Google tag

jeudi 31 mars 2022

L'Algérie va demander à rejouer contre le Cameroun : l'arbitre du match serait accusé de corruption

Le Cameroun a assuré sa place à la Coupe du monde au Qatar en dominant l’Algérie tout au bout des prolongations, lors du barrage retour, mardi 29 mars 2022 soir à Blida. Un résultat contesté par l'Algérie qui ne compte pas en resté là selon LSI Africa. Bakary Gassama aurait reçu de l'argent pour siffler en faveur du Cameroun.

L’Algérie pensait avoir fait le plus dur en s’imposant à Douala à l’aller (0-1). Mais c’est bien le Cameroun qui disputera sa huitième Coupe du monde (record pour un pays africain) à l’issue d’un match renversant, mardi soir à Blida (1-2, a. p.). Le Lyonnais Karl Toko-Ekambi a envoyé les Lions Indomptables au Qatar tout au bout des arrêts de jeu des prolongations (120e+4). Menés dès la 22e sur un but d’Eric Choupo-Moting, les Fennecs n’auront tenu leur billet pour le Mondial que six minutes, après l’égalisation d’Ahmed Touba (118e).

Après ce match, les Algériens qui n'ont pas manqué de crier à l'injustice demanderont officiellement que ce match soit rejoué à en croire une information exclusive de LSI Africa, sur sa page Facebook, ce mercredi 30 mars 2022. Pour cause, l'arbitre du match, Bakary Gassama, “aurait reçu 40.000 euros" pour siffler en faveur des Lions Indomptables du Cameroun. Ainsi, la Fédération Algérienne de football tiendra ce jeudi matin, une assemblée générale extraordinaire au cours de laquelle d’importantes décisions seront prises, nous fait également savoir le media d'information panafricaine . Cette initiative, si elle est avérée, aura-t-elle des chances d'aboutir ?




Makundi yatavyokuwa World Cup 2022

Makundi ya Fainali zijazo za kombe la Dunia yanapangwa kesho Ijumaa.


Huu ndiyo mgawanyo wa timu kulingana na Ubora
Timu zilizo katika POT Moja haziwezi kupangwa katika kundi moja


Hivi ndivyo Pots zitakavokuwa kwenye Draw ya World Cup kesho ijumaa. ⏳




mercredi 30 mars 2022

Chama cha Soccer Misri cha laani vikali walicho fanyiwa wachezaji wake

Chama cha soka nchini Misri kitawasilisha malalamiko yake kwa FIFA kulalamikia vitendo vya mashabiki wa Senegal kuwasumbua kwa tochi zenye mwanga mkali wachezaji wake wakati wa mchezo wa marudiano kufuzu kombe la Dunia


FA ya Misri inadai vitendo hivyo vimechangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kupoteza kwa mikwaju ya penati katika mchezo huo


Kuna matumaini huenda Senegal ikaadhibiwa kwa kutozwa faini kwa vitendo hivyo vya mashabiki wake

dimanche 27 mars 2022

Masta ya AY nooma saaana

AY AACHIA MASTA “HUWA NATABASAMU NIKITAZAMA ZILE TUZO ZA MTV, WALINIWEKA KUNDI MOJA KANYE NA JAY Z”


Hayo ni mashairi ya ngoma mpya ya mkongwe kwenye game @aytanzania wimbo unaitwa Masta.

Rapa huyo wa kiwango cha hali ya juu ameachia video ya wimbo huo akiwa na @sir_nature huku ndani yake ukiwa na madini mengi.


AY kwenye Masta ametaka kuonyesha miaka yake 22 kwenye game ya muziki ikiwa ni safari yenye mafanikio mengi katika muziki wa Tanzania.

Katika video zimeonekana video za nyimbo zake za zamani pamoja na matukio makubwa yakikamii aliyoyafanya.

Juma Nature

Katika ngoma hii mkongwe @sir_nature amepita na chorus katika viwango vyake vilivyowahi kupendwa zaidi. Mastaa wengine walionekana kwenye video ni @johmakinitz , @naytrueboytz , @mhtemba na mengine.

Una mtazamo gani juu ya project hii mpya ya Ay ndani ya mwaka 2022?

Video hiyo unapatikana YouTube kupitia link iliyopo kwenye bio yake.

samedi 26 mars 2022

Huenda Lionel Messi akastaafu soka la Kimataifa

Huenda Lionel Messi akastaafu soka la Kimataifa baada ya Kombe la Dunia baadae mwaka huu na huenda mchezo wa usiku wa kuamkia leo wa Argentina dhidi ya Venezuela ukawa ndio mechi yake ya mwisho katika ardhi ya nyumbani.


Argentina iliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Venezuela huku Messi akiwa mmoja wa wafungaji.

Mess katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi alisema huenda mechi hiyo ikawa ndio mechi yake ya mwisho katika ardhi ya nyumbani kwa sababu baada ya World Cup hajui nini kitafuata ila atakuwa na nafasi ya kufilikilia zaidi.

Baba mzazi wa Diego someone afariki duniya

Carlos Simeone, baba mzazi wa kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone amefariki Dunia siku ya Ijumaa Machi 25.


Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Klabu hiyo Mzee Carlos Simeone (80) ambaye pia alikuwa babu wa mshambuliaji wa Atletico Madrid B Giuliano amefariki jana Ijumaa katika Jiji la Buenos Aires nchini Argentina.


Katika kumkumbuka Bendera katika uwanja wa Wanda Metropolitano itapepea nusu mlingoti.


Klabu mbalimbali na wachezaji wametuma salamu zao za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii.


lundi 14 mars 2022

BERKANE WAMSHTAKI REFA WA MECHI YAO DHIDI YA SIMBA CAF


Klabu ya RS Berkane ya Morocco imewasilisha malalamiko kwa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuhusu mwamuzi wa DR Congo, Jacques Ndala Chuma alicheyechezesha mchezo dhidi ya Simba SC na kutaka afungiwe.


Berkane wanadai Ndala alihongwa ndio maana aliwanyima penati kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Pia wanasema walipata bao la wazi lakini walinyimwa kwa sababu mchezaji wao alikuwa tayari ameshaotea (offside). 

Wamorocco hao walisema, Simba ilipoteza muda mwingi na mwamuzi wa akiba akaongeza dakika nne tu za kuchezwa.

Klabu hiyo inaitaka CAF kumuadhibu mwamuzi na wasaidizi wake wote kwa kufungiwa ikiwezekana kwa kushindwa kutenda haki katika mchezo huo uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

vendredi 11 mars 2022

Neymar na Donaruma za waka moto

Wachezaji wa PSG ya Ufaransa Neymar na Gianluigi Donnarumma inaelezwa kuwa walizozana vikali hadi kupelekea kupigana kwenye vyomba vya kubadilishia nguo na hii yote ni baada ya PSG kushindwa kushinda mbele ya Real Madrid katika mchezo wa pili wa michuano ya Ligi ya Mabingwa ULAYA UEFA.


Kwa mujibu wa gazeti la Marca, mzozo huo ulianza uwanjani pale mshambuliaji huyo wa Brazil alipomtuhumu mlinda mlango huyo wa Italia kuwa alifanya kosa la kipuuzi lililopelekea bao la kusawazisha la Real Madrid dhidi ya Paris.

Tayari baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, ilipobainika kuwa wababe hao wa Ufaransa wametolewa kwenye mashindano, mapigano kati ya wachezaji wa timu yaliendelea kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

Neymar inaelezwa alimlauma Donnarumma kuwa alifanya kosa la kipuuzi huku mlinda mlango huyo naye akimtuhumu Neymar kufanya kosa la kipuuzi pia baada ya kupoteza mpira mbele ya modric na kushindwa kumpokonya hadi kupelekea goli la pili kufungwa na Benzema.

PSG wametupwa nje ya michuano ya UEFA baada ya kupokea kichapo cha goli 3-1 katika dimba la Bernabu na kufanya jumla ya magoli 3-2 baada ya mchezo wa kwanza Real Madrid kupoteza goli 1-0 dhidi ya PSG. magoli yote ya PSG yakifungwa na Benzema huku magoli ya PSG yakifungwa na Mbappe.

Timu ambazo tayari zimetinga robo fainali ya UEFA ni Liverpool, Bayern Munich, Manchester City, na Real Madrid bado michezo minne ambayo ni Manchester United vs Atletico Madrid, Chelsea vs Lille, Ajax vs Benifica na Juventus vs Villareal.

Fainali za UEFA mwaka huu zitafanyika katika uwanja wa Stade de France ulipo jijini Paris ambao ni uwanja wa taifa la Ufaransa mnamo tarehe 28 mwezi wa tano na hii yote ni baada ya uwanja kubadilishwa kutoka St, Petersburg Urusi kutokana na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine.

mercredi 9 mars 2022

Vita ya Urusi na FIFA huko CAS

Wakati vita vya Kisiasa vikiendelea kati ya Urusi na Ukraine, Urusi imeibua vita vingine vya kisheria dhidi ya FIFA na UEFA.


Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imepokea rufaa ya Urusi kuhusu FIFA na UEFA kuzifungia vilabu vyake na timu zake za taifa kucheza.


Rufaa hiyo pia inaomba timu za Urusi zirejeshwe kwenye mashindano husika.


(Source : Sky Sports)

mardi 8 mars 2022

Msuluhishi wa Ukraine auwawa

Msuluhishi wa Ukraine kwenye mzozo wa kivita dhidi ya Urusi, ameuawa baada ya maafisa usalama wa Ukraine kugundua kuwa alikuwa ni jasusi aliyetumika kupeleleza pande zote mbili.


Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Denis Kireev amesema oparesheni hiyo ya kumuua mpelelezi huyo imetekelezwa na kitengo cha Usalama wa Taifa cha Ukraine baada ya kukataa kujisalimisha.

Urusi na Ukraine wametoa shutuma kuwa alikuwa mpelelezi aliyetumika kwa mataifa yote mawili.

Gazeti la Urusi, Pravda limeripoti kuwa Usalama wa Taifa wa Ukraine ulipata ushahidi wa mawasiliano ya jamaa huyo ambayo yaliashiria kuwa anatumika na pande zote mbili.
Kachero huyo alikuwa sehemu ya timu inayoshugulika kupatikana kwa suluhu kati ya Ukraine na Urusi.

lundi 7 mars 2022

UKRAINE: STAA WA FILAMU PASHA AFARIKI DUNIA KWA KOMBORA LA RUSSIA


Msanii mashuhuri wa filamu nchini Ukraine, Pasha Lee aliyeamua kuweka sanaa pembeni na kuingia vitani kuipigania nchi yake, ameuawa baada ya kupigwa na makombora ya Urusi katika Mji wa Irpin ambako mashambulizi makali yanaendelea.


Pasha aliyefariki akiwa na umri wa miaka 33, alipata umaarufu mkubwa kutokana na kazi yake ya uigizaji na utangazaji ambapo filamu za Lion King na Hobbit, zilimfanya apate umaarufu ndani na nje ya nchi hiyo.


Siku tano kabla ya mauti yake, staa huyo ambaye ni mzaliwa wa Crimea, aliposti picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa amevaa mavazi ya kijeshi na kusindikiza na maneno ya 'LET'S UNITE' akiwataka wananchi wa Ukraine kuungana kupambana na uvamizi wa Urusi.


dimanche 6 mars 2022

Vladmir Putin: Africa haitokuwa huru kamwe

"Afrika haitokaa iwe HURU. Waafrika wanawaamini Wazungu, Wamarekani na Wachina zaidi kuliko wanavyojiamini wao wenyewe....hawajiamini wao wenyewe hata kidogo.


Mtu mweupe anafanya makosa Afrika tena makosa ya jinai ila hakuna hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yake kwa sababu mamlaka za Afrika zinatutazama sisi weupe kama miungu, jambo ambalo liko mbali sana na ukweli.

Mtu mweusi (Mwafrika) anaweza kuteswa, kunyanyaswa na hata kuuawa kinyama Ulaya lakini hakuna mamlaka yoyote ya Afrika inayoweza kuuliza wala kuhoji.

Waafrika wamejikubali na kuamini kuwa wao ni watu DHAIFU wasio na tumaini haswa linapokuja suala la kupambana na Wazungu, Wamarekani na Wachina. Mzungu, Mmarekani au Mchina anaweza kumdhalilisha, kumtukana, kumpiga na hata kumuua Mwafrika katika ardhi ya Afrika tena kwenye nchi yake au nje ya Afrika na Viongozi wa Afrika wataliona hilo na kila mmoja atajiweka kana kwamba hakuona wala kusikia.

Adui wa Mwafrika ni Mwafrika. Mwafrika mpe silaha, pesa au ahadi ya madaraka madogo tu kwa sharti moja tu la kumuua Mwafrika mwenzake, atamuua kinyama kuliko ulivyotarajia. Adui wa Mwafrika sio mzungu, sio Mmarekani wala sio mchina. Adui wa Mwafrika ni AKILI na fikra zake na ndio maana leo Wazungu, Wamarekani, Waarabu na Wachina wameitawala tena Afrika kwa kutumia dini, Elimu, uchumi, teknolojia, siasa na utamaduni.

Waafrika ni watu wanaochukiana na wasioaminiana na ndio maana Afrika haiwezi kuungana na haitokaa iungane kuwa na dola imara. Chuki ya wenyewe kwa wenyewe na utengano ndio inayowapa wakoloni wao nguvu ya kuendelea kunyonya rasilimali za Afrika."

Je unakubaliana na Rais Vladmir Putin?
Je ni kipi unaweza kuongeza kuhusu Afrika?
(Via Remmy Cameroon)

samedi 5 mars 2022

Patrick Mboma secoue la toile en postant une photo de lui et ses filles

L’ancien footballeur Cameroun, consultant chez Canal Plus Afrique, a fait grand bruit en postant une photo de lui à la plage, accompagné de ses jeunes filles.


Cette simple photo du père et ses filles en bikini a suscité plusieurs commentaires sur les réseaux sociaux camerounais et d’autres pages facebook africaines.

Plusieurs internautes trouvent encore tabou qu’un père prenne bain, même à la plage, avec ses filles habillées en petite tenue.


Pour rappelle, le pasteur Moise Mbiye avait aussi fait les frais des critiques après avoir posté une vidéo de lui et sa petite nièce.

Vladmir Putin asema Hakuna World Cup mwaka huu

"HAKUTAKUWA NA KOMBE LA DUNIA MWAKA HUU"...Putin Aionya FIFA kuingilia Mambo ya Kijeshi..


"Msithubutu kuingilia Mambo ya Kijeshi, Bakini kwenye Mpira wa Miguu",...Mkijaribu mjue hakutakuwa na Kombe la Dunia Qatar 🇶🇦. Putin amesema hayo jana akijibu swali la Mwandishi wa habari juu ya Adhabu kutoka FIFA..

"Huyo Mjinga Nani anayesema Russia haitashiriki Kombe la Dunia Qatar 2022?, nasema Russia Lazima Itacheza Kombe la Dunia mwaka huu, Aidha wapende ama wasipende..Sahau kuhusu Mzaha huo..


"Lazima nawaambia Lazima, Wakijaribu kutuzuia Basi wajue Mwaka huu hakutakuwa na Michezo hiyo".

"Sipendi Double Standards za kipuuzi, hayajaanza Leo Mambo haya ya kivita, tumeshuhudia mara nyingi Mataifa ya Magharibi yakivamia na kupigana vita, Vietnam, Korea, Libya, Iraq, Syria, Amerika kusini, kati....na hata sisi akiwemo Ukraine tulipigana vita ndefu Afghanistan 🇦🇫, Sijawahi kuwaona Wala Kusikia FIFA akitenda haya...

Mwamba Anakwambia wachague, Urusi irudishwe, ama Awafanyie Mbaya na Kombe la Dunia lisiwepo...😄😄😄

FOA YA DIAMOND YAZUWA GUMZO

Msanii wa muziki Diamond platnumz ambaye ni Rais wa WCB wiki hii alianza ku-teaser ujio wake mpya wa EP ambayo imepachikwa jina #FOA. Katika ujio huo tumeona branding ya project hiyo kupitia nguo #FOA za rangi ya njano ambazo zimeonekana tayari kuwa gumzo mtandaoni.


Kama utakuwa na kumbukumbu miaka ya nyuma msanii alikuwa akitaka kuachia project ya wimbo au albamu basi ataandaa T-shirt pamoja na kofia kwaajili ya promotion ingawa trend hiyo ilipotea.


Njia hiyo iliwasaidia sana wasanii wengi kwenye promotion ya kazi zao, ambapo mpaka zikazaliwa brand kama African Boy ya Jux, PKP ya Ommy Dimpoz ambazo kwa sasa ni brand chache sana ambazo bado zinaendelea kufanya vizuri.


Diamond kupitia #FOA tayari amekuwa gumzo mtandaoni na huwenda hii ni ishara kwamba amefanikiwa kutengeneza shauku kwa mashabiki wake pamoja na mashabiki wa muziki.


Mashabiki wengi wa muziki tayari wamekaa mkao wa kula kwaajili ya ujio wa project hiyo ambayo bila shaka itakwenda kukata kiu yao.

mardi 1 mars 2022

RAIS WA UKRAINE AKATALIWA KUJIUNGA NA UMOJA WA ULAYA


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, mchana wa leo Jumanne Machi 01, amezungunza kwa hisia kali na Bunge la Ulaya akiliomba likubali ombi la nchi yake kujiunga na Umoja wa Ulaya (European Union) na kushangiliwa kwa nguvu na wabunge hao.


Rais huyo, ambaye katika siku za hivi karibuni ameonekana kama kiongozi mwenye msimamo na ishara ya ujasiri, amezungumza na wabunge hao mjini Brussels Ubelgiji kwa njia ya video akizungumzia kutoka nchini mwake katika mji wa Kyiv.

“Tutashinda, nina uhakika. Ningependa kuwasikia na nyie mkisema kuwa chaguo la Ukraine la kuwa sehemu ya Ulaya, ni chaguo lenu pia. Tunahitaji kuwa wanachama wa Ulaya. Bila ya nyinyi, Ukraine itakuwa mpweke,” aliliambia bunge na kugusa hisia za wabunge wengi ambao walisimama na kumpigia makofi kabala na bada ya kuhutubia.


Katika hatua nyingine, Mkuu wa mambo ya sera za nje wa Umoja wa Ulaya, amekaririwa akisema kuwa ombi la Ukraine la kujiunga na umoja huo linaweza kuchukuwa miaka mingi, hivyo ombi lao la kutaka kukubaliwa kujiunga mara moja haliwezekani, hii ni kwa mujibu wa chaneli ya WION English News

Franck Ribéry afanya ajali

Mchezaji wa zamani wa klabu Bayern Munich, Frank Ribery amepata ajali baada ya gari alilokuwa akisafiria kugonga taa za barabarani.


Ribery (38) aliyekuwa miongoni mwa abiria katika gari hilo ameumia vibaya kichwani na kuwahishwa hospitali.

BOSI WA GSM, GHALIB AFIWA NA BABA YAKE MZAZI


Mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed (GSM) amefiwa na Baba yake, Mzee Said Mohamed ambaye amefariki dunia alfajiri ya leo March 1 2022 na atazikwa leo saa kumi jioni kwenye makaburi ya kisutu Dar es salaam.


Marehemu Mzee Said ni Mfanyabiashara wa muda mrefu Tanzania ambapo alianzisha biashara ya kwanza mwaka 1955 kwa kuuza bidhaa ndogondogo Tanga lakini baadae alihamia kuuza nguo na kuhama kutoka Tanga hadi Songea ambako alijitanua katika kilimo cha korosho ambacho Familia yake imekiendeleza hadi leo.


Inna lillahi wa inna ilayhi rajuun