Google tag

jeudi 7 septembre 2017

Wanaume mpo tayari kwa nguo hii ya ndani?

Kumekuwa  na idadi kubwa ya wabunifu wa mavazi mbalimbali duniani, jopo la wabunifu wamekuja na aina mpya ya nguo ya ndani kwa upande wa wanaume. Je! wewe kama mwanaume upo tayari kutinga nguo hii kwa sasa.

Rick Ross na Briana Camille wapata mtoto wa kike

Rapper kutoka Maybach Music Group(MMG), Rick Ross amebahatika kupata mtoto wake wa kwanza na mwanamitindo Briana Camille.

Licha ya kuwa wawili hao hawakuwahi kutangaza kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na wala hawakuwahi kuonekana pamoja ila wamebahatika kupata mtoto wa kike. Inaelezwa kuwa Camille alikuwa akimsapoti rapper huyo mara kwa mara na kupelekea watu kuhisi wapo katika mahusiano hayo.
Kwa sasa familia ya Boss wa MMG imekuwa na watoto watatu ambapo wawili ni wakeki na mmoja ni wa kiume, ambao ni Toie Roberts na William Roberts III.
wa mujibu wa vyanzo vya karibu vimeeleza kuwa mtoto huyo amezaliwa siku ya Labor Day wikiendi iliyopita na tayari ameshaanza kupokea zawadi kutoka kwa baba yake.

Wachezaji 47 wa Afrika wanaocheza Ligi Kuu England

Katika msimu wa 2017/2018 kutakuwa na wachezaji 47 kutoka nchi za Afrika wanaochezea klabu za Ligi Kuu ya England.

Hii ni kwa mujibu wa orodha ya wachezaji 25 wa kila timu ambao waliwafilishwa kwa Ligi ya Premia.
Wachezaji hao ni asilimia 9 ya wachezaji wote katika ligi hiyo, ambalo ni ongezeko ndogo ukilinganisha na msimu uliopita ambapo walikuwa 45.

Leicester City wanaongoza wakiwa na wachezaji saba, wakifuatwa na Crystal Palace, Newcastle United na West Ham ambao wana wachezaji wanne kutoka Afrika kila klabu.
Ni klabu moja pekee - Burnley - ambayo haina mchezaji wa kutoka Afrika msimu huu.
Senegal inaongoza kwa kuwa na wachezaji wengi zaidi, tisa, ikifuatwa na Nigeria iliyo na wachezaji sita.
DRC, Ghana na Ivory Coast zina wachezaji watano kila nchi.
Wachezaji kwa nchi (zenye wachezaji wengi):

Senegal
Pape Souare
Idrissa Gana Gueye
Oumar Niasse
Sadio Mane
Mohamed Diame
Henry Saivet
Mame Diram Diouf
Chekhou Kouyate
Diafra Sakho

Nigeria
Alex Iwobi
Ahmed Musa
Wilfred Ndidi
Kelechi Iheanacho
Isaac Success
Victor Moses

Ivory Coast
Wilfred Zaha
Yaya Toure
Eric Bailly
Wilfried Bony
Serge Aurier

Ghana
Jeffrey Schlupp
Daniel Amartey
Christian Atsu
Jordan Ayew
Andre Ayew

DRC
Benik Afobe
Yannick Bolasie
Elias Kachunga
Chancel Bemba
Arthur Masuaku

Wachezaji kwa klabu:

AFC Bournemouth
Benik Afobe (DRC)

Arsenal
Mohamed Elneny (Misri)
Alex Iwobi (Nigeria)

Brighton & Hove Albion
Gaetan Bong (Cameroon)

Chelsea
Victor Moses (Nigeria)
Crystal Palace
Bakary Sako (Mali)
Jeffrey Schlupp (Ghana)
Pape Souare (Senegal)
Wilfred Zaha (Ivory Coast)

Everton
Yannick Bolasie (DRC)
Idrissa Gana Gueye (Senegal)
Oumar Niasse (Senegal)
Huddersfield Town
Elias Kachunga (DRC)
Steve Mounie (Benin)

Leicester City
Daniel Amartey (Ghana)
Yohan Benalouane (Tunisia)
Riyad Mahrez (Algeria)
Ahmed Musa (Nigeria)
Wilfred Ndidi (Nigeria)
Kelechi Iheanacho (Nigeria)
Islam Slimani (Algeria)

Liverpool FC
Sadio Mane (Senegal)
Joel Matip (Cameroon)
Mohamed Salah (Misri)

Manchester City
Yaya Toure (Ivory Coast)

Manchester United
Eric Bailly (Ivory Coast)

Newcastle United
Mohamed Diame (Senegal)
Chancel Mbemba (DRC)
Christian Atsu (Ghana)
Henry Saivet (Senegal)

Southampton FC
Sofiane Boufal (Morocco )
Mario Lemina (Gabon)

Stoke City
Eric Choupo-Moting (Cameroon)
Mame Biram Diouf (Senegal)
Ramadan Sobhi (Egypt)

Swansea City
Jordan Ayew (Ghana)
Wilfried Bony (Ivory Coast)

Tottenham Hotspur
Serge Aurier (Ivory Coast)
Victor Wanyama (Kenya)

Watford FC
Isaac Success (Nigeria)
Molla Wague (Mali)
Brice Dja Djedje (Ivory Coast)

West Ham United
Andre Ayew (Ghana)
Chekhou Kouyate (Senegal)
Arthur Masuaku (DRC)
Diafra Sakho (Senegal)

West Bromwich Albion
Allan Nyom (Cameroon)
Ahmed Hegazi (Misri)

lundi 5 juin 2017

Kiungo wa zamani wa timu ya Newcastle United Cheick Tiote afariki dunia

Kiungo wa zamani wa timu ya Newcastle United Cheick Tiote amefariki dunia akiwa an miaka 30 baada ya kuzimia wakati wa mazoezi nchini China, msemaji wa mchezaji huyo amesema.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alikaa miaka saba Newcastle na kuwachezea mechi 138 ligini.
Alihamia klabu ya Beijing Enterprises mwezi Februari.

"Ni kwa huzuni kubwa ambapo ninathibitisha kwamba Cheick Tiote alifariki mapema leo baada ya kuzimia wakati wa mazoezi," msemaji wake alisema.

"Hatuwezi kusema zaidi kwa sasa na tunaomba kwamba familia yake iheshimiwe kipindi hiki kigumu. Tunaomba maombi yenu."

Tiote alizaliwa Ivory Coast na alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.

Alianza uchezaji wake wa soka ya kulipwa Ubelgiji akiwa na klabu ya Anderlecht mwaka 2005 kabla ya kuhamia FC Twente ya Uholanzi ambapo alicheza mechi 86 na kushinda taji la ligi ya Eredivisie msimu wa 2009-10 chini ya meneja Steve McLaren.

Tiote, ambaye ni kiungo wa kati mkabaji, kisha alihamia Newcastle mwaka 2010 kwa £3.5m.

Mwaka 2011, alifunga bao linalokumbukwa sana alipowasaidia Newcastle United kujikwamua kutoka 4-0 chini Ligi ya Premia dhidi ya Arsenal na kutoka sare.

mardi 30 mai 2017

Totti kuaga AS. ROMA

Francesco Totti alitokwa na machozi alipokuwa anaaga baada ya kucheza mechi yake ya mwisho katika klabu ya AS Roma.

Mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 40 amechezea klabu hiyo kwa miaka 25.
Katika kipindi hicho, amefunga mabao 307 katika mechi 786 alizocheza.
Aliingia uwanjani mara ya mwisho dakika ya 54 mechi yao dhidi ya Genoa.

Roma walishinda 3-2 kupitia bao la dakika ya mwisho la Diego Perotti ambalo liliwahakikishia nafasi ya kucheza hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Baada ya mechi, Totti alisoma barua kwa mashabiki, na kusema: "Naogopa. Sijui siku za usoni zitakuwaje."

"Tafakari, kwamba wewe ni mtoto na umo katikati ya ndoto nzuri...na mamako anakuamsha uende shuleni.
"Unajaribu kurejea kwenye ndoto yako...unajaribu sana lakini huwezi.
"Wakati huu si kwamba ni ndoto, ni uhalisia. Na siwezi kurejea tena."
Nahodha Totti pia alipewa nambari 10 iliyowekwa kwenye fremu, nambari ya jezi yake.

Mkewe na watoto pia walikuwa uwanjani.
Anatarajiwa kuwa mkurugenzi katika klabu ya Roma lakini kumekuwepo na taarifa kwamba huenda akaelekea kwingine.

mercredi 17 mai 2017

Wafungwa wauawa wakijaribu kutoroka jela DRC

Idadi ya wafungwa wasiojulikana wameuawa kwa kupigwa risasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mapema leo baada ya jaribio la kuhepa kutoka gereza kubwa lililoko mjini Kinshasa.
Waziri wa sheria nchini humo, Alexis Thambwe Mwamba amesema baadhi ya wafungwa wapatao 100 wamekamatwa huku wengine hamsini na watano wakiendelea kusakwa.

Miongoni mwa wanaodaiwa kufanikiwa kutoroka ni mfungwa mmoja aliyekuwa akitumikia kifungo cha maisha gerezani kwa mauaji ya rais wa zamani wa DRC, Laurent Kabila.
Maafisa wa usalama wameanzisha oparesheni kali mjini Kinshasa ili kuwakamata wafungwa hao.
Aidha, baadhi ya wafungwa wameuawa kwa kupigwa risasi wakijaribu kukimbia .
Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema amewaona maafisa wa shirika la Msalaba Mwekundu, wakikusanya miili yao.
Miili ya waliofariki imepelekwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti mjini Kinshasa.

Hii sio mara ya kwanza kwa wafungwa kutoroka kutoka magereza nchini DRC kwani Januari mwaka uliopita, kisa kama hicho kilishuhudiwa mashariki mwa taifa hilo ambapo wafungwa hamsini walitoroka.
Miongoni mwa waliofanikiwa kutoroka ni wafungwa wa kesi za mauaji na ubakaji.
Mamlaka za magereza zimelaumiwa kwa visa hivyo kwa ulegevu huku magereza mengi yakiwa na msongamano.
Mashirika ya kutetea haki za kibanadam yanalaumu idara ya mahakama kwa kutokamilisha kesi haraka.

Sheddy Clever aiomba serikali kutumbua maprodyuza feki

Mtayarishaji wa muziki nchini, Sheddy Clever ameitaka serikali iweke sheria na viwango vya kudhibiti watayarishaji wa muziki feki ambao ni chanzo cha kusababisha nyimbo kutodumu mda mrefu katika tasnia hali inayopelekea kushuka kwa muziki bongo.

Sheddy amedai serikali inapaswa pia kusimama na kuangalia maslahi ya watayarishaji wa muziki kwani wamekuwa wakiwatajirisha wasanii huku wao wakibaki kwenye maisha yale yale.
“Maprodyuza feki ni wengi sana wale waliopo real ni wachache sana. Zamani kina P -Funk walikuwa wanatengeneza nyimbo zinadumu muda mrefu na ni kali lakini za sasa hivi imebidi ma director wa video wawe wabunifu kutengeneza video kali ili wimbo uonekane ni mzuri,” Sheddy alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.

Aongeaza, “Upande wa maslahi inabidi serikali ijipange ituwekee maslahi mazuri kwani mtayarishaji wa muziki kama anahitaji maisha mazuri itambidi awe anakazi nyingine na siyo kutegemea production tuu. Unaweza ukawa na hit kibao redioni lakini maisha yako yakawa ya tabu sana,”
Mtayarishaji huyo ameshatengeneza hit nyingi ikiwemo ‘Marry You’ ya Diamond na Ne-Yo.

Memphis Depay azua gumzo katika tuzo ya mchezaji bora Ufaransa

Mshambuliaji wa klabu ya Lyon, Memphis Depay, amepokea tuzo yake ya bao bora la mwaka. Wakati akienda kupokea tuzo hiyo ya heshima, ameonekana kuvalia Jacket lake mithili ya Msanii nguli wa Pop Duniani, Michael Jackson.

Nyota huyo wa timu ya taifa ya Uholanzi amenyakuwa tuzo hiyo baada ya kufunga bao akiwa umbali wa nusu ya Uwanja.
Depay mwenye umri wa miaka 23 amekuwa na mafanikio toka alipoondoka katika klabu ya Manchester United na kujiunga na klabu ya Lyon ya Ufaransa. Muonekano wake katika tuzo hizo umewaduwaza walio wengi na kuwavutia Ukimbini hapo kwa namna alivyovalia ikiwa ni jambo ambalo halikutarajiwa na wengi.
Nyota wa zamani wa Uholanzi Frank de beor aliwahi kumuonya Depay kwa kumtaka aweke akili yake zaidi uwanjani kabla ya kujiingiza katika mambo mengine ya nje ya uwanja.

Baada ya kufunga mabao 5 katika michezo 15 aliyoingia uwanjani, ni wazi sasa Depay anahisi ni muda wake muafaka way yeye kurudi katika ulimwengu wake wa mitindo anaoonekana kukosa kwa muda mrefu sasa.

mardi 9 mai 2017

Jaji wa mahakama kuu afungwa jela India

Mahakama ya juu zaidi nchini ndia imemhukumu jaji wa mahakama kuu ya Calcutta, kifungo cha miezi sita gerezani.
Jaji Chinnaswamy Swaminathan Karnan ndiye jaji wa kwanza wa mahakama kuu kufungwa gerezani katika historia ya nchi hiyo.
Jaji Karnan, amepatikana na kosa la kudharau mahakama siku moja baada ya hatua yake ya kujaribu kumhukumu jaji mkuu wa India na majaji wengine sita wa mahakama ya juu zaidi kifungo cha miaka mitano Jela.
Katika miezi ya hivi karibuni, kumekuwepo na hali ya mvutano na majibizano katika mahakama ya juu nchini India.
Mwezi Januari Jaji Chinnaswamy Karnan aliwashutumu majaji kadhaa wa mahakama ya juu nchini India kwa kuwa wafisadi.
Katika shutma hizo jaji huyo wa mahakama ya juu alimwandikia waziri Mkuu waraka maalum akitaka kuungwa mkono kwa juhudi zake zake za kutaka majaji hao wa mahakama wakamatwe, wachunguzwe na kutupwa jela miaka tano kwa madai ya ufisadi.

Hata hivyo jaji huyo hakutoa ushahidi wowote wa kuonyesha kwamba hao wakubwa zake ni wafisadi.
Kwanzia wakati huo uhasama kati yake na majaji wa mahakama ya juu nchini India ukazidi.
Majaji hao wakamtumia ilani wakimtaka afike mbele yao kwa kujibu mashataka ya kuwaharibia majina.
Hata hivyo alipuuza agizo hilo.
Jaji mkuu wa nchi hiyo katika siku za hivi karibuni ametoa agizo kwamba jaji huyo apelekwe hospitali kupimwa akili kwani alisema wanadhani kwamba si mzima wa akili.

Mwanafunzi anayefanana na Lionel Messi nchini Iran azua gumzo

Mwanafunzi mmoja nchini Iran amelazimika kupelekwa katika kituo cha polisi mwishoni mwa wiki iliyopita kisa na mkasa! Kufanana kulikokithiri na Lionel Messi.
Watu wengi katika mji wa Hamaden wamekuwa wakiomba kupiga picha na kijana huyo aitwaye Reza Parastesh, na hivyo kusababisha msongamano wa watu kila atakakokanyaga, hivyo polisi walilazimika kumhifadhi kwa muda ili kuondoa msongamano huo.

Mchanganyiko huo ulianza miezi michache iliyopita wakati baba wa kijana huyo aliyefanana mno na Messi alipompiga picha akiwa amevalia fulana ya timu ya Barcelona yenye namba kumi.
Reza Parastesh, ana umri wa miaka ishirini na mitano kwa sasa, hivi karibuni alianzisha mtindo wa ukataji nywele na kupunguza ndevu zake mithili ya mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina .
Reza Parastesh, kwa sasa amebatizwa jina 'Messi wa Iran' amejikuta kila wakati na kila mahali akiombwa kupiga picha na watu wa aina kwa aina katika mji wa nyumbani kwao Hameden, nchini Iran.
Kijana huyo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kwa sasa watu  wananiona mimi kuwa ndiye Messi wa Iran na kunitaka nifanye kiila kitu afanyacho Messi halisi, na pindi ninapotokeza mahali, watu hupatwa na mshtuko.

Nina furaha kubwa kuona kwamba ninawapa furaha na hili linapotokea linanipa ari mpya.
Parastesh aka Messi amekuwa ni mtu mwenye kufanyiwa mahojiano ya mara kwa mara na vituo vya habari na kufanikiwa kusaini mikataba mikubwa ya uoneshaji mavazi, na sasa ana fanya mazoezi makubwa ya kujua mbinu za mpira wa miguu ili akidhi vigezo vya Messi halisi.

samedi 6 mai 2017

Picha za utupu za mgombea urais Rwanda zavuja mtandaoni

Baada ya siku chache za Diane Shima Rwigara kutoka Rwanda kutangaza kugombea urais nchini humo, hatimaye amekutwa na skendo ya kuvujisha picha zake za utupu mtandaoni.

Diane 35, ambae ni msomi wa Uchumi na mtoto wa aliyekuwa tajiri maarufu nchini Rwanda Asinapol Rwigara, picha zake za utupu zilianza kusambaa mapema jana nchini Rwanda hususani kwenye mitandao ya kijamii kama WhatsApp na Facebook na baadae kutapakaa duniani kote.
Kwa mujibu wa mtandao wa Habari Pevu umeeleza kuwa picha hizo zilitumwa awali kwa njia ya e-mail na mtu aliyejiita ni Muandishi wa habari aliyejulikana kwa jina la Twahirwa Emmy huku akishinikiza kuwa mrembo huyo hafai kuchaguliwa kuwa Rais kwa vitendo vyake vichafu vya kupiga picha za utupu.

Hata hivyo Jitihada za kumpata mrembo huyo kuzungumzia picha hizo zilizovuja ziligonga mwamba baada ya waandishi wa habari nchini Rwanda kumsaka bila mafanikio.
Uchaguzi mkuu wa Rais nchini Rwanda unatarajiwa kufanyika mwaka huu mwezi wa Augosti, na mpaka sasa kuna wagombea watatu tuu ambao ni Mpayimana Philippe ambae ni mgombea binafsi na Franck Habineza kutoka chama cha Green pamoja na Diane Rwagira wote wakitarajiwa kuleta upinzani mzito kwa Rais Paul Kagame .

jeudi 4 mai 2017

Aaron Lennon kuugua ugonjwa wa ki Akili

Winga wa klabu ya Everton Aaron Lennon amezuiliwa chini ya kifungu cha polisi cha afya ya kiakili kuhusu wasiwasi wa hali yake.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alipelekewa hospitalini kwa ukaguzi wa kiafya baada ya maafisa wa polisi kuitwa katika eneo la Salford siku ya Jumapili.

Lennon kwa sasa anapata matibabu kwa ugonjwa unaosababishwa na shinikizo la kiakili ,kulingana na klabu hiyo.
Mchezaji huyo wa Uingereza aliyejiunga na Everton kutoka Tottenham 2015 hajachezea kikosi cha kwanza tangu mwezi Januari.

Maafisa wa polisi wa Manchester walisema: Polisi waliitwa saa kumi na nusu mchana kufuatia wasiwasi wa mtu mmoja aliyekuwa katika barabara ya zamani ya eneo la Eccles .
Maafisa wa polisi waliitikia wito huo na mtu mwenye umri wa miaka 30 alikamatwa chini ya kifungu cha 136 cha afya ya kiakili na kupelekwa hositali kwa ukaguzi.

Habari kuhusu kulazwa kwa Lennon zilivutia ujumbe wa kumuombea katika mitandao ya kijamii miongoni mwa wachezaji wa soka na mashabiki wa klabu yake ya zamani na ya sasa.

Conte: Kuna Antonio wawili, na mmoja ni mnyama

Meneja wa klabu ya Chelsea Antonio Conte amesema yeye huwa "mnyama" wakati wa mechi, baada yake kushuhudia viongozi hao wa Ligi ya England wakilaza Everton 3-0 Jumapili.

Mwitaliano huyo alisherehekea uwanjani na wachezaji wake baada ya mchezo kumalizika Goodison Park, ambapo mabao yalifungwa na Pedro, Gary Cahill na Willian.

Chelsea wanahitaji kushinda mechi tatu kati ya nne walizosalia nazo msimu huu kushinda taji la ligi, msimu wa kwanza chini ya Conte.
"Kuna Antonio wawili. Ni watu wawili tofauti," alisema Conte, 47.
"Wakati wa mechi, najua kwamba mimi huwa mnyama.

"Baada ya mechi, lazima niwe nimetulia baada yetu kushinda lakini nafikiri ni vyema kusherehekea (ushindi) na wachezaji, wafanyakazi na mashabiki. Hili lina maana kubwa katika maisha yangu."

Conte, ambaye alishinda mataji matatu mtawalia ya ligi ya Serie A akiwa na Juventus kati ya 2012 na 2014, anafahamika sana kwa vituko vyake na nguvu anazoonekana kuwa nazo akielekeza mechi inapokuwa inaendelea.
Alisherehekea mabao ya klabu yake dhidi ya Everton kwa kuruka na kurusha ngumi hewani na kukimbia sehemu inayotengewa wakufunzi nje ya uwanja.
Mwitaliano huyo huwa ametulia wakati wa mahojiano na wanahabari kabla na baada ya mechi, sifa ambazo anasema huwa anapenda wachezaji wake wawe nazo.

"Lazima tuwe na furaha kwa sababu tulicheza mchezo kwa kutumia vichwa vyetu, na kipindi kama hiki katika msimu, ni muhimu kutumia vichwa vyetu, kisha moyo na baadaye miguu," alisema.
Conte anaamini sana kuhusu hilo, kiasi kwamba aliandika kitabu chenye kichwa Testa, cuore e gambe (Kichwa, moyo na miguu) mwaka 2014.

Mechi za Chelsea zilizosalia 2016-17

#Jumatatu, 8 Mei Middlesbrough (Nyumbani)
#Ijumaa, 12 Mei West Brom (Ugenini)
#Jumatatu, 15 Mei Watford (Nyumbani)
#Jumapili, 21 Mei Sunderland (Nyumbani)
#Jumamosi, 27 Mei Arsenal (fainali Kombe la FA)

lundi 1 mai 2017

Sulley Muntari apewa kadi ya manjano akilalamikia kubaguliwa

Mchezaji wa Pescara Sulley Muntari, aliondoa uwanjani baada ya refa kumpa kadi ya manjano, alipolalamika kuwa alikuwa akidhulumiwa kwa misingi ya rangi wakati wa mechi.

Kiungo huyo wa zamani wa Ghana mwenye umri wa miaka 32, alimuomba refa Daniele Minelli asimamishe mechi hiyo ya Jumapili.

Lakini badala yake refa alimpa kadi ya manjano dakika ya 89, hatua iliyosababisha mchezaji huyo wa zamani ya vilabu vya Portsmouth na Sunderland kupinga kwa kuondoka uwanjani.

Kwa hasira aliwakabili mashabiki wa klabu ya Cagliari akisema kwa sauti. "Hii ni rangu yangu."
Akiongea baada ya mechi Muntari alisema: "Refa hastahili kukaa tu uwanjani na kupiga firimbi, ni lazima afanye kila kitu.
"Ni lazima aone vitu hivi na kuonyesha mfano.
"Nilimuuliza ikiwa alikuwa amesikia matusi. Nikasisitiza kuwa ni lazima asimamishe mechi."

Meneja wa Pescarfa Zdenek Zeman ambaye upande wake ulishindwa kwa bao 1-0, alisema kuwa alimuomba refa kuingilia kati lakini akasema hakuona wala kusikia chochote.

dimanche 30 avril 2017

INTER HAVE FINANCIAL MUSCLE TO SIGN MESSI, CLAIMS MAZZOLA

Inter have financial muscle to sign Messi, claims Mazzola

Inter boast the financial power to sign Lionel Messi from Barcelona, former Nerazzurri star Sandro Mazzola has said.

There has been speculation for some months that the Serie A side, bankrolled by their Suning Holdings Group owners, could try to sign Messi with a stunning transfer bid at the end of the season.

Former Inter president Massimo Moratti said in January the club are planning to sign a global superstar before next season, although he rejected the suggestion that Messi is their top target.

But Mazzola, a double European champion as part of the famous Inter side of the 1960s, believes Suning's backing makes Messi at San Siro a very real prospect.

"Suning have the strength to get those they want, including Messi," he told Il Mattino.

To read full article - https://goo.gl/AY3ByW

Sunderland kupoteza nafasi ya kubaki Premier League

Kipindi cha miaka kumi cha klabu ya Sunderland katika ligi ya Uingereza hatimaye kimekwisha baada ya kushindwa na Bournemouth nyumbani.
Matokeo hayo pamoja na yale ya sare kati ya Hull City na Southampton yanamaanisha timu hiyo ya David Moyes ina pointi 14 ikiwa imesalia mechi nne.

Joshua King wa Bournemouth alifunga bao la pekee ikiwa imesalia dakika 2 na kuipa ushindi timu yake.
Raia huyo wa Norway pia karibu afunge katika dakika ya 20 lakini shambulio lake lilipiga mwamba wa goli na kurudi katika mikono ya kipa Pickford.

Hiyo ni mara ya 23 ya Sunderland kupoteza ,hatua inayomaanisha timu hiyo ya Black Cat imeshushwa dajara kutoka ligi ya Uingereza kwa mara ya nne.

jeudi 20 avril 2017

Uefa Champions League semi-finalists 2017

UCL semi-finalists

Siku ambayo BBC ilikosa habari za kutangaza

Siku hizi ni vigumu sana kutafakari hali ilivyokuwa kabla ya mafanikio makubwa kupatikana katika teknolojia ya mawasiliano.

Imekuwa kama ada kwamba kila wakati lazima kuwe na habari.
Lakini zamani, hali ilikuwa tofauti kabisa.
Miaka 87 iliyopita, mnamo 18 Aprili 1930, msomaji wa habari katika BBC alikosa cha kutangaza.

Taarifa aliyoisoma wakati wa taarifa ya habari ya saa tatu kasorobo usiku ilikuwa: "Hakuna habari".

Baadaye, kinanda kilichezwa kwa dakika 15 zilizosalia ambazo zilikuwa zimetengewa habari.

Baadaye, matangazo yalipelekwa Ukumbi wa Malkia katika jumba la Langham Place, London ambapo kulikuwa na tamasha la muziki wa Wagner.

Miaka 87 baadaye, hali ni tofauti kabisa. Jumanne ilikuwa siku iliyojaa habari tele.
Watu walipokuwa wanashiriki pilkapilka za hapa na pale baada ya Pasaka, Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May aliitisha kikao saa tano mchana na kuahidi kutoa tangazo muhimu.

Wengi walianza kutafakari tangazo lake lingekuwa nini - hadi pale alipotangaza mpango wa kuitisha uchaguzi wa mapema tarehe 8 Juni.

Kulikuwa pia na mzozo kati ya Marekani na Korea Kaskazini ambao umekuwa ukitokota kwa wiki kadha sasa.
Kulikuwa pia na maadhimisho ya uhuru wa Zimbabwe ambapo kiongozi wa muda mrefu wa taifa hilo Robert Mugabe aliwahimiza raia kuutetea na kuulinda uhuru huo.

Nchini Ufaransa, mmoja wa wagombea wakuu katika uchaguzi wa urais Marine le Pen alisema atazuia wahamiaji kuingia nchini humo iwapo atashinda uchaguzi
Siku hizi, BBC ina wafanyakazi wengi na uwezo mkubwa wa kukusanya habari tofauti na hali ilivyokuwa 1930.

Kumekuwa pia na mabadiliko ya maana ya habari.
Wakati huo, habari nyingi zilitoka kwa mashirika ya habari ya kimataifa na matangazo ya serikali.
Siku hizi, watu wa kawaida wanaweza kuwa mada ya habari.

Wakati huo, watangazaji walikuwa pia hawafahamiki na wasikilizaji.
Siku hizi, wengi wa watangazaji wanafahamika sana na hata ni watu mashuhuri.

mercredi 19 avril 2017

UEFA: Real Madrid yailaza Bayern Munich 4-2 Ligi ya Mabingwa Ulaya

Cristiano Ronaldo alifunga mabao matatu na kuwawezesha mabingwa watetezi wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Real Madrid kuwatimua Bayern Munich kutoka kwenye michuano ya msimu huu katika hatua ya robofainali.
Mechi hiyo iliyomalizika 4-2 hata hivyo ilijaa utata na mshindi alipatikana katika muda wa ziada.

Kiungo wa kati wa Bayern Munich Arturo Vidal alitimuliwa uwanjani dakika ya 84 jambo ambalo lilionekana kuathiri mwelekeo wa mechi hiyo.
Ronaldo naye alionekana kuwa alikuwa ameotea alipokuwa anafunga bao la pili la Real muda wa ziada.
Bayern, ambao walihitaji mabao mawili kusonga, alikuwa wameongoza kupitia penalti iliyofungwa na Robert Lewandowski.

Madrid walitatizika kutamba kwenye mechi hiyo iliyochezewa Bernabeu kabla ya Ronaldo kufunga kwa kichwa kutokana na krosi ya Casemiro.
Bayern walijibu sekunde 36 baadaye Sergio Ramos alipojifunga na kulazimisha mechi hiyo kuingia muda wa ziada.
Ni hapo ambapo Ronaldo alifunga bao la utata la Madrid.
Nahodha huyo wa Ureno kisha alifunga la tatu - lake la 100 katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Marco Asensio aliwakamilishia ushindi kwa kuongeza la tatu.

Madrid watamfahamu mpinzani wao nusufainali wakati wa droo Ijumaa.
Majirani wao Madrid Atletico Madrid walisonga kwa kuwaondoa Leicester City.
Kwenye robofainali hizo nyingine, Barcelona wanakutana na Juventus nao Monaco wakutane na Borussia Dortmund baadaye Jumatano.

Mashabiki wamrushia panya mchezaji nchini Denmark

Mechi ya ligi kuu ya Denmark kati ya Brondby na FC Copenhagen ilitibuka baada ya mashabiki kuwarushia panya waliokufa uwanjani.
Mashabiki wa Brondby walimrushia panya mlinzi wa Copenhagen Ludwig Augustinsson alipokwenda kupiga kona.

Copenhagen ilishinda mechi hiyo 1 - 0 na sasa ni wa kwanza huku ikiishindia timu ya pili ambayo ni Brondby kwa alama 13.
"Sio vyema kuwa na baadhi ya wageni ambao hawawezi kuwa na tabia njema," alisema mkurugenzi wa michezo wa Brondby, Troels Bech.

Video iliyorekodi yaliyotokea uwanjani inaonyesha mchezaji wa Slovenia Benjamin Verbic akimsaidia mwenzake Augustinsson kuwatoa angalau panya wawili kutoka uwanja huo wa Brondby ambao unaweza kubeba mashabiki elfu 28.
Brondby ni mabingwa mara 10 wa Denmark na FC Copenhagen inayosimamiwa na aliyekuwa meneja wa Wolverhampton Wanderers Zamani Solbakken, wameweza kunyakua ushindi mara 11

samedi 15 avril 2017

Wema Sepetu, Gabo kuwasha moto kwenye filamu ‘Heaven Sent’

Malkia wa filamu Wema Sepetu pamoja na Gabo Zigamba wataonekana kwenye filamu mpya ‘Heaven Sent’ inayoongozwa na Neema Ndepanya chini ya kampuni ya Fontana Entertainment.

Katika filamu hiyo Wema atakuwa kwenye mahusiano na Gabo Zigamba.
“Sometimes in Life, You meet people for a Reason…. Im so happy I found the Reason I met you Gabo Zigamba #TheMaking of #HeavenSent,” aliandika Wema Instagram akiwa katika maandalizi ya kazi hiyo.

Aliongeza, “Msichana naona mpaka mwaka kuisha watanzania watakuwa wameshaona uwezo wangu wa kubadilika wenye character tofauti. Nashukuru maana mpaka uchizi umenichezesha. Nashkuru sana binti Ndepanyaa.,”

Stori pamoja na script ya filamu hiyo imeandaliwa na Neema Ndepanya.

Hatma ya Arsenal kuhusu Big 4

Arsenal inakabiliwa na changamoto kubwa kufuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya kulingana na mkufunzi wa klabu hiyo Arsene Wenger ambaye ameongezea kuwa hakuna kilichobadilika kuhusu hatama yake ya siku zijazo.
Kushindwa kwao kwa 3-0 na Crystal Palace kuliiwacha klabu hiyo ikiwa katika nafasi ya sita ,na ponti saba nyuma ya klabu ya Manchester City iliopo katika nafasi ya nne huku ikiwa imesalia mechi nane pekee.

Wenger ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu ameiongoza Arsenal katika nafasi nne bora za ligi hiyo katika miaka 20 aliyokuwa mkufunzi wake.
Kuhusu timu nne bora, alisema: ''Tunaweza kuwa katika timu nne bora au la''.

Raia huyo wa Ufaransa amepewa ombi la kandarasi ya miaka miwili ijapokuwa hajatangaza iwapo ataendelea au la.
Kushindwa kwao kwa mechi tano kati ya 10 katika mechi za ligi kuu kumewafanya mashabiki wa Arsenal kumtaka Wenger kuondoka katika klabu hiyo.
Alipoulizwa kuhusu hatma yake ya baadaye alisema: kile kitakachoamuliwa na bodi hakinihusu mimi.
''Ninafanya kile nilichoajiriwa kufanya, mchezo mzuri wa timu na kile mashabiki wanachotaka ambacho ni timu iweze kucheza vyema''.

The Gunners watacheza dhidi ya Middlesborough siku ya Jumatatu.
Wenger amekataa kujibu madai kwamba mshambuliaji Alexis Sanchez amepewa kandarasi mpya ya £300,000 kwa wiki.

vendredi 24 mars 2017

Arsenal imesitisha mazungumzo na Sanchez na Ozil

Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema klabu hiyo imesitisha kwa muda mazungumzo kuhusu mikataba ya Alexis Sanchez na Mesut Ozil hadi mwisho wa msimu.

Sanchez na Ozil mikataba yao katika klabu ya Arsenal inamalizika mwezi juni mwakani na wamekuwa wakisusua kusaini mikataba mipya ya kuendelea kuitumika timu hiyo.
Mfaransa huyo amesema hayo wakati akihojiwa na kituo cha BeiN Sports huku akikataa kuweka wazi mustabali wake klabuni hapo.
Arsenal wameshuka hadi nambari sita Ligi ya Premia baada ya kushindwa mechi nne kati ya tano walizocheza karibuni zaidi.
Kuhusu mustakabali wake, Wenger alisema: “Bila kujali nitasalia katika klabu hii muda gani bado nitabaki kujitolea na kuangazia kabisa (majukumu yangu) muda wote nitakaokuwa katika klabu hii.”
Gunners watarejea uwanjani Ligi ya Premia Jumapili tarehe 2 Aprili watakapokuwa wenyeji wa Manchester City.

Buffon kutengeneza rekodi nyingine timu ya taifa leo

Kipa wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Italia, Gianluigi Buffon akizungumza na waandishi wa habari jana kuelekea mchezo wake 1,000 wakati timu yake ya taifa, Italia itakapoikaribisha Albania leo mjini Palermo katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia.
Amesema “Najiona ni mwenye furaha sana kufukisha mechi 1000 kwa taifa langu”, alisema Buffon ambaye alionekana kuwa ni mwenye furaha.

Buffon alicheza mechi yake ya kwanza Parma akiwa ana umri wa miaka 17 mwaka 1995, kabla ya kuhamia Juventus mwaka 2001 na kipa huyo ameichezea Italia kwa miaka zaidi ya 19 tangu Oktoba 29, mwaka 1997 akiwa ana umri wa miaka 19.

Harusi by The Light of Peace ( Nuuru Salaam ) official video



Abuchief.Com

mardi 14 février 2017

Diamond Platnumz athibitisha kuwa mbioni kumrudisha Q-Chief kwenye ramani

Diamond Platnumz amethibitisha kuwa amejipanga kumrudisha Q-Chief kwenye ramani ya muziki baada ya uongozi wake wa QS Mhonda kushindwa kufanya hivyo licha ya kudai kutumia zaidi ya shilingi milioni 200 bila kupata faida.
 Kwa muda kulikuwepo na tetesi kuwa Diamond ana mpango wa kumsainisha msanii huyo mkongwe kwenye label ya WCB. Na sasa, ingawa hajasema kuwa amepanga kumsanisha kwenye label hiyo, Diamond amekiri kuwa kwenye mipango ya kufanya kazi na legend huyo.
 

“Unajua lengo langu kama mimi au sisi vijana wa sasa hivi tunajaribu kuona tunavyoweza kufanya kazi kwa ushirikiano, so tuko na maongezi na bro tunaangalia tunawezaje kufanya kazi kwasababu ni mtu ambaye kwanza mimi namfeel halafu ambaye namuamini,” Diamond ameiambia Dizzim Online.

“Ni mtu ambaye najua kabisa yaani akibonyeza button hii basi huu mji mzima umechafuka. Kwahiyo siwezi kuyaongea mengi sema Watanzania watuombee dua tunachokiplan kifanyike vizuri,” ameongeza staa huyo.
Naye Q-Chief alisema, “mimi nahisi project inayofuata Simba anahusika kwasababu ni mtu ambaye ameniita kwa ushauri nikiwa na QS, amemuambia vitu vingi vya msingi, yeye shahidi hapa, lakini kama ni mtu anayeelewa mdogo wake ameniita amesema nini mpaka mimi nimeelewa na hajafanya maybe [QS] is not ready to do business but Diamond is a business man and I am ready to join a business man so long as kuna misingi. Lakini naamini ngoma inayofuata Diamond amenipa baraka zake.”

Hivi karibuni muimbaji huyo ambaye jina lake kamili ni Abubakar Katwila amekuwa kwenye vita vya maneno na kampuni inayomsimamia ya QS Mhonda anayoishutumu kwa kushindwa kumfikisha popote licha ya uwekezaji mkubwa ilioufanya kwake.

Ndugu zake pia walihoji kuhusu mkataba wa maisha aliosainishwa mtoto wao kwenye kampuni hiyo na kwamba tangu awe chini ya kampuni hiyo hawajaona mabadiliko ya maana kwenye maisha yake.

Nai (Model wa video ya Darassa): Mimi si msichana rahisi rahisi kwa wanaume

Rayvanny amtaja msanii wake mmoja wa TZ ambaye anatamani kufanya naye kolabo

Msanii wa muziki kutoka WCB, Rayvanny amedai msanii wa kundi la Weusi Joh Makini ndiye msanii ambaye anatamani kufanya naye kolabo.
 

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Rayvanny amedai bado hajazungumza na rapper huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Waya’.

“Bongo kuna wasanii wengi ambao ningependa kufanya nao kolabo lakini ukisema nimseme mmoja ambaye nawish ningefanya naye kitu ni Joh Makini,” alisema Rayvanny. “Joh namkubali sana na naona kama kuna kitu fulani chaajabu kitatokea nikifanya naye kolabo,”

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na kolabo ya wimbo ‘Kijuso’ aliyoshirikishwa na Queen Darleen, amedai bado hajafanya mazungumzo na Joh Makini kuhusu kolabo hiyo.
“Bado sijamwambia Joh Makini, lakini nadhani ukifika muda kila kitu kitafanyika. Kila kitu kitajulikana hapo lakini kama nikikutana naye nataka kufanya kitu tofauti sana,” alisema Rayvanny.

vendredi 3 février 2017

Michuano ya ligi kuu Uingereza wikendi hii

Chelsea wako kifua mbele katika ligi na alama 9 na wanaweza kujiimarisha kileleni wakati wakiipokea Arsenal ilio nafasi ya tatu.

Mechi hii kwa Chelsea ni fursa kujivua aibu baada ya kulambishwa sakafu na arsenal bao tatu kwa bila katika mechi ya awali.

Na baada ya hapo ndio ulikuwa mwanzo mzuri wa Chelsea kufululiza na matokeo mazuri .
Arsenal ambao jumanne walipokea kichapao cha Watford , wana wasiwasi mkubwa hasa baada ya kiungo wake Aron Ramsey kuumia mguu.

Pia watakosa huduma za Granit Xaka anayetumikia adhabu huku Mohamed Elneny akiwa michezo ya fainali za kombe la Afrika na timu yake ya Misr.

Ushindani pia ni kati ya washambuliaji wawili Diego Costa wa Chelsea na Alexis Sanchez ambao wanaongoza kama wafungaji bora na mabao 15.

Katika mechi nyingine hapo kesho Tottenham ilio nafasi ya pili wanaipokea Middlesbourg.

Nayo Liverpool itasaka ushindi wake wa kwanza mwaka huu wakiwa ni wageni wa Hull City .

Jumapili, Manchester City wanachuana na Swansea City huku Leicester City wakiikaribisha Man U

Nyumba ya Nicki Minaj yaporwa Marekani

Polisi kwenye jimbo la Los Angeles nchini Marekani wanachunguza wizi uliofanyika kwenye nyumba ya Nicki Minaj amabapo malia ya thamani ya dokl 175,000 iliibiwa.


Wizi huo ulitokea kwenye nyumba yake ya kifahari eneo la Beverly Hills lakini mwanamuziki huyo hakuwa nyumbani wakati huo.

Inaripotiwa kuwa nyumba hiyo ilivunjwa wakati wa uvamizi huo na baadhi ya nguo za Nicki Minaj kuibiwa.
Fanicha iliharibiwa huku picha na chupa za manukato zilivunjwa.
Bado haijulikani ni vipi waalifu waliingia nyumbani humo.

Waliiba vito vya thamani na bidhaa zingine zenye gharama ya dola 175,000.


Haya ndio maamuzi ya Frank Lampard kuhusu soka

Mchezaji wa zamani wa vilabu vya West Ham, Manchester City, Chelsea, New York City na timu ya taifa ya Uingereza Frank Lampard ambaye anamiaka 38, ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka na kusalia kuwa mtazamaji na kuchukua mafunzo ya Ukocha.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lampard ametoa uamuzi huo kwa kuandika ujumbe huu.

Frank Lampard ameshinda mataji matatu ya EPL, Makombe manne ya FA, vikombe viwili vya kombe la Ligi, Taji moja la Klabu Bingwa Ulaya na Europa, na kumfanya atimize michezo 1039 na Magoli 302 kwa miaka 21 aliyoitumikia kama mchezaji kwenye vilabu mbalimbali na timu yake ya taifa.

samedi 28 janvier 2017

Video ya ‘Hela’ ya Madee yatoweka YouTube

Nini kimeikuta video ya wimbo wa ‘Hela’ ya Madee?
Video hiyo ambayo imetoka wiki iliyopita kwenye mtandao wa YouTube na kuanza kufanya vizuri kwenye vyombo mbalimbali vya habari kwa sasa imeonekana kufutika katika mtandao huo kwa mujibu wa meneja wa Tip Top Connection, Babu Tale.


Kupitia katika mtandao wa Instagra, Tale ameandika ujumbe kwa mashabiki unaosomeka, “Hii hatari sijui nini kimetokea mzigo umefutika kabisaa YouTube ila tuna pambana kuurudisha wadau mtuwie radhi tuta wapa taarifa kitakachojiri. @madeeali.”

Video hiyo ilifanikiwa hadi kushika namba moja ya video zilizo trend katika mtandao wa YouTube.

mardi 24 janvier 2017

Huyu ndie mwamuzi atakae chezesha mechi ya Liverpool dhidi ya Chelsea

Mwamuzi Mark Clattenburg ameteuliwa kuchezesha mechi ya Chelsea dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield wiki ijayo.
Chelsea watasafiri hadi Anfield wiki ijayo siku ya Jumanne (Januari 31) wakiwa na pointi 10 dhidi ya timu ya Jurgen Klopp.

Clattenburg ana historia kadhaa anapo chezesha mechi za Chelsea, mechi ya mwisho msimu uliopita katika uwanja wa Stamford Bridge dhidi ya Tottenham Hotspur ikizua utata.

Kadi kumi na mbili za njano zilitolewa katika pambano hilo, na vitendo vya vurugu baina ya wachezaji katika sare ya 2-2.
Chelsea na Tottenham zilitozwa faini ya paundi 375,000 na 225,000 mwenyeji kuhusika katika kile kilichotokea, lakini Clattenburg hakuweza kutoa kadi nyekundu katika mechi hiyo.

Hii itakuwa mara ya pili kwa mwamuzi huyo kutoka County Durham kuchezesha mechi ya Chelsea msimu huu, baada ya kuchezesha Blues wakishinda 3-0 dhidi ya Burnley mwezi Agosti.

Mimi siwezi kuoa kwa sababu fulani kaoa – Chege

Msanii mkongwe wa muziki Chege Chigunda amedai hawezi kufuata mkumbo kuoa kwa sababu fulani kaoa.
Muimbaji huyo ambaye hivi karibuni ameachia wimbo mpya “Kelele za Chura” akiwa amemshirikisha Nandy, amedai suala la kuana linakuja kutoka kwa Mungu na sio kuigana.


“Mimi siwezi kuoa sijui kwa sababu nikienda kwenye interview nitaulizwa, mbona wewe haujaoa, mbona mwenzako kaoa, na siwezi kuoa kwa sababu Mh Temba kaoa,” Chege aliiambia Global TV. “Mimi nitaoa pindi tu mwenyezi Mungu atakaposema Chege oa lakini sio kwa sababu fulani kafanya hivyo,”
Muimbaji huyo ni msanii pekee wa Kundi la TMK Wanaume Halisi ambaye bado anafanya vizuri katika muziki.

Nimeanza kuupenda muonekano wangu, sitaki tena kuuharibu kwa sumu – Ray C

Msanii mkongwe wa muziki Ray C amedai ameupenda muonekano wake mpya huku akijipa mtihani wa kujizua kurudi katika mambo ambayo yalimpelekea kuupoteza muonekano wake mzuri wa mwili.

Ray C ndani ya muonekano mpya
Muimbaji huyo hivi karibuni amekuwa akipost picha zake mpya ambazo zinamuonyesha akiwa na muonekano mzuri hali ambayo imewafanya mashabiki wake katika mitandao ya kijamii kuona kweli mrembo huyo ana nia ya kubalika na kutoka katika matumizi ya Madawa ya kulevya.
Jumanne hii muimbaji huyo amepost picha yake katika mtandao na kuandika: Nimeanza kumpenda Huyu dada Ray C sitaki kumdhuru tena kwa sumu wala bunduki nataka Azidi kunivutia kila nimuonapo kiooni.

Kwa sasa muimbaji huyo anarekodi nyimbo zake katika studio ya Wanene Entertainment kufanya maandalizi ya ujio wake mpya

jeudi 19 janvier 2017

Rais Bush na mkewe walazwa hospitalini


Rais mstaafu wa Marekani George HW Bush aliyekuwa amelazwa hospitalini huko mjini Texas tangu Jumamosi, amepelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Baada ya kutibiwa ugonjwa wa homa ya mapafu, Bush mwenye umri wa miaka 92 sasa anaendelea vizuri.
Mke wake Barbara, amelazwa katiaka hospitali hiyo hiyo kama tahadhari kwa sababu ya uchovu.

Kiungo wa zamani wa Misri Aboutrika atajwa kwenye listi ya magaidi wa nchini hiyo

Mamlaka za usalama za Egypt zimemweka mchezaji wa zamani wa soka wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Mohamed Aboutrika katika ya magaidi baada ya kuhusishwa na kikundi cha waislam wa Brotherhood, amesema mwanasheria wa mchezaji huyo.


Mr Aboutrika anashutumiwa kuwasaidia kifedha kikundi cha Brotherhood, kikundi ambacho mamlaka za Misri kimewaeka kwenye kundi la magaidi.
Mnamo mwaka 2012, alimpigia kampeni ya urais Mohamed Morsi, ambaye ni mwanachama wa Brotherhood.
Jambo hilo lilipelekea kuwagawa mashabiki wa mchezaji bora wa mwaka wa BBC wa mwaka 2008.
Kwa sheria za Misri, mtu yoyote anayewekwa kwenye listi ya ugaidi, hufungiwa kusafiri na passport yake pamoja na mali zake hushikiliwa.
Mwanasheria wa Aboutrika, Mohamed Osman, alisema mteja wake hajatiwa hatiani wala hajapewa taarifa rasmi juu ya mashtaka wanayomtuhumi nayo. Pia ameahidi kukata rufaa juu ya tuhuma hizo kwa mteja wake.
Kiungo huyo wa zamani wa Al-Ahly na timu ya taifa ya Misri, alikuwa kipenzi cha wananchi wa Misri na walifikia hatua ya kumpa majina ya The Prince of Hearts, The Magician na The Saint wakati akicheza soka, lakini uamuzi wake wa kumsapoti Mohammed Morsi, ambaye alikaa madarakani kwa mwaka mmoja tu, uliwagawa mashabiki zake.
Mwaka 2015, mali zake nyingi ziliwekwa kizuiani, hisa zake kwenye makampuni tofauti zilishikiliwa na mamlaka za usalama za nchi hiyo.

FIFA kufanya mapinduzi ya soka, waweka wazi mpango wa kufuta offside na kubadili upigaji wa penati

Raisi mpya wa FIFA Gianni Infantino anaonekana kutaka kubadili soka kabisa.Infantino anaonekana kuondoa kila kitu cha Sepp Blatter na kuleta vyake.Baada ya kuongeza timu zitakazoshiriki kombe la dunia 2026 kufikia timu 48 sasa Infantino amekuja na mpya.Kwa kumtumia mkurugenzi wa mambo ya ufundi wa FIFA Marco Van Basten amependekeza baadhi ya sheria mpya katika soka.


Akihojiwa na gazeti la Ujerumani liitwalo Bild,Van Basten amesema wanawaza kuondoa mchezo wa kuzidi katika soka.
“sipati picha soka isipokuwa na ofside,washambuliaji watapata nafasi nyingi sana za kufunga”.Van Basten alisema mpira wa miguu utakuwa wakuvutia sana kama offside itaondolewa na anaamini jambo hilo litawafurahisha mashabiko na washambuliaji.
Kubadili upigaji wa penati.Van Basten pia anaona kuna haja kubwa kwa FIFA kubadili aina ya upigaji wa penati.Kwa sasa adhabu ya penati mchezaji anauweka mpira mita kadhaa karibu na goli ma kuupiga.Lakini Van Basten anaona penati ibadilishwe.Anataka mpiga penati auweke mpira mita 25 kabla ya goli na kama anaweza atembee nao kuelekea golini kwa muda usiozidi sekunde nane.Aina hii ya upigaji penati sio ngeni kwani mwaka 1999 ilishafanyiwa majaribio nchini Marekani.
Kupunguza adhabu mipira ya kushika.Van Basten anaona kama adhabu ya kadi nyekundu ni kali mno kwa tukio hilo.Na analiona kama tukio dogo lisilohitaji kadi nyekundu na anazani inapaswa ipunguzwe adhabu hiyo.Kusitolewe kadi nyekundu mpira ukishikwa.Adhabu kam ile ya tukio la Luis Suarez mwaka 2010 wakicheza dhidi ya Ghana aliposhika mpira wakati ukiingia golini Van Basten anataka kadi iwe ya njano.
Kapteni awe mtu pekee kuongea na mwamuzi.Kama katika Rugby ni kapteni tu anayeongea na mwamuzi,asiruhusiwe mtu yeyote,mchezaji yeyote kuongea na mwamuzi.
Style ya faulu ya mchezo wa kikapu.Katika mchezo wa kikapu pale mchezaji anapocheza faulu tano anatakiwa atoke uwanjani.Na sasa Van Basten anaamini staili hiyo inapaswa kuletwa katika soka.
Kupunguza idadi ya mechi.Hii itafurahiwa sana na makocha wageni Uingereza.Alianza Van Gaal akaja Jurgen Klopp walilalamikia idadi ya mechi kuwa nyingi Epl.Van Basten anataka idadi ya mechi zipunguzwe kutoka mechi 80 kwa msimu hadi 50 kwa msimu.
Kuongeza idadi ya Substitution.Van Basten anatamani kuongeza idadi ya wachezaji wa sub kuanzia 5-7,kwa muda mrefu wadau wa soka wamekuwa wakizungumzia kuhusu suala la kuongeza wachezaji wa akiba na sasa FIFA inatarajia kuliangalia suala hili.
Kuzifanya dakika 10 za mwisho kutumika ipasavyo.”Tunajua kutokana na kuongeza idadi ya wachezaji wa akiba pamoja na aina ya upigaji penati vitachukua mda mrefu uwanjani na itatubidi kuhakikisha dakika 10 za mwisho zinatumika kiuhakika” Van Basten alisema watahakikisha hakuna upotezaji muda katika dakika zamwisho za mchezo.
Hayo ni mapendekezo tu kutoka kwa mkurugenzi wa ufundi wa FIFA, na sasa atawasilisha mapendekezo hayo katika kamati ya FIFA yaweze kujadiliwa.

Shukran by The Light of Peace (Nuuru Salaam)

Twamtukuza Rabaana


New Kaswida Colaboration of Group
 The Light of Peace (Nuuru Salaam), Madrasatul Firdaus & Wana Karori

samedi 14 janvier 2017

Harusi za kifahari zapigwa marufuku Somalia


Mji mmoja nchini Somalia umepiga marufuku harusi za gharama ya juu ili kuwashinikiza vijana zaidi kuoa.

Kamishna wa wilaya Mohamud Hayd Osman wa Bula Hawa karibu na mpaka wa Kenya waliambia BBC kwamba ni mbuzi wasiozidi watatu ndio wanaofaa kuchinjwa pekee ili kuwalisha wageni na kwamba sherehe katika hoteli hazitaruhusiwa.
Amesema kuwa mahari itakuwa chini ya dola 150 pekee.
Uamuzi huo unajiri baada ya maafisa kubaini kwamba takriban watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa hivi karibuni.

Kamishna huyo ameongezea kwamba gharama ya harusi, ukosefu wa ajira na kiangazi ndio maswala yanayowafanya watu kulihama eneo hilo.
Waandishi wanasema sio kawaida kwa familia ya bwana harusi kutumia takriban dola 5000 katika harusi nchini Somalia.

"Mafunzo ya kiislamu yanasema kuwa ndoa inafaa kuwa ya gharama ya chini, alisema Osman.
Hatua ya kupunguza matumizi kuhusu sherehe za kifahari pamoja na matumizi mengine baada ya ya maafisa kugundua kwamba ni kwa nini watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa mjini humo.
Wasichana walikuwa wanakataa kuolewa hadi pale kitita cha pesa kitakapotumika kwa dhahabu pamoja na fanicha, alisema.

AFCON: Matukio sita makuu historia ya Kombe la Mataifa Afrika

Michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, makala ya 31, itang'oa nanga Jumamosi 14 Januari pale wenyeji watakapokabiliana na Guinea-Bissau ambao wanashiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza.
Kwa baadhi ya mashabiki, hii ni michuano tu ya kawaida ya soka.

Lakini AFCON kwa sasa ni michuano yenye ushindani mkali na yenye wachezaji nyota kama vile Riyad Mahrez, Sadio Mane na Pierre-Emerick Aubameyang.

Michuano hii inapong'oa nanga, tunaangalia matukio muhimu ya furaha na ya kusikitisha pia ambayo hayasahauliki katika historia ya AFCON.

1994: Zambia yajikwamua baada ya mauti

 Mnamo 27 Aprili 1993, timu ya taifa ya Zambia ilikuwa safarini mechi ya kufuzu Kombe la Dunia nchini Senegal ndege iliyowabeba ilipoanguka na kutumbukia baharini mita 500 kutoka mji wa Libreville, Gabon.
Abiria wote 25 waliangamia pamoja na wahudumu watano.
Mwaka mmoja baadaye, Zambia ilijijenga na kufana sana michuano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika 1994. Walifika fainali ingawa walishindwa na Nigeria 2-1.

2012: Herve Renard asaidia Zambia kutwaa kombe


Herve Renard and Zambia win the Africa Cup of Nations in 2012Getty Images
Zambia walikosa ushindi fainali 1994 lakini walifanikiwa 2012 chini ya kocha wao Mfaransa Herve Renard ambapo walikabiliana na Ivory Coast fainali.
Kwenye mechi hiyo, kulipigwa mikwaju 18 ya penalti, na Zambia wakashinda 8-7.

2015: Morocco yajiondoa kwa sababu ya Ebola

 

 

Kutokana na kuenea kwa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi, wenyeji waliopangiwa kuandaa michuano ya 2015 Morocco walijiondoa wakihofia michuano hiyo ingefikisha ugonjwa huo nchini mwao.

CAF ilikataa ombi la kujiondoa, na baada ya Morocco kusisitiza timu yake ikafurushwa kutoka kwa michuano hiyo.
Mataifa matano yalikataa kuwa mwenyeji kabla ya Equatorial Guinea kukubali. Ivory Coast waliibuka washindi kwa kulaza Ghana 9-8 kupitia mikwaju ya penalti.

2010: Basi la Togo lashambuliwa

Basi la timu ya Togo lilishambuliwa na watu wenye silaha timu hiyo ilipokuwa ikirejea kambini Angola.
Kundi moja la waasi kutoka eneo la Cabinda lilikiri kuhusika

Watu watatu waliuawa na wengine tisa kujeruhiwa. Nyota wa zamani wa Arsenal na Manchester City Emmanuel Adebayor ni miongoni mwa waliokuwa kwenye basi hilo.
Togo ilijiondoa kutoka kwa michuano hiyo.

2006 & 2012: Drogba ashindia amani Ivory Coast

Mshambuliaji wa Ivory Coast Didier Drogba alikuwa stadi sana uwanjani kwa taifa na Chelsea na pia alitumia hadhi yake kufanikisha amani nchini mwake.
Wakati wa vita kati ya 2002 na 2007, alipiga magoti moja kwa moja kwenye runinga akiwa na wachezaji wenzake 20045 kuwahimiza waliokuwa wanapigana kuweka chini silaha.

Kipindi cha amani kilifuata. Mwaka 2008, alisisitiza mechi ya kufuzu Kombe la Taifa Bingwa Afrika dhidi ya Madagascar ichezewe ngome ya zamani ya waasi Bouake kama wito kwa raia kuungana.
Mwaka 2006 na 2012, Drogba alisaidia taifa lake kufika fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika lakini wakashindwa kwa mikwaju ya penalti.
Hata hivyo, hakufanikiwa kushinda.

2002 & 2004: Jezi za Cameroon

Cameroon walishinda michuano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika 2002 kwa kulaza Senegal kupitia mikwaju ya penalti kwenye fainali.

Lakini kinachokumbukwa sana ni jezi za Simba Wasioshindwa ambazo zilikuwa hazina mikono.
Fifa hata hivyo waliwazuia kuzivalia wakati wa Kombe la Dunia 2002.
Mwaka 2004 walikuwa na jipya tena. Walivalia jezi moja iliyoshikana - fulana na kaptura nchini Tunisia.
Fifa hawakufurahia, na ikizingatiwa kwamba walikiuka ahadi ya awali ya kuzitumia kucheza mechi za makundi pekee,
Fifa waliwapiga faini kwa kucheza mechi ya robofainali ambayo walishindwa na Nigeria.