona kaachia video kabisa nikaona kumbe dogo yupo serious kabisa.”

“Kama pochi ya dada naiminya kwapani, namuamini Mungu funga virago shetani. Joh Makini akiwa mweusi Barakah tumuite nani?,”
mistari ambayo Raymond anadaiwa kuchukua kwenye wimbo wa msanii huyo unaoitwa ‘Mwendo wa Pushapu’.

Naye Manyo Lee katika wimbo wake aliouachia mwezi Septemba mwaka huu ameimba,
“Kama pochi ya dada naiminya kwapani, namuamini Mungu virago funga shetani. Makini ajiite mweusi na Nigga ajiite nani?.”

Brazil kupanda hadi nafasi ya pili viwango vya Fifa mwezi huu

Timu ya soka ya wanaume ya Brazil inatarajiwa kupanda hadi kwenye nafasi ya pili kwenye viwango vipya vya mwezi huu kwenye shirikisho la soka duniani (Fifa) vinavyotarajiwa kutangazwa Novemba 24.

Viwango vya mwezi uliopita timu hiyo ilishika nafasi ya tatu huku nafasi ya pili ikishikiliwa na timu ya taifa ya Ujerumani na Argentina akiongoza orodha hiyo.

Hata hivyo imedaiwa kuwa timu hiyo ineweza kushika nafasi ya kwanza kwenye viwango hiyo endapo Argentina ingefungwa na timu ya taifa ya Colombia kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia Jumanne ya wiki hii.
Kwa sasa Brazil inaongoza kundi la timu za bara la Amerika ya Kusini zinazowania kufuzu kwenye kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018 ikiwa na pointi 27.

Mr T-Touch aeleza kwanini watayarishaji wa muziki hutoa beat bure kwa wasanii

Producer aliyetengeneza hits kibao, Mr T –Touch amefunguka kwa kuitaja sababu inayowafanya watayarishaji wengi wa muziki kuwapatia beat bure wasanii.

Mtayarishaji huyo amekiambia kipindi cha Ladha 3600 cha EFM, “Tunatoa beat bure ili tuweze kuaminiwa. Nimetoa beat za bure kwa takribani miaka mitatu.”

Touch ameongeza kuwa hakuna producer anayenufaika kupitia studio yake labda awe na kazi nyingine nje ya muziki. Kwa sasa Mr T anamiliki studio yake inayojulikana kwa jina la Touchez Sound aliyoifungua mwezi Julai mwaka huu.

Wayne Rooney ajutia kulewa kwenye sherehe ya harusi

Wayne Rooney amemuomba radhi kaimu meneja wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate baada ya picha kutolewa zikimuonesha akiwa mlevi wakati wa sherehe ya harusi.

Nahodha huyo alihudhuria sherehe hiyo ya harusi katika hoteli ambayo timu hiyo ilikuwa inakaa wakicheza mechi ya kimataifa.

Nahodha huyo amesema kupitia taarifa kwamba picha hizo "hazifai".

Amesema ingawa picha hizo zilipigwa wakati wake wa kupumzika, "hazifai kwa mtu wa hadhi" yake.
Gazeti la The Sun la Uingereza lilichaisha picha hizo ambazo zinamuonesha Rooney, 31, akiwa kwenye sherehe usiku wa Jumamosi baada ya mechi ya England ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Scotland.

England walishinda mechi hiyo.
Chama cha Soka cha England (FA) kimesema kitathmini upya sheria kuhusu mambo ambayo wachezaji wanaruhusiwa kufanya wakati wao wa kupumzika.

Gazeti la The Sun linadai FA imechukua hatua hiyo kwa sababu wachezaji 10 wa England walikaa kwenye kilabu cha usiku hadi saa 04:30 GMT Jumapili.

Rooney hakucheza mechi ambayo England walitoka sare 2-2 na Uhispania Jumanne kwa sababu ya jeraha ndogo kwenye goti.